Kwa hiyo umempima Lowassa kwa kigezo kimoja tu cha kuwa na hubris. .
Hubris ni hulka ya mtu binafsi, hulka inayotaka kutuingiza vitani kutetea maslahi ya nchi hiyo sio hubris, huyo mtu ni foreign policy hawk..
Wapo tunaotaka foreign policy hawk sawa sawa na alivyofanya Lowassa kutaka kufutilia mbali mkataba na Wamisri kwamba sisi tusitumie maji ya lake Victoria eti kwa sababu yanaenda Misri. ..
Tishio la vita na Malawi sio katika issues za kitaifa zinazojadiliwa katika uchaguzi wa rais ajaye. .
Afya na umri wa wagombea wanaoongelewa, mitazamo yao kuhusu Katiba mpya na Muungano, matatizo ya nishati ya umeme, thamani ya shilingi, soko la mazao ya wakulima, mustakabali wa uwekezaji wa nje haswa unaoondoa raia kwenye maeneo yao, rushwa ofisi za juu, ajira za vijana (wazee hawaongelewi), ujangili na ujambazi, mustakabali wa matarajio ya neema ya gesi na mafuta (kama kuna neema kweli), migogoro ya ardhi na umaskini wa Watanzania kwa ujumla, ndio baadhi ya masuala yanayoongelewa au yanayotakiwa kuwa msingi wa kuchambua wagombea kujua nani atakuwa bora ya Kikwete. Lowassa na wenzake wote tuwapime kwa hayo..
Sio hubris ya Lowassa kwa sababu eti atatuingiza vitani, hofu ya uwezekano wa vita na Malawi haupo kwenye gumzo la kitafa.
Taifa hili linakazi hata majuha nao wanahoji utendaji wa jk,kwa tarifa tu ni kwamba jk kila siku anasema mda wake ukiisha ataondoka kwa mujibu wa katiba ila kumbuka kuwa hatakuja kupatikana kirahisi mtu mpenda maendeleo kama jk japo wajinga wachache kama wewe akina mengi na mafisadi wengine ndiyo wanamkwamisha lakini hachoki kuleta maendeleo kwa watanzania.
Wapo watakao tofautiana na mimi kimtizamo lkn wenye positive mind watakubaliana kuwa JK hakupaswa hata kuwa katibu taarifa,hana kipaji cha uongozi,mtaakubaliana na mimi kuwa serikali ya kikwete imekua ikikumbwa na dhoruba nyingi kuliko awamu nyungine zozote,mfano richmond,operation tokomeza,iptl na Escrow,mpaka sasa hakuna action zaid ya wahusika kujiuzulu,Jk rais wangu utakumbukwa kwa lipi kwenye uongozi wako? Awamu yako imeuza kila kitu gas,madini,uranium,bandari nk ni nini hatma ya kizazi kijacho? Vijana wengi waliohitimu vyuo watakwenda wapi kama uwekezaji unaofanyika hautoi fursa za ajira? Ni awamu hii tumeshuhudia utekaji,utesaji na hata kuuwawa kwa watz wenzetu walioamua kupaza sauti zao kwa kuonyesha udhaifu,ubadhirifu wa serikali yako,tumeshuhudia jinsi familia yako kupitia mkwe wako ndg albert marwa,ridhwani kikwete na wengine wanavyotumia taasisi ya rais kufanya ubadhirifu ilihali ofisi yako ikiwa kimya,uliwahi kusema nanukuu"urais wangu hauna ubia ba mtu" lkn mh rais ni nini tafsiri ya kauli hii kwa kipindi hiki nchi ikiwa njia panda? Bado huna mbia kwenye urais wako? Ni ukweli ulio wazi sasa kuwa urais una ubia na watu mfano familia yako,albert marwa,rostam aziz and coy,home shopping center,patel na wengine wengi,sina hakika kama ulikuwa na tafsir kamili ya neno ubia lkn bado naamini umeganda kwenye tope
ambalo kamwe huwezi kutoka kwa sababu urais wako una ubia na wabadhirifu na wezi wa mali za umma,sitaki kuamini kuwa singasinga ambaye kenya yuko black listed mmeleta kuja kufanya ubadhirifu kachukua pesa kaondoka,nchi yetu watu wake ni masikini sana pamoja na utajir mungu aliotujalia,mh rais nimalizie kwa kusema nimechangia ujenzi wa maabara ilihali tusikia huko dsm wanabeba pesa kwa viroba,je ipo wapi haki hapa?
Mungu ibariki Tanzania
Kwakuwa imebaki miezi michache kabla ya JK kumalizia madaraka yake basi hatuna budi kusubiri walengwa wa ESCROW kuondoka naye.
Kuvunja baraza la mawaziri kwa sasa ni gharama kwa wananchi.
wahusika wamalize muda wao halafu ndio wahukumiwe ikiwa ni pamoja na kurudisha fedha zetu.
wahisani tusameheni kwa muda huu msitubanie sana kwani tunaoumia ni sisi wananchi.
Natamani ingekuwa wiki Moja! Ufisadi umekithili, umasikini umejenga kibanda, hali ni mbaya kuliko hapo kwanza alipochukua nchi.
Wapi nimekwambia hivyo?
Unapimaje kwamba Lowassa hatatuingiza vitani kwa kukosa kiasi na hubris na atatuingiza kwa maslahi ya nchi?
Lowassa alishindwa kuongea na wakuu wa wilaya tu kama kiongozi anayethamini "collective responsibility" na mutual respect ethics of leadership, ataweza "foreign policy"?
Tanzania tuna "foreign policy" zaidi ya boilerplate outdated directionless Nyerereism?
Lowassa kwanza hiyo kazi hata hajafanya yeye, yeye kachukua credit tu. Kazi kubwa kafanya Anthony Diallo. Talk about when opportunism meets ignorance.
Even more reason to support my assertion that we are going downhill. The populace itself is not imaginative, how do you expect sharp candidates?
If one cannot chew gum and walk, of course adding one item to your laundry list will cause a doomsday scenario.
Kwa nini mimi niende tu na yale yaliyopo kwenye gumzo la kitaifa? Yale yaliyopo kwenye gumzo la kitaifa leo hayajawa na mwanzo pale ambapo hayakuwapo katika gumzo la kitaifa? Kwa nini una limit nini kinafaa kuzungumzwa na nini hakifai kwa msingi wa "gumzo la taifa"?
Hili "gumzo la taifa" ni la taifa gani hili ambalo mwananchi wake hawezi kuongezea kitu?
Kwa nini tishio la vita Malawi lisiwe mfano tu unaoonyesha suala zima la Lowassa kukosa kiasi na kuongoza nchi kwa munkari, jazba na inda iliyojaa kiburi cha ujuaji asionao?
Mungu AKULINDE SANA .
HAYA NDIO MAMBO MAZURI ALIYOFANYA KWENYE UTAWALA WAKE AMBAYO WATANZANIA HAWATASAHAU SOMA HAPA KUJUA ZAIDI
HUKU zikiwa zimebaki miezi michache tu ili Rais Jakaya Kikwete kumaliza vipindi vyake vya miaka kumi alivyokuwa mpangaji wa ikulu,hayo ndio baadhi ya mambo mazuri ambayo yatamfanya akumbukwe daima kwenye utawala wake
1. Ujenzi wa Sekondari za Kata ni maamuzi sahihi ingawa yana changamoto zake zinazoweza kutatuliwa na watakaomfuatia, lakini hapa JK ametumia madaraka yake vizuri
2. Ameendelea na uendelezaji wa Miradi ya Barabara, suala lililoanza kujitokea wakati wa awamu ya 3, JK ameendelea nalo suala hilo kwa kasi kubwa na kwa kipindi chote
3. Daraja Kigamboni, Malagarasi na Kilombero ni miongoni mwa mambo yatakayokumbukwa forever
4. Ongezeko la Taasisi za Elimu ya Juu limefanyika vizuri sana katika awamu ya Kikwete, mbali na UDOM lakini taasisi na vyuo vingi vimeimarishwa, kupandishwa hadhi na vyuo vingi binafsi vimeanziswa. Kwa sasa Taifa haliko tena na dhana ya UDII, Mzumbe na SUA. Aidha ari na moyo wa watanzania kulipia huduma za elimu umeongezeka.
5. Kumekuwa na ongezeko kubwa la ajira ukilinganisha na awamu mbili zilizomtangulia. Mkapa aliendesha Serikali nyembamba, suala ambalo ni zuri lakini lina changamoto zake kwa wale waliokuwepo wameliona hata akapewa sifa ya mzee wa "ukapa"
6. Mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara kwa lengo la kutatua kero ya Umeme ni hatua nzuri ambayo haijawahi kufanywa katika awamu ya 2 na ya Tatu (Vyanzo vya Nishati)
7. Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Chuma (Kule Liganga?) ambao maandalizi ya ujenzi wake yamekamilika ni hatua nzuri ili kuvutia au kuanzisha uwekezaji wa zana za Chuma pamoja na Viwanda vikubwa.
8. Hatua ya Kujenga Bandari mpya eneo la Bagamoyo yenye hadhi ya 4th Generation ni tukio litakalokumbukwa na vizazi Dahri vijavyo.
9. Hatua ya Utekelezaji wa mradi wa DRT ambao ulikuwepo miaka mingi pia ni miongoni mwa mazuri yaliyotendeka katika awamu ya JK
10. Zoezi la kutambua na kuwarudisha kwao wahamiaji haramu pia ni zoezi zuri ambalo bila shaka halijawahi kufanywa katika uongozi wa awamu nyinginezo kwa kiwango na utashi wa namna hiyo
11. Kitendo cha utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya Taifa ni credit kubwa kwa JK ambao hakuna sababu za wazi kwanini nchi imekaa miaka 50 pasipo na vitambulisho vya uraia kwa wakazi wake na raia wake
12. Ameendelea kuiweka Tanzania kwenye mahusiano mazuri kimataifa hususan SADC, UN na nyanja nyingine za Kitaifa. Ukiacha EAC ambayo sababu za kuzorota kwake ziko wazi, lakini maeneo mengine ame-play well.
Huyu kingunge nini?1Tatizo sikubaliani na kuwapo kwa mungu.
Taifa hili linakazi hata majuha nao wanahoji utendaji wa jk,kwa tarifa tu ni kwamba jk kila siku anasema mda wake ukiisha ataondoka kwa mujibu wa katiba ila kumbuka kuwa hatakuja kupatikana kirahisi mtu mpenda maendeleo kama jk japo wajinga wachache kama wewe akina mengi na mafisadi wengine ndiyo wanamkwamisha lakini hachoki kuleta maendeleo kwa watanzania.
Watanzania wazalendo wanaopenda maendeleo, wanatamani JK aongezewe miaka mingine mitano ili aendelee kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Sijui wewe mleta mada uko nchi gani!
Huyu kingunge nini?1
WE WISH ANGEPATA MIAKA MINGINE KUMI
TUNAMHITAJI sana, amefanya kazi sana kuimarisha miundombinu kama mabarabara, madaraja, mahosipitali, mashule, mavyuo n.k. hakuna rais yeyote kabla yake aliyewahi kufanya aliyoyafanya Kikwete. Pili kuhusu kuuza rasilimali zetu, mkapa ni kinara (kama wewe ni wa ile dini ya escrow huwezi ona hili) kauza, NBC, Tanesco, na mashirika karibia yote ya umma tuyajuayo (kama hujui sema nikutajie), migodi mingi imeuzwa na mkapa na ndo muanzilishi wa sisi kupata 3% tu kwenye mapato hayo. lakini pia uongozi wake uligubikwa na kashifa nyingi ila hakukuwa na uhuru wa vyombo vya habari kama tuvionavyo kipindi hiki. kulikuwa na scandal kama za EPA, mwananchi gold, radar, ndege ya rais, meremeta, kujiuzia mgodi wa kiwira, kujianzishia benki iitwayo anaben, rushwa za kajengo BOT, alex and stewart na upuuzi mwingi ambao sina muda wa kuulist hapa.
Sema unamhitaji weweJK aongezewe miaka mingine mitano. Watanzania tunamuhitaji sana