Kikwete ateta na Mshauri wa Trump

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,931
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo na Bw. Massad Boulos, Mwanadiplomasia na Mshauri Mwandamizi wa Rais wa Marekani, Donald Trump anayeshughulikia masuala ya Nchi za Afrika, Uarabu na Mashariki ya Kati.

Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Oslo Forum 2026 unaoendelea jijini Oslo, Norway, kuanzia leo Juni 10 hadi 12, 2026.

Mkutano huo umewakutanisha Viongozi, Wanadiplomasia Waandamizi na Wataalamu wa masuala ya amani na usuluhishi kutoka Nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kujadili changamoto za usalama, diplomasia na juhudi za kuimarisha amani katika maeneo mbalimbali ya dunia.


​
 
well done Jakaya Mrisho Kikwete, retired President of United Republic of Tanzania,

unafanya kazi nzuri na kubwa sana baba kwa maslahi mapana ya Taifa hata baada ya kustaafu
 
Huyu mzee alitakiwa awe Rais mpk leo hii badilishabadilisha haina maana wala faida yyte
 
 
La kuvunda halina ubani, huyu mzee ana mchango mkubwa kwa maafa ya 29.10.2025
 
Kila mtu anataka kuuza tanganyika yetu chura aka kizimkazi amepata URUSI na JK amepata U.S.A mwenye Dau kubwa auziwe tu.watanganyika hawajielewi.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…