MENGELENI KWETU
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 9,552
- 24,164
Rais mstaafu Jakaya Kikwete imeelezwa kuwa anafahamu kilichokuwa kinaendelea katika suala la makontena bandarini na taarifa za kiuchunguzi zinaonyesha alipewa taarifa na akazikalia kimya.
Imejulikana kwamba aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe alibaini upotevu wa makontena hayo, akaandika taarifa ya kina kwenda Ikulu lakini kilichomkuta hatakisahau maishani..!!.
Ripoti hiyo ilimkaanga mwenyewe Mwakyembe kwani baada tu ya JK kuipitia, akamwondoa Wizara ya Uchukuzi na kumpeleka Wizara ya Afrika Mashariki.
Taarifa za kina zinasema kuwa Rais Magufuli kabla ya kumteua Mwakyembe kwenye Wizara ya Sheria na Katiba aliyo sasa, alimwita na kumhoji kuhusu upotevu wa makontena hayo na hiyo ndio ikawa nafasi ya Mwakyembe kutoa fundo alilokuwa nalo moyoni.
Pia Mwakyembe alikutana na Waziri Mkuu Majaliwa kuhusiana na upotevu huo.
Pia Ridhiwani Kikwete anatajwa katika sakata hili na inasemekana ameshaitwa kuhojiwa na Waziri Mkuu.
Source: Gazeti la Jamhuri la leo 22/12/2015, Toleo no 221.