Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Katika habari ile ya daily news yenye kuelezea michango aliyotoa Kikwete na wenzake kusaidia ccm Mara, kuna quote kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amesema yafuatayo:
Kwanza, Kikwete anatumia reference gani kusema kuwa ccm ndiyo chama pekee kilichotibitisha kuwa kinaweza kuchangia amani? Hii ina maana kuwa kuna vingine vilivyopewa madaraka na vikashindwa kutunza amani?
Pili, Kikwete anatumia kumbukumbu (reference) gani ya neno amani wakati historia inaonyesha mauaji ya kikatili yaliyofanywa dhidi ya watanzania wa Pemba na Mwembechai?
Tatu, Kikwete anatumia tafsiri gani ya neno amani iwapo mamilioni ya watanzania hawana uhakika wa kupata hata mulo mmoja wa siku, maji safi, umeme, mawasiliano, na mengine mengi? ni amani ipi hii anayosema?
Zaidi pia, ina maana Kikwete anasema kuwa usipochangia ccm basi unachangia kinyume cha amani? Hii statement ina tofauti gani na ile iliyotolewa na jeshi la zimbabwe kuwa kuchagua upinzani ni kuvuruga au kutishia usalama wa taifa?
Hii ni habari nzito sana na inabidi Kikwete au wasaidizi wake waitolee ufafanuzi na ikiwezekana kuwaomba msamaha watanzania wa Pemba na mwembechai waliopoteza maisha ya ndugu zao wakati wa ukosefu wa amani uliofanyika chini ya serikali ya ccm!
Inabidi pia Kikwete awaombe msamaha wananchi wa Kigoma ambao wamekosa amani kwa miaka yote hii kwa kutokuwa na mawasiliano ya uhakika na wenzao katika sehemu zingine za Tanzania!
Ni jumapili kwa hiyo niko limited kidogo (nachukua off kufurahia maisha mafupi niliyonayo) so mengine zaidi ya uvunjifu wa amani yaliyofanywa kuanzia miaka ya Nyerere, Mwinyi, hadi leo yatakuja na kuendelea hapa rasmi kesho!
Taarifa hiyo ilisema Rais Kikwete alihamasisha uchangiaji kwa kusema kuwa CCM ni chama kilichothibitisha kuwa kinaweza kutunza amani na hivyo kuchangia chama hicho ni kuchangia amani ya nchi.
Kama mnavyojua ndugu zangu, chama chetu ni chama ambacho kimedumisha amani ya nchi hii, hivyo hata kwa wafanyabiashara kuchangia CCM ni kuchangia amani na hakuna lolote, ikiwamo biashara inayoweza kufanyika bila nchi kuwa na amani, kwa hiyo nawaombeni ndugu zangu kuchangia chama chetu, alisema.