Kikwete anaiogopa CHADEMA?

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,597
1,005
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimeendelea kuwa tishio kwa ccm baada ya Rais kikwete kuogopa kuteua mbunge kutoka ndani ya chama hicho. Je kwa kuogopa huko ni dalili ya chama hicho kuwatishio kwa ccm?.

Bunge lilopita aliteua Jusa kutoka cuf, na cuf walikuwa chama kikuu cha upinzani.
Najua raisi anaweza kuchagua kutoka chama chochote lakini kushindwa kuteua kutoka cdm nadhani amedhihirisha kuwa cdm ni chama chenye kutishia uwepo wa ccm.
Nawasilisha
Maoni haya ni ya mlala hoi!.
 
Bwana Bangoo. Tanzania ukitaka kupewa cheo inabidi uwe kibaraka, mnafiki na mbabaishaji. Ukiwa mkweli na mchapa kazi huendi popote. Mifano ipo mingi ... angalia kina John Cheyo, Augustine Mrema, na James Mbatia nasikia ameteuliwa kuwa mbunge nk nk nk....
 
Upinzani sio uadui mkuu wala kupinga kila kitu!

Sasa kuna vyama tanganyika viongozi wake wanadhani kuwa mpinzani maana yake we uwe against na kila linalofanywa

na serikali hilo ndio tatizo la hao CDM, tofauti n vyama vingine ambavyo katika baadhi ya masuala yenye manufaa na

taifa wanakubaliana na serikali au wanatoa maoni yenye kuboresha CDM yenyewe imejengeka katika mfumo wa kupinga

tu.

Sasa katika hali hiyo usitegemee atokee mbunge wa kuteuliwa toka kwa hawa watu.
 
Sipati picha!! ikiwa waliochaguliwa kwa kura halali za wananchi anawatengua ubunge kwa kutumia mahakama atatoa wapi nguvu ya kuteua mbunge toka cdm! labda ale mavi!!
 
Watanzania wanaelewa chama kipi hakipendi wizi unaofanywa na ccm
 
haya mazingira Jk anayotengeneza yanaweza yakaleta serikali ya mseto 2015
 
Kwani unataka akakiri mara ngapi zaidi ya kukusanya vyama vyote vya upinzani kwa upande wa CCM?

NCCR-Mageuzi, chama mwana-mpotevu, sasa kimerudi rasmi tena bila kificho nyumbani kwa baba yao wa UFISADI mheshimiwa CCM sawa tu na wenzake UDP, DP, TLP na CUF na tangu sasa wananchi kote nchini sasa tunaelewa leo kuliko hapo jana kwamba chama cha kweli cha upinzani chenye kubeba matumaini ya WaTanzania kujinasua toka lindi la UFISADI ni chama gani - jibu zuri unalo wewe hapo!!

Lakini kosa kubwa analolifanya ni kule kujisahaulisha kwamba vyama hivyo siku nyingi sana havina wanachama hai zaidi ya kuwa simba mkali ndani ya ki-brief case ya huyo huyo mbebaji na familia yake (Cheyo, Mrema, Lipumba, Mtikila aka Mzee wa loose balls na sasa Mbatia).

CDM ongezeni kasi kupitia M4C kila kona ya nchi hii maadam ANTIREFORMISTS sasa wameamua kurundikana pamoja bila kificho tena mchana kweupe wanafiki wote haoooo!!
 
Hivi ingekuwa dr Slaa ndiyo kateuliwa au Lipumba angekubali kuwa mbunge wwakuteuliwa?
 
cdm ni majembe hatutegei kuteuliwa. Tutapambana kwenye majukwaa
 
ccm wakiwapa cdm nafasi za uwaziri ndio kabisa ni kama wanawasafishia njia ya kuingia ikulu kwa sababu cdm wataanza kupata experience ya kuongoza wizara na serikali kitu ambacho ccm hawataki hata kwa dawa...wanajua nccr cuf hawawezi kuchukua nchi.

Bt rais anavyofanya kuangalia talent kwenye vyama mbalimbali ni nzuri...kuna wasomi na wachapa kazi kwenye upinzani sio mbaya akiwachagua kufanya kazi..mwisho wa siku sisi wote ni watanzania na tunataka maendeleo ya nchi yetu regardless mtu anatokea chama gani
 
Upinzani sio uadui mkuu wala kupinga kila kitu!

Sasa kuna vyama tanganyika viongozi wake wanadhani kuwa mpinzani maana yake we uwe against na kila linalofanywa

na serikali hilo ndio tatizo la hao CDM, tofauti n vyama vingine ambavyo katika baadhi ya masuala yenye manufaa na

taifa wanakubaliana na serikali au wanatoa maoni yenye kuboresha CDM yenyewe imejengeka katika mfumo wa kupinga

tu.

Sasa katika hali hiyo usitegemee atokee mbunge wa kuteuliwa toka kwa hawa watu.

CDM si CCM B. Unataka CDM wakubaliane ufisadi, kulindana na kutumia hovyo hovyo rasilimali za nchi? Hilo ni hapana siku zote.
 
Ama kweli baada ya mbatia kuwa kibaraka wa muda mrefu wa ccm apewa fadhila zake!
 
cdm hatuna mda na kuhongwa ubunge,yetu ni pipooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooz
 
mfitinishaji hawezi chagua People's power maana inaweza kumuondosha madarakani
 
TAIFA SASA LINASUBIRI KUONA KATI YA MBATIA NA KAFULILA NANI NI KIBARAKA ZAIDI KWA CCM UKIZINGATIA UNDANI WA MZOZO WAO CHAMANI MAPEMA MWAKA HUU?

Mara baada ya kukiua kile chama kilichokua maarufu sana kule visiwani Zanzibar, CUF, sasa Mhe Kikwete kaonelea hata Bara CCM hakifi peke yake hivihivi. NCCR Mageuzi kwishney!!!

Chama hiki cha NCCR Mageuzi sasa kimerudi RASMI nyumbani kwa baba yake CCM kwenda kugawana mabua dam dam.

Sasa tunasubiri kuona udhati wa kile alichokua akikiping David Kafulila je ataendelea kushiriki na Mhe Mbatia kula vya UKIBARAKA KWA CCM au sasa ataachia ngazi kulinda heshima na msimamo wake hapo nyuma kidogo?
What? Mbatia?....kweli nimeamini Mbatia na NCCR yake ni kibaraka wa ccm
Na sasa naamini CDM ndicho chama cha upinzani wa kweli Tanzania. Kazi ipo!
 
Kikwete huwa hateui kwa kufuata weledi, anaangalia Technical Know Who.

Mbatia aliyekataliwa na wananchi ndani ya sanduku la kura kumpa ubunge ni kuchezea nafasi. Wana CCM wazembe ndio waliobadili katiba kuruhusu huu upuuzi
 
Dah thread nyingine bwana, yaani kwa akili zako, Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuogopa chama cha vilaza kama Chadema?.
.
"Ama kweli CHADEMA NI SAWA NA NG'OMBE ASIYE NA BEI SOKONI".
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Back
Top Bottom