Kikwete ana kipi special hadi asingiziwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ana kipi special hadi asingiziwe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Sep 6, 2011.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Salva Rweyemamu msemaji wa lkulu amepinga vikali kuwa raisi wetu hakupokea hongo ya suti.
  Je wikileaks wana ugomvi gani na kikwete hadi wamsingizie? Au kuna mkono wa Chadema kwenye hii KASHFA YA RAISI?
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  Chadema tena? Du, hii kali
   
 3. n

  ngokowalwa Senior Member

  #3
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nadhani Mhe. Salva badala ya kuhangaika na propaganda angetoa kusudio la siku saba mmiliki wa Wikileaks achapiche tamko la kuomba radhi la sivyo atafikishwa mahakamani kwa kuchafua kilicho kisafi , zaidi ya hapo tutajua ni juhudi za kufua kwa maji taka huku unatarajia kung'arisha
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ndo namsikiliza hapa kwenye media,,,,,,,ushuzi mtupu,,,,
   
 5. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwani Wikileaks ndio walioandika hayo? nadhani watu wengi hawajaelewa nini maana ya weakleaks. Hizo ni "Classified diplomatic communication cables" kutoka ubalozi wa Marekani kwenda Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Kwa hiyo walioandika siyo weakleaks bali ni maafisa wa US embassy. Walichofanya Wikileaks ni kuvujisha mawasiliano ambayo ni siri hayakupaswa kujulikana kwa watu walio nje ya mfumo wa intelijensia ya marekani.

  Kama ni uongpo mwongo ni US Embassy na sio Wikileaks.
   
 6. P

  Pokola JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Jamani,

  Ni kweli walimhadaa kwa suti akatoa ardhi (Na sasa Mahakama ya Rufaa). Mwarabu wa Kempiski kidume bana.

  Eti wanajitetea kuwa Marekani wameanza chokochoko za kutaka kuing'oa serikali ya Tanzanania kama ilivokuwa Libya. Ole wenu tutakapoamka dhidi yenu mnaotuibia, hakuna wa kutuzuia.

  Fait Accompli.
   
 7. T

  Testimony Senior Member

  #7
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nadhani hatua sahihi ingekuwa kumwita balozi wa marekani pale mambo ya nje na kumuuliza kama hicho kilichoandikwa na weakleaks ni kweli ni mawasiliano yao wamarekani na si weakleaks. manake wao ndo waliomdharirisha mh 'raisi' (feki - mchakachuaji) kwa mawasiliano yao yaliyonaswa na weakleaks na kuvujishwa hadharani! vinginevyo kama alivyosema mdau mmoja hapo, ni kusafisha nguo kwa maji taka!
   
 8. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Weakleaks wanavujisha taarifa za kiintelijensia za Ubalozi wa Marekani na kuutoa. Serikali ilitakiwa iwabane hawa Weakleaks wathibitishe kama kweli hizo taarifa wamezitoa Katika mawasiliano ya Us Embasy na kama ni kweli Us Embasy ilitakiwa wabanwe wathibitishe wakishindwa tuwafukuze wafunge ubalozi wao hapa kwetu maana watakuwa hawatutakii mema. Kwakutokuwabana inaonyesha haya yote ni ya kweli
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  Lakini kwa nini US Embassy umsingizie Kikwete? Kikwete akiri madhambi yake, atuombe radhi kisha ajiuzulu. Ameliaibisha taifa
   
 10. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  JK na ikulu yake waibane USA embassy?Mimi nakufa..Anavyopenda kwenda huko kula bata...Nakwambia hawazi kusema chochote wala hata barua hataandika kwa huo Ubalozi wa USA.Akileta longolongo no Visa to USA...kwisha kazi.
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Mada yako ni nzuri ila unaipotosha kwa kuingiza ChADEMA, kumbuka wikileaks huyohuyo amesema kuwa slaa hakushinda- ni mkono wa ccm ama?!
  <br />
  <br />
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Heeeh, since when???!!! au ukiwa katibu muhtasi wa ikulu, basi unaitwa mheshimiwa?
   
 13. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Duuh ! natamani niijue hizo suti.....itabidi nipitie picha za zamani za JK kwani najua hatozivaa tena. Kama rais anapitisha bakuli kuomba misaada si ajabu kupewa suti pia kama msaada....ila kulipa fadhila kwa muarabu ni ghali na kunawagharimu watanzania.
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,269
  Likes Received: 22,029
  Trophy Points: 280
  Tunauza nchi kwa suti za kuvaa raisi, hii ni aibu ya karne
   
 15. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Nilichokipenda zaidi ni kuwa anatmia vyumba vya kempinsk kwa mambo yake ya siri marakwa mara na haorodheshwi kwenye orodha ya wageni. Kwangu mimi ni more shamefull kwa kiongozi wanchi kusaidia taasis kukwepa kodi. Kama salva angekuwa na hekima angejibu hoja moja baada ya nyingine na siyo kukurupuka na kumtaka mmilikiwa hotel kuthibitisha. Salva atuambie: JK si mteja wa hotel?!, hakusafiri safari ya hisani na kununua suti?, hakupokea mchango wa uchaguzi?. Na pia Salva ajifunze protocol ya kuhoji mambo: nani aulizwe/ ajibu juu ya hili- mmiliki wa hotel?!, boss wa hotel?!, weekleaks?! Au ubalozi wa marekani?!.
   
 16. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Duh ebwana ndio, huyo ndo jk na ikulu yake. Kila siku midundiko!
   
 17. kanywaino

  kanywaino Senior Member

  #17
  Sep 6, 2011
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  weakleaks i nani kwani humu ulimwenguni..nani kawapa mamlka wakiongea kila kitu tuwaamini?
   
 18. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  mna ubavu wa kuwafukuza wa marekani nyie,au unaongea 2,infact ha2wez vunja uhusiano we2 na Us eti kisa mpuuzi mmoja{jk}kachafuliwa.
   
 19. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jk anaona aibu sana, anajua wakubwa zake huko US wanajua ni mwepesi, hata suti anahongeka.
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Anaitwa JK a.k.a OMBAOMBA
   
Loading...