Kikwete: I may be having a smiling face but am firm on issues | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: I may be having a smiling face but am firm on issues

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Najijua, Apr 13, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  I MAY BE HAVING A SMILING FACE BUT AM FIRM ON STRONG ISSUES: ni kauli ambayo mkuu wa kaya alishaitoa mwaka 2006 na ameanza kuitimiza juzi juzi tu baada ya kuamua kumtosa swahiba wake mkubwa ambae wameshatueleza hawakukutana barabarani ila juzi amempa nafasi ya kutafakari na kuchukua uamuzi mwenyewe kabla chama hakijawaonyesha mlango wakutokea
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  unayaamini hayo au unatutaka sisi tuyaamini tu!?
   
 3. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kama tukiwa na viongozi kama huyu wa kutoa Kauli kisha aanze kuitimiza 6yrs later basi katiba mpya impe Rais fursa ya kutawala miaka 20 iliyogawanya ktk mihula miwili.
  Kwa hiyo aliyoahidi kwenye kampeni 2010 (meli ziwa victoria, meli ziwa nyasa, u/ndege Bukoba, treni iendayo kasi, barabara za juu, machinga kompleksi n.k) yatatimizwa na nani maana anamaliza urais wake 2015.
   
 4. B

  Blande Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  every step starts wit one step
   
 5. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Alipoingia madarakani JK alisema katika hotuba yake Bungeni baada ya kuchaguliwa kuwa rais kwa mara ya kwanza kwamba watu wasihadaike na tabasamu lake la muda wote kwani yuko "firm on issues".
  Sikuwahi kufikiria sana msemo huu lakini leo katika somasoma zangu nimekutana na maana ya neno firm katika Oxford Advanced Learner's Dictionary 7th Ed pale lilipotumika kama adjective (sawasawa na alivyolitumia JK) linamaanisha yafuatayo:-
  1. fairly hard; not easy to press into a different shape.
  2. not likely to change
  3. strongly fixed in place. SECURE.
  4. strong and steady
  5. strong and in control

  Ukifuatilia kwa makini utawala wa JK utagundua huyu Mh. Dkt ni madhubuti katika anayoyaamini na hawezi kubadilishwa na pressure zozote wala kutoka mahala popote. Jaribu kutafakari tabia zake katika malalamiko ya baadhi ya watu kuhusiana na haya yafuatayo na madai ya kumtaka abadilike na upime kiwango chake cha kubadilika.
  • Serikali kubwa aliyoiunda na kubeba mawaziri 60.
  • Matumizi ya magari ya kifahari yanayoligharimu sana taifa.
  • Safari kibao za nje ya nchi hasa Marekani bila kujali hali ya taifa kifedha.
  • Kuwafumbia macho mafisadi hasa rafiki zake vs madai ya wananchi kumtaka awabane.
  • Ufahari mwingi wa serikali kuliko kazi.
  • Madai ya wananchi kushinikiza baadhi ya viongozi wavuliwe madaraka kama DC Mabiti aliyekuwa Tarime ambaye sasa ni RC Simiyu, Andrew Chenge wakati wa issue ya rada, Waziri na Naibu Waziri wa Afya hivi juzijuzi nk.

  Haya ni machache tu katika mengi lakini pressure zote hizo zinaonesha jinsi JK alivyo madhubuti katika kuendeleza yale yanayomfanana na kuyaamini yeye. JK habadilishwi na lolote na wananchi wenye hekima zenu zoeeni hilo na muishi nalo. Our president is Firm on Issues.
   
 6. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Good analysis, big up and your right sir
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  vipi kuhusu suala la katiba mpya?
   
 8. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Anataka swala la uraia wa nchi mbili liruhusiwe tangu Katibani na si pale wizarani kwa Membe tu. Katika swala hili unajua watafaidi asilimia ngapi wa waTZ wa kawaida? Watu watakaofaidi kutokana na kuwa na passport za nchi zaidi ya moja baadhi yao tayari wanazo na wanaendelea kukwapua fedha kibao wakisaidiwa na viongozi wetu. Baadhi yao ni matajiri sana kiasi kwamba hata katiba isiporuhusu bado wanao uraia wa aina hiyo.
  Ukiondoa maslahi ya matajiri wasiokuwa waaminifu na wanasiasa raia wa kawaida watakaonufaika na hili sidhani kama wanafika hata laki.
   
 9. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Umechambua vizuri Mkuu....
  Bila kusahau suala la Madaktari wetu na sekta nzima ya afya kwenye mgogoro wa juzi...
  Ametuonyesha jinsi alivyo "firm" pale alipowakatalia Mponda na Nkya wasijiudhuru nyadhifa zao kuokoa maisha ya WATU.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  The Analyst.....
  unatakiwa uandike kitabu kuhusu utawala wa JK.......
  sijui title utaaiitaje....lol
   
 11. T

  Topical JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar mfupa uliowashinda wengi

  Vipi kuhusu kuwapeleka Mahakamani Mawaziri na Katibu wakuu mfupa uliowashinda wengi..

  Vipi kuhusu .....
   
 12. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Unaweza kushindwa kuamini ukweli huu, pamoja na kumtabiria anguko kwa kutochukulia hatua baadhi ya mambo mazito JK bado anapeta tu na anaendelea na smile yake almost muda wote. Richmond, DOWANS, EPA (Kagoda) na yote ambayo amepuuza maoni ya watu wakweli takriban wote ndani na nje ya nchi waliomsisitiza achukue hatua, yanaendelea kusahaulika kwa show off zinazoibuka kila kukicha.
  Unaikumbuka ile ya miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika? Inadaiwa imekula billions kibao halafu mwezi huo huo mishahara ya watumishi wa serikali ikalipwa kutokana na mikopo ya benki za hapa nchini (Inasemekana).
   
 13. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mgogoro wa Zanzibar ulikuwa mpango wa Amani na Seif + wazanzibari wanaoijua pesa. Mgogoro wa Zanzibar haukuwa na maslahi kwa biashara ya utalii biashara ambayo ukiwaulizia wazanzibari watakwambia ilivyokuwa na umuhimu kwa uchumi wa visiwa hivyo na kwa Rais Mstaafu Amani mwenyewe.
  Mawaziri waliopelekwa mahakamani walikuwa wanamuunga mkono mgombea tofauti na wanamtandao so it is another show off isiyo na deal. Usishangae ikaishia watu kuachiwa huru. Kwa mwenye nia ya kuthubutu Kagoda isingechomoa kirahisi wala DOWANS.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Topical,
  Mawaziri gani unaowazungumzia wewe? Unazungumzia Mramba na Yona? Mbona hawa hawana kesi za kujibu?
  Mramba yuko mahakamani simply because alimpunja Kikwete mgao kwenye lile dili la Alex Stewart.
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Aisee dowans si umeondoka na PM (rafiki yake) ulifikiri bila kuwa firm angeweza kubaki na PM wake..lakini anafuata sheria ukiboranga unaondoka..

  Hizo ni romuors tu, kama hawana kesi ya kujibu itakuwa kosa la mahakama na wanasheria wetu (ukosefu wa uzalendo) na si JK
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Siyo kweli,

  Nazungumzia Mramba, Yona, Mgonja, Liyumba et al. JK hana muda na hizo dili mkuu..

  Wakishindwa kutiwa hatiani tuwabane uzalendo wa wanasheria wetu si JK..
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kama watu wanamwelewa JK ni kuwa
  yoote anayoyafanya ni kwa mujibu wa upeo wake....
  anaamini yuko sahihi kwa kila anachofanya.....
  haoni kwamba anakosea....na anaona wanaomkosoa hawamuelewi
   
 18. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kaka hufuatilii mambo? DOWANS kuvunjiwa mkataba (pamoja na madai ya wananchi wengi kudai uvunjwe) ulivunjwa kwa kuwa kulishaonekana mwanya wa kupata fedha zaidi kuliko ungesubiri kumalizika time. TANESCO walipokata rufaa swala la ufake wa Richmond halikuwasilishwa mahakamani ili DOWANS wapate mwanya wa kushinda na ikawa. Mwanasheria wa TANESCO alikuwa mwajiriwa wa Rostam (Voda) hadi miezi kadhaa iliyopita sawa na Waziri wa Wizara hiyo kabla ya kuingia Bungeni. Ndiyo maana Ngeleja alikuwa wa kwanza kushangilia malipo mapya ya DOWANS na sasa inadaiwa bado TANESCO wanaweza kukata rufaa kupinga kufanya malipo hayo jambo ambalo litawaongezea ulaji watakaposhinda mwishoni. Hujui serikali yetu kwa maana ya wakubwa wanapata zaidi DOWANS ikishinda kesi kuliko ikishindwa?
   
 19. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  We jamaa ni bonge la mwandishi inabidi ufanyie kazi wazo la mkuu wangu TB (The Boss).....

  Kwa kurudi kwenye hiyo post yako, nadhani kinachoendelea kumuweka mheshimiwa pale magogoni, jibu lake lipo kwenye signature yako...

  "Viongozi Dhaifu na Mafisadi + Wananchi wavivu, walalamishi na wasiojua haki zao + Imani Iliyopotoshwa = Umasikini wetu."

  Ila tunaweza kurekebisha (kuhariri) kidogo huo Mlinganyo.....
  Hapo kwenye "Viongozi Dhaifu" tuweke iwe "Mfumo Dhaifu"
  Na hapo kwenye jibu la mwisho badala ya Umasikini wetu (hilo halina shida linafahamika) tuweke "Kikwete kuendelea kubaki Ikulu yetu"
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  katika tanzania hii ni serikali ya kikwete pekee ndio imeonyesha kwa vitendo jinsi inavyopambana na mafisadi wakubwa mf.mramba,yona,liyumba nk
   
Loading...