Kikwete au hoseah nani kujiuzulu?

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Kutokana na habari zinazoendelea ni wazi kabisa hakuna uwezekano wa kikwete na hoseah kufanya kazi katika serikali moja. kwani kama yaliyosemwa na hoseah ni kweli basi kikwete anatakiwa kujiuzulu na kama si hivyo basi kikwete ni dhahiri atamuwajibisha hoseah.............
je ni nani kati ya watu hawa ataondoka katika kiti chake?
 
Hosea yeye aliongea ukweli mtupu kwa vile alipewa huakika kwamba maneno yake yatakuwa siri kati yake na wamarekani.Sasa maneno yameanikwa na wikileaks Hosea kaona bora hakanushe maneno yake hili aweke uhusiano na bosi wake vizuri.

Kuhusu nani ajiuzuru tunapoteza mda wetu mafisadi wangapi wanaendelea kushika nafasi zao?
 
Hakuna Kiongozi hata mmoja wa Tanzania mwenye aibu mara afanyapo madudu! Hivyo kujiuzuru ni ndoto kwa watu walioingia kwaajili ya maslai yao binafsi. Unafikiri kuna mwenye uchungu hata mmoja hapo na Shutuma walishazoea kwao ni kama kumpigia Mbuzi Gitaa acheze!
 
Hosea yeye aliongea ukweli mtupu kwa vile alipewa huakika kwamba maneno yake yatakuwa siri kati yake na wamarekani.Sasa maeneo yameanikwa na wikileaks Hosea kaona bora hakanushe maneno yake hili aweke uhusiano na bosi wake vizuri.

Kuhusu nani ajiuzulu tunapoteza mda wetu mafisadi wangapi wanaendelea kushika nafasi zao?

Hakika mazungumzo ya Hosea na yule Mmarekani yalikuwa ni ya siri. Na katika siri mtu anaongea kile anachoamini ni ukweli. Hosea akatoa yote anayoyajua (ukweli) akijua kwamba ni siri kati yake na mmarekani. Na kweli imekuwa ni siri mpaka hapo wajanja wa wikileaks walipoyatoa hadharani. Bila wikileaks haya mambo yangebaki ni siri; wala serikali wala wananchi wasingejua kitu. Big up wikileaks!
 
Well kama hosea atasimamia ukweli ya alichokisema basi Kikwete inabidi ang'oke kwa kutokuwa na dhamira safi ya kuwachukulia hatua mafisadi. Lakini kwa kuwa hosea ameanza kuogopa na kuikimbia dhamira yake basi hofu hiyo itamwandama hadi kukosa ujasiri na hatimaye kung'olewa katika madaraka yake bila support ya jamii.
 
Hosea sio msafi na hivyo hawezi kuthubutu kusema ukweli......kikwete hata weza kumtimua hosea kwasababu kufanya hivyo nikuthibtisha kauli ya hosea ambayo tayari kisha ikana na kumuweka kikwete pazuri kwa wadanganyika..........hivyo wote watabaki na kuendeleza mapambano dhidi ya ukombozi ili watawale milele
 
jambo kubwa si usafi wa hoseah bali rais kuingilia mapambano ya vita dhidi ya rushwa, nadhani tume huru ingeundwa kuchunguza ukweli wa mambo na ikidhibitika sheria na uwajibikaji uchukue mkondo wake
 
Kutokana na habari zinazoendelea ni wazi kabisa hakuna uwezekano wa kikwete na hoseah kufanya kazi katika serikali moja. kwani kama yaliyosemwa na hoseah ni kweli basi kikwete anatakiwa kujiuzulu na kama si hivyo basi kikwete ni dhahiri atamuwajibisha hoseah.............
je ni nani kati ya watu hawa ataondoka katika kiti chake?

Mkuu,

Tanzania hakuna ustaarabu, utaratibu wa kuwajibika au kuwajibishwa.
Linalofanyika ni kukuhamisha kutoka sehemu moja kwenda nyengine na mara nyingi huwa ni kukupandisha cheo.

Wakikuchoka sana sana wanakumaliza, story inaisha.

Ile ya Lowasa ilikuwa geresha b.w.e.g.e, funika komba, si unaona anavyopigania arudi? Na akirudi anataka nafasi ya juu zaidi. Sasa tukae vizuri au tutaona maigizo kuliko maigizo!

Kwanza ndiyo hivyo wanazitaka bilioni ngapi vile?
 
Ikulu inatakiwa itoe tamko kujibu tuhuma za Mh JK. Kama ni uongo basi hao wikileaks washtakiwe kwa uchochezi ili tulipwe fidia. Kukanusha peke yake haitoshi hasa kama una uhakika na unachokitetea
 
Kutokana na habari zinazoendelea ni wazi kabisa hakuna uwezekano wa kikwete na hoseah kufanya kazi katika serikali moja. kwani kama yaliyosemwa na hoseah ni kweli basi kikwete anatakiwa kujiuzulu na kama si hivyo basi kikwete ni dhahiri atamuwajibisha hoseah.............
je ni nani kati ya watu hawa ataondoka katika kiti chake?

Both kwani wame misuse the Tanzania Constitution wametufanya sie wadanganyika kweli
 
hii ni bongo kaka,hakuna wakujiuru hapo,kama ni hivyo hosea angejiuzuru kitambo tu lakini mpaka leo anapeta,waarabu wapemba hujuwana kwa vilemba
acha waibe bwana
 
Back
Top Bottom