Upinzani sio uadui mkuu wala kupinga kila kitu!
Sasa kuna vyama tanganyika viongozi wake wanadhani kuwa mpinzani maana yake we uwe against na kila linalofanywa
na serikali hilo ndio tatizo la hao CDM, tofauti n vyama vingine ambavyo katika baadhi ya masuala yenye manufaa na
taifa wanakubaliana na serikali au wanatoa maoni yenye kuboresha CDM yenyewe imejengeka katika mfumo wa kupinga
tu.
Sasa katika hali hiyo usitegemee atokee mbunge wa kuteuliwa toka kwa hawa watu.
Mkuu, nahisi hujafanya utafiti wa kutosha juu ya unalolisema kuwahusu CDM, Chadema ndio kimekuwa chama kinachotoa mapendekezo mengi tu kwa maendeleo ya nchi, kwani kuhusu Katiba mpya si ni chadema waliolivalia njuga hadi JK akakubali? Kuhusu wizara hiyo ya madini na nishati kugawanywa, kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, ni Mhe mwenyekiti wa CDM ndiye aliyependekeza Bungeni kuwa kutokana na umuhimu wa wizara hii ni heri kuzigawanya, wabunge wa magamba walibisha sana hili, Zitto Kabwe akakomelea msumari wa moto kwenye kidonda, leo kiko wapi? si umesikia JK ameisha fanya nusu ya hilo? Hivi ile hotuba ya JK mwezi April, 2011 hasa bei ya sukari, si ni chadema waliompa mwongozo hata kumfanya PM kuamka usingizi akaanza kutembela mikoa inayo zalisha Sukari? Without research no right to speak.
Nimalizie hii, wakati Kikwete anaingia madakani 2005, alikuwa na baraza kubwa kweli la mawaziri, CDM (of course hapa na CUF waliingia) walilipigia kelele nyingi kweli hili Baraza, nadhani unakumbuka nini kilitokea, JK alipunguza 2008, hivi kuvunjwa kwa hili Baraza la Mawaziri, chanzo ni nini kama tutakuwa wakweli? haraka haraka utasema ni Bungeni, but rudhisha kumbukumbu zako nyuma, Dr Slaa na Zitto Kabwe ndiyo waazilishi wa hii topic, leo kiko wapi? si ni jana tu JK kafanya kama alivyo elekezwa? Hata kama kitu hukipendi jaribu basi kuwa mkweli, CDM ndio wanaongoza nchi kwa remote kwakweli, magamba hawana Think Tank, wanasuburi CDM waseme nini ndio wanafanya, umesahau CDM waliposusia mjadara wa Bunge juu ya issue ya Katiba? walipokwenda Ikulu na mapendekezo yao, nini kilitokea?
Tafakari!!!