Kikwete, kigugumizi kitakuisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, kigugumizi kitakuisha lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Aug 23, 2011.

1. Bujibuji

Bujibuji JF-Expert Member

#1
Aug 23, 2011
Joined: Feb 4, 2009
Messages: 35,376
Likes Received: 22,242
Trophy Points: 280
Tangu mwaka 2005 ulipoingia madarakani ulisema majina ya wauza madawa ya kulevya unayo, kwanini hadi leo huwataji licha ya kwamba unawafahamu?

2. GAZETI

GAZETI JF-Expert Member

#2
Aug 23, 2011
Joined: Feb 24, 2011
Messages: 3,563
Likes Received: 1,072
Trophy Points: 280
Labda wanakamatwa kimyakimya.

3. Mwita25

Mwita25 JF-Expert Member

#3
Aug 23, 2011
Joined: Apr 15, 2011
Messages: 3,840
Likes Received: 18
Trophy Points: 0

Kwani wewe ni mtu wa usalama hadi uyajue hayo majina. Uliza nini kinaendelea chini ya kapeti uambiwe.

4. Rejao

Rejao JF-Expert Member

#4
Aug 23, 2011
Joined: May 4, 2010
Messages: 9,239
Likes Received: 245
Trophy Points: 160
Anakusanya ushahidi bado!

5. Son of Africa

Son of Africa JF-Expert Member

#5
Aug 23, 2011
Joined: Jan 16, 2011
Messages: 233
Likes Received: 5
Trophy Points: 0

Kumbe jibu unalo. Uwe unatembelea mahakama ujue yanayojili

6. Son of Africa

Son of Africa JF-Expert Member

#6
Aug 23, 2011
Joined: Jan 16, 2011
Messages: 233
Likes Received: 5
Trophy Points: 0

Utaratibu wa wahalifu...huwa wanarudi katika tukio walofanya kusikilizia nini kimeendelea baada ya uhalifu wao. Kama ulikuwa hujui na wewe umo Majina yako matatu ni...........a.k.a BUJIBUJI

7. Nish

Nish JF-Expert Member

#7
Aug 23, 2011
Joined: Jul 22, 2011
Messages: 732
Likes Received: 0
Trophy Points: 33
maaskofu wameshatajwa

8. s

sanjo JF-Expert Member

#8
Aug 23, 2011
Joined: Oct 29, 2010
Messages: 943
Likes Received: 22
Trophy Points: 35
Mkuu kwani hujui mtaji wa watawala wetu ni kuamini kuwa Watanzania ni wepesi wa kusahau na kusamehe. Unakumbuka matukio yafuatayo?

(1) Ultimatum given to EPA suspect kuwa wasiorudisha pesa za EPA watakiona cha mtemakuni baada ya tarehe 31 October 2009.
(2) Wakazi wa Kimara Kuahidiwa tatizo la maji kuwa historia baada ya Machi 2010.
(3) Nunueni magari wakazi wa Dar es Salaam kwani flyovers zinakuja na foleni litakuwa historia. Ishi Kimara, Mbezi, Kibamba utaelewa gharama halisi ya foleni barabarani.
(4) Marekebisho ya Katiba ya Jamhuri wa Tanzania yanakuja.
(5) Ukosefu wa Madawati katika shule za msingi/sekondari/vyuo.
(6) UKOSEFU WA UMEME-fikiria gharama yake
(7) RUSHWA idara mbalimbali za serikali (Polisi, Ardhi, hospitali (eg. Mwananyamala), Mahakama.
(8) MADINI, BAHARI ZETU, WANYAMA WETU (yote ni shamba la bibi). Wale ambao wametembelea Kahama au Geita watakubaliana nami kuwa madini hayajasaidia na hayatasaidia jamii inayozunguka. WIZI NA UONGO MTUPU.
(9) Vigogo kugawana na kupora ardhi na mali ya umma.
(10) RELI YA KATI kuhujumiwa. Kwa nini strategic infrastructure kama reli umpe mhindi?
(11) Kuuwa TIPER refinery na kutelekeza Depot kubwa kabisa ya mafuta nchi. etc etc

Maswali:
(i) Je tumefunza nini juu ya historia yetu?
(ii) Je tuna viongozi wanaoona mbali? wenye uchungu na nchi hii?

9. RealMan

RealMan JF-Expert Member

#9
Aug 23, 2011
Joined: Nov 9, 2010
Messages: 2,352
Likes Received: 160
Trophy Points: 160
Ushahidi kwamba hakuna kinachoendelea chini ya kapeti ni kuona mateja wakiongezeka badala ya kupungua.
Wala rushwa TRA na Bandarini ambao rais alisema anawajua bado wapo, wanakagua lebo za seat belt ili wakwambie kigari chako ni cha mwaka 80.

Kimsingi wananchi hatuhitaji rais mwenye kujisifu anajua hiki au kile, katiba yetu inampa fursa (kupitia vyombo mbali mbali) kujua karibu kila kitu kinachoendelea nchini, tumempa taasisi ili kwazo aondoe matatizo hayo.

Yule kamanda wa kikosi hicho nae anasema hayo hayo..."tunawajua viongozi wa dini wauza unga"....."baadhi ya viongozi wa Wakatoliki na Bakwata wanatumiwa na wauza unga"... lyrics kama hizi zinasaidiaje kuondoa tatizo???

Tungekuwa na viongozi mahiri tungepeana story tu..."Padri au mchungaji au shehe fulani yuko korokoroni kwa kuhusika na madawa ya kulevya"

Mbona watuhumiwa (masawe, Raymond...) wa ujambazi walifikishwa mahakamani hata pale hapakuwa na ushahidi wa kutosha??

Ukimtetea kiongozi dhaifu ni kuonyesha udhaifu wako...

Loading...