Kikwete amteua Peter Noni Mkurugenzi mpya TIB!

Kikwete amteua Peter Noni Mkurugenzi mpya TIB!

mwanakijiji hamjui NONI,ndio maana anatuletea vipande vya magazeti hapa.!

wewe unaye mjua mbona hutuambi lolote badala yake unaonekana kushabikia tu au na wewe ni miongoni mwa wanaufaika?
 
Sawasawa.

Sawasawa.

Mbona unajipinga mwenyewe. Kwanza, kwa nini siwezi na unapata wapi jeuri ya kudai sina fact. Pili, wewe unapata wapi uwezo wa kusema hivyo na kudai kuwa si fisadi ? Kwani wewe ndiye Noni ?

Unasahau kuwa mhusika hakuwahi kukanusha hicho unachokiita kipande cha gazeti. Je, unakanusha haya aliyosema Wakili Sanze kuwa "Niliitwa na Bw. Malegesi ofisini kwa Bw. Rostam Aziz, 50 Milambo, Ofisi za Caspian Construction Limited. Nilipofika…niliwakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni na Bw. Malegesi, wakaniambia fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa CCM na rais wake".

Anayepinga hapa ni wewe. Kulingana na maelezo ya Noni mwenyewe mahakamani, "all applications for EPA funds passed through the governor, who in turn forwarded the documents to me as the then BoT director of economic policy, before the applications were sent to the bilateral and commercial debt department, which was headed by Imani Mwakosya". Sasa hapa kwa nini Mwakosya ni mshtakiwa na Noni ni shahidi upande wa mashtaka.

Mtimti, naona unaumia sana rohoni huyu jamaa kuitwa fisadi, je unaamini moyoni kuwa hakuna ufisadi uliofanyika benki kuu. Inaonekana wazi kuwa mhusika alikuwa karibu sana na Balali na alishiriki kupitisha hayo malipo kulingana na maelezo yake yeye mwenyewe. Humu JF hatuangalii sura, undugu, urafiki, ushikaji wala ujinsia - tunamkona nyani kwa umbile lake lolote lile.

mimi siumii kwa noni kuitwa fisadi,ila nnachosimamia ni kuwa NONI hakufaidika na pesa za EPA.noni anashindwa kushtakiwa hivyo kuwa shahidi kwa sababu KWANZA yeye hakuwa mtu mwenye kauli ya mwisho ya kuithinisha hayo malipo,mwenye kauli ya mwisho alikuwa balali na mwakosya anashitakiwa kwa sababu alikuwa mkuu wa kitengo cha madeni hivyo kuna watu walianzisha vikampuni vyao vya uongo na kweli na kwenda BOT kuchota pesa,hivyo nyaraka zote feki zilipitia kwenye idara hii ya kina mwakosya na komu,kwa maana nyingine ni kwamba wizi wote wa EPA ulianzia kwenye hii idara,hivyo kumhusisha noni moja kwa moja na EPA ni ngumu ndio maana amefanya kuwa shahidi
 
FAUSTINE KAPAMA

My Take:
Kama huyu jamaa kweli ana chembe yoyote ya kile kinachoitwa Uadilifu, atakataa nafasi hii aliyoteuliwa hadi kesi ya EPA itakapokwisha na Rais ataacha huu mchezo wa kuinfluence the course of justice kwa kumteua mmoja wa washtakiwa katika nafasi kubwa ya kusimamia benki ambayo imepokea fedha zinazohusika katika mashtaka ambayo yeye (noni) ni shahidi.

This is a classic example of travesty of justice.

Mwanakijiji,
Kwani umesahau kuwa nchi hii rais ni Rostam Azizi na Kikwete ni "rubber stamp" tu? Umeshasahau juzi kuhusu uteuzi wa wakuu wa wilaya walioteuliwa wakiwa na kesi za rushwa mahakamani na mmoja alikuwa chini ya uchunguzi wa TAKUKURU?

Mchezo ni uleule wa EPA, sasa hivi wanahamishia kambi TIB na wanampeleka huyu jamaa huko kwa utekelezaji. Utasikia PESA nyingi zimepelkwa huko kwa ajili ya kusaidia kilimo na kisha kingmaker kama kawaida yake atachota na kuweka mfukoni mwake na kuwagawia CCM kidogo kwa ajiili ya kampeni.
Peter Noni na RA ni damu damu kwani hivi sasa hisa zao za VodaCom wamezificha kwenye kivuli cha kampuni ya Mirambo (RA=19 %, Noni 16%). Usitegemee akatae hii nafasi kwani ni system inasukwa kwa wizi mwingine. Wakulima wanaotegemea support ya TIB na hasa makampuni ya maua huko Arusha wajiandae kulia mwakani kwani hakutakuwa na pesa za kuwapa.
JK kweli hafai kabisa. Rais gani unafumba macho hata kwa uozo wa wazi namna hii?
 
mimi siumii kwa noni kuitwa fisadi,ila nnachosimamia ni kuwa NONI hakufaidika na pesa za EPA.noni anashindwa kushtakiwa hivyo kuwa shahidi kwa sababu KWANZA yeye hakuwa mtu mwenye kauli ya mwisho ya kuithinisha hayo malipo,mwenye kauli ya mwisho alikuwa balali na mwakosya anashitakiwa kwa sababu alikuwa mkuu wa kitengo cha madeni hivyo kuna watu walianzisha vikampuni vyao vya uongo na kweli na kwenda BOT kuchota pesa,hivyo nyaraka zote feki zilipitia kwenye idara hii ya kina mwakosya na komu,kwa maana nyingine ni kwamba wizi wote wa EPA ulianzia kwenye hii idara,hivyo kumhusisha noni moja kwa moja na EPA ni ngumu ndio maana amefanya kuwa shahidi

- Mkulu Mtimti, heshima zako unajua jina lako huwa linanikumbusha sana mjini Dar enzi za waya mkali tulikuwa tunalitumia sana kama code ya neno US dollar, kwenye kubadilisha mtaani kwa mwendo wa kuruka, Bwa! ha! Bob Mkandara atakuwa anakumbuka sana na Mkulu Spearman,

- Anyways, huyu mkulu Noni nimemsikia sana kuhusika na EPA na KAGODA, mara ya mwisho kuna dataz nilizianasa kwamba huyu ndiye aliyesaini mkataba wa BOT na KAGODA, yeye Noni alisaini kwa niaba ya BOT na Rostam alisaini kwa niaba ya KAGODA, mpaka leo sijui ukweli sana wa hizi dataz lakini vipi unaweza kuwa unazijua mkuu umwage maana naona kama unamfahamu sana huyu mkulu, nimemsikia sana lakini sijawahi hata kumuona, najua kwamba he is a very smart man siku zote chini ya Radar,

- Je hizo habari zina ukweli wowote kama unazijua!

Respect.

FMEs!

wewe unaye mjua mbona hutuambi lolote badala yake unaonekana kushabikia tu au na wewe ni miongoni mwa wanaufaika?

Unajua,watu wanamuhusisha NONI na EPA kwa sababu idara yake ndio ilikuwa inashughulika imekalia hizi fedha na yeye ndio alikuwa anatoa mapendekezo kuwa walipwe,lakini ikumbukwe kuwa huu mchezo ulikuwa unaanzia kwa balali kisha anapeleka kwa katibu wa benki na katibu anampelekea noni ili atoe mapendekezo (sio idhini),idhini alikuwa anatoa mwenyewe balali,pia wengine walikuwa wanaanzia huku kwenye idara ya madeni na mikopo ambaayo ilikuwa inaongozwa na mwakosya na komu(washtakiwa wa EPA),hukun walikuwa wanakuja na nyaraka feki na kampuni za uongo na hii idara inapitisha madai yao kisha mkulu balali anaidhinisha noni atoe pesa,sasa hapo unaweza sema noni ni mwizi kwa kuwa kashuhudia uchafu?au utamweka awe shahidi ili aeleze jinsi uchafu ulivyokuwa unafanyika?
 
- Mkulu Mtimti, heshima zako unajua jina lako huwa linanikumbusha sana mjini Dar enzi za waya mkali tulikuwa tunalitumia sana kama code ya neno US dollar, kwenye kubadilisha mtaani kwa mwendo wa kuruka, Bwa! ha! Bob Mkandara atakuwa anakumbuka sana na Mkulu Spearman,

- Anyways, huyu mkulu Noni nimemsikia sana kuhusika na EPA na KAGODA, mara ya mwisho kuna dataz nilizianasa kwamba huyu ndiye aliyesaini mkataba wa BOT na KAGODA, yeye Noni alisaini kwa niaba ya BOT na Rostam alisaini kwa niaba ya KAGODA, mpaka leo sijui ukweli sana wa hizi dataz lakini vipi unaweza kuwa unazijua mkuu umwage maana naona kama unamfahamu sana huyu mkulu, nimemsikia sana lakini sijawahi hata kumuona, najua kwamba he is a very smart man siku zote chini ya Radar,

- Je hizo habari zina ukweli wowote kama unazijua!

Respect.

FMEs!

mkulu,noni alikuwa ni mtoa mapendekezo juu ya walipwaji wa EPA baada ya balali kuyapeleka madai kwa katibu wa benki kisha katibu kuyahakiki,baadae mapendekezo yanakwenda kwa balali ambae anayaidhinisha.
hapa ukiangalia,gavana alikuwa alikuwa anafuata procedure ya kiini macho tu lakini huyo gavana ndio alikuwa na kauli ya mwisho juu ya nani alipwe na nani asilipwe
sasa ukiangalia kwa mtiririko huo utaona jinsi suala la KAGODA lilivyomkalia noni
 
mimi siumii kwa noni kuitwa fisadi,ila nnachosimamia ni kuwa NONI hakufaidika na pesa za EPA.noni anashindwa kushtakiwa hivyo kuwa shahidi kwa sababu KWANZA yeye hakuwa mtu mwenye kauli ya mwisho ya kuithinisha hayo malipo,mwenye kauli ya mwisho alikuwa balali na mwakosya anashitakiwa kwa sababu alikuwa mkuu wa kitengo cha madeni hivyo kuna watu walianzisha vikampuni vyao vya uongo na kweli na kwenda BOT kuchota pesa,hivyo nyaraka zote feki zilipitia kwenye idara hii ya kina mwakosya na komu,kwa maana nyingine ni kwamba wizi wote wa EPA ulianzia kwenye hii idara,hivyo kumhusisha noni moja kwa moja na EPA ni ngumu ndio maana amefanya kuwa shahidi

Mtimti,
Inawezekana Noni akawa baba mdogo, mjomba wako au mtu wa karibu nawe sana na kwa namna moja au nyingine unanufaika na pesa zake, kwahiyo usingefurahi kuona anaitwa fisadi. Lakini hiyo haifuti ukweli wa kwamba Noni ni fisadi na tena ameanza kuiba BOT siku nyingi si kwenye EPA tu. Noni amekuwa na kampuni ya Planetel tangu miaka ya 90 (90s) wakishirikiana na kampuni ya Iridium Africa katika biashara ya simu za kutumia satelite mpaka kampuni mama huko Marekani lilipofilifisika wakapewa ushauri wa kutafuta mbia mwingine wa simu za mkononi ndo wakawaita VodaCom South Africa. Sasa jiulize mfanyakazi wa BOT hata kama ni mkurugenzi ana mshahara kiasi gani na marupurupu kiasi gani cha kuweza kumiliki 16 % ya VodaCom Tanzania ambayo pato lake kwa siku hivi sasa si chini ya bilioni 1 ambayo maana yake ni kwamba kipato chake huko si chini ya milioni 160 kila siku kabla ya kodi? Haya huko ofisini kwa Rostam walikokuwa na Maregesi wakisuka deal la Kagoda ilikuwa bure tu? Tangu lini mtu akasaidia kufanikisha wizi wa mabilioni halafu yeye asinufaike na wizi huo? Fikiria zaidi.
 
Mtimti,
Inawezekana Noni akawa baba mdogo, mjomba wako au mtu wa karibu nawe sana na kwa namna moja au nyingine unanufaika na pesa zake, kwahiyo usingefurahi kuona anaitwa fisadi..

- Haina sababu yoyote ndio chanzo cha kuharibu mijadala, mtimti ameweka hoja na wewe weka hoja tuchambue, haya ya binafsi yasipewe nafasi hapa JF.

Ahsante Mkuu.

FMEs!
 
- Mkulu weka darasa zaidi hapa au muongozo, ukiweza!

Respect.

FMEs!

KAGODA ndio pesa zilizoiweka serikali ya muungwana madarakani,mtiririko wa uchukuaji pesa wa KAGODA ulianzia kwa gavana na ukaishia kwa gavana.
 
Mtimti,
Inawezekana Noni akawa baba mdogo, mjomba wako au mtu wa karibu nawe sana na kwa namna moja au nyingine unanufaika na pesa zake, kwahiyo usingefurahi kuona anaitwa fisadi. Lakini hiyo haifuti ukweli wa kwamba Noni ni fisadi na tena ameanza kuiba BOT siku nyingi si kwenye EPA tu. Noni amekuwa na kampuni ya Planetel tangu miaka ya 90 (90s) wakishirikiana na kampuni ya Iridium Africa katika biashara ya simu za kutumia satelite mpaka kampuni mama huko Marekani lilipofilifisika wakapewa ushauri wa kutafuta mbia mwingine wa simu za mkononi ndo wakawaita VodaCom South Africa. Sasa jiulize mfanyakazi wa BOT hata kama ni mkurugenzi ana mshahara kiasi gani na marupurupu kiasi gani cha kuweza kumiliki 16 % ya VodaCom Tanzania ambayo pato lake kwa siku hivi sasa si chini ya bilioni 1 ambayo maana yake ni kwamba kipato chake huko si chini ya milioni 160 kila siku kabla ya kodi? Haya huko ofisini kwa Rostam walikokuwa na Maregesi wakisuka deal la Kagoda ilikuwa bure tu? Tangu lini mtu akasaidia kufanikisha wizi wa mabilioni halafu yeye asinufaike na wizi huo? Fikiria zaidi.
sikatai na unachosema,mimi noni ni mtu wangu wa karibu sana,na juzi tu tulikuwa pamoja kwenye msiba wa mdogo wake,tukaenda bhupandagila kuzika...ila nataka kukwambia kitu,mimi sinufaiki na pesa ya noni,mi nna familia yangu,naishi vizuri tu hapa uk.kama noni akifanya madudu au nikijua madudu yake sintoacha kumchana,na pia kujua profile nzuri ya mtu kama ulivyoandika hapo juu jinsi jamaa alivyohangaika na kampuni yake mpaka leo kufika hapo haikufanyi wewe kumwita fisadi,je unajua planetel ina shareholder wangapi?
 
mzee mwanakijiji inaonekana jamaa unamwelewa vizuri.kuna kitu nataka kuuliza.katika pita pita zangu katika hii thread nimeone watu wanamuhusisha na vodacom.Sasa kusema ukweli mimi sijaelewe kwanza -

Hiyo planetel ni nini?
Ni ya kina nani?
Na inafanya kazigani?
Na huyu mteule wetu (noni ) anahusika vipi?

pili

Noni ana share vodacom kupitia kampuni gani?mana nilivyosikia jamaa ana shae voda ilinibidi niingie kwenye web ya voda kupata details lakini sijaona jina lake mana kwenye web ya voda nimekuta Mirambo ya papa ra 35% na voda group 65%.sasa jamaa aliiingiaje

Mwisho

Voda na planetel zinaingilianaje?

hii itaniweka sawa kidogo kumuelewa huyu mkulu

Mwana siasa,
Shareholders wa Vodacom wamebadilishwa hivi juzi yaani mwaka huu tu baadaya ya kingmaker RA kuhisi kizunguzungu kama kawaida yake akaamua kuweka kivuli (yaani kuificha Caspian na Planetel kwenye share holders na zote zikawa chini ya Mirambo ambayo nahisi ukiuliza utaambiwa wamiliki wake hawajulikani kama Kagoda). Mwanzoni kabisa mambo yalikuwa hivi:

Vodacom Tanzania Partnership
It has been claimed that Vodacom Group has a habit of choosing politicians and their friends as business partners to extends its operations on the continent. It was reported by The Mail & Guardian that Mozambican President Armando Guebuza had become a shareholder in Vodacom Mozambique.

Vodacom Tanzania was licensed in Tanzania with its local partners Planetel Communications holding 36% and Caspian Construction holding 16%. Later Planetel decreased its stake to 16%, while Caspian’s increased to 19%.

A representative of Caspian on the Vodacom Tanzania board is businessman-politician Rostam Aziz, a close supporter of President Jakaya Kikwete. At the time Vodacom was licensed in Tanzania, neither man was quite as powerful as now.

Kikwete was Foreign Minister and Aziz had yet to occupy any formal position in Tanzanian politics.

While spreading its political bets, the CCM's and the former Speaker of Parliament Pius Msekwa was granted Vodacom Tanzania’s non-executive chair between 2003 and 2005. When Vodacom Tanzania hosted a “VIP gala night” to bid farewell to outgoing president Mkapa in December 2005, Msekwa attended, presumably in both capacities.

Source: Wikipedia, the free encyclopedia
 
Last edited:
Mwana siasa,
Shareholders wa Vodacom wamebadilishwa hivi juzi yaani mwaka huu tu baadaya ya kingmaker RA kuhisi kizunguzungu kama kawaida yake akaamua kuweka kivuli (yaani kuificha Caspian na Planetel kwenye share holders na zote zikawa chini ya Mirambo ambayo nahisi ukiuliza utaambiwa wamiliki wake hawajulikani kama Kagoda).

kwani kuwa shareholder sehemu kuna tatizo?au kwa kuwa yupo na rostam?uchafu wa rostam utabakia kwa rostam na wa noni utabakia noni,huwezi kumuhukumu noni eti kwa sababu yeye na rostam wana share voda.
 
Hebu sasa jiulize kwanini wameficha majina ya kwanza na kuyawekea kivuli cha Mirambo? Nini kinafichwa hapa?
 
sikatai na unachosema,mimi noni ni mtu wangu wa karibu sana,na juzi tu tulikuwa pamoja kwenye msiba wa mdogo wake,tukaenda bhupandagila kuzika...ila nataka kukwambia kitu,mimi sinufaiki na pesa ya noni,mi nna familia yangu,naishi vizuri tu hapa uk.kama noni akifanya madudu au nikijua madudu yake sintoacha kumchana,na pia kujua profile nzuri ya mtu kama ulivyoandika hapo juu jinsi jamaa alivyohangaika na kampuni yake mpaka leo kufika hapo haikufanyi wewe kumwita fisadi,je unajua planetel ina shareholder wangapi?
Mtimti,
Wewe kwa sababu ya ukaribu kwa noni na kumjua noni basi umetoa yote ya kumhukumu Balali, na wale walio-karibu na Balali wakisema opposite sijui iweje. Balali is a dead body, at this time everybody will say what he wishes, kwa kuwa hakutakuwa na ushahidi.
Mwanakijiji amekuletea hadi gazeti la Serikali (unayoiamini wewe) limeelezea shahidi alivyosimulia "role" ya Noni na wala wewe uamini; you must be kidding!
You better re-start another strategy!
 
Mimi naamini aliyoyasema mwaka jana Mtikila kuwa RA anawaona Watanzania ni "matahaira". Haiwezekani mtu umezungukwa na kashfa kiasi hiki na bado unaendelea kupeta!

Turudi kwa Noni: Hizi "kama" zifuatazo:

a. Kama Peter Noni ni mtu mwadilifu na alishuhudia nyaraka za uongo za makampuni ya EPA zikipitishwa mikononi mwake kutoka kwa kina Mwakosya kwenda kwa Ballali au kutoka kwa Ballali kwenda kwa Mwakosya na yeye akakaa kimya na kuacha wachote fedha kama kisimani basi ni mwoga na hana uadilifu.

b. Kama aliziona nyaraka hizo na mawasiliano hayo na hakujua kuwa ni za uongo na yeye akaziacha zipite na kuzikubalia badala ya kupiga kelele wakati huo kiasi kwamba mwenyewe amekiri ati alitoa mapendekezo kwa mdomo (akijua Marehemu hawezi kukanusha) kuwa mambo yasifanyike hivyo ni mtoto mdogo tu anaweza kuamini. Kama hakujua nyaraka (nyingine zipo hapa ni za uongo) kitu ambacho ni rahisi hata kwa mtu ambaye si msomi ina maana hana uwezo wa kusimamia idara nyeti na zaidi kabisa hana uwezo wa kuchambua mambo ya kiuchumi huko TIB.

c. Nakataa kabisa kuona RAis anamteua shahidi wa kesi muhimu wizi mkubwa wa mabilioni kuwa afisa wa juu wa benki nyingine wakati akiwa katika Benki Kuu aliachilia madudu yafanyike. Aidha Kikwete mwenyewe ameshiriki katika wizi huu (and I'm serious!) au yeye mwenyewe hajui kuwa Peter Noni amewahi kufanya kazi Benki Kuu wakati wa wizi wa EPA. Vinginevyo alichofanya ni kuwachezea akili watanzania kama alivyofanya kwa kumteua tena Chenge kuwa Waziri!!
 
Huyu jamaa si fisadi kama tumfikiriavyo,labda anaweza kutiwa hatiani kwa kufuata maagizo kutoka juu. Mimi najua mke wake ni mfanyabiashara na ndiye alikuwa na hisa kidogo Planetel.Alianza kwa kulima mchicha pale Upanga na kuuza, ni miaka ya 80 mwanzoni. Baadaye akaanza kufuga kuku,wakati huo kuku wa kisasa na wafugaji wake ni wachache sana na vifaranga vilikuwa vinatoka Zambia. Alikuwa anasambaza mahotelini New Africa, Kilimanjaro na hata soko la Kisutu. Baadaye akafungua duka la nguo kwa akina mama na vitu kama hivyo. Hii ni familia ya wachapakazi, kama kuchapa kazi kwao kunawafanya waishi vizuri kidogo na baba yupo BOT haimaanishi ni mafisadi. Hili swala la EPA kuna watu wanaotakiwa kuguswa na hawajaguswa bado. Noni si mmoja wao.

Biashara kitu gani bwana. Hata Rostam anadai babu zake walianza biashara siku nyingi (bila shaka ya watumwa) Je hiyo imemuzia kuwa tu siyo mwizi bali jambazi mahiri? Wacha wagawiane tu kuna siku wajukuu zangu lazima wajichukulie halali yao.

Mongrels, scoundrels alcataraz and ten years of badluck
 
jk kumpoint noni ni uchafu?acha kushikiwa akili...usifikiri hiyo ni nafasi ya kisiasa,noni ameenda shule,angalia record yake na nafasi alizoshika toka ameingia BOT

Issue hapa si shule ni USAFI unless hujuwi (which could be true otherwise usingesema hivyo) namna ambavyo huyu mteule alishiriki katika wizi wa aibu wa EPA. Kama shule hata Hosea na Mwnyika wameenda shule lakini ndio hawafai wamechafuka vibaya masikini na sakata la Richmond.
 
Tanzania Investment Bank picked broker in recovery of CIS loans

2008-07-23 10:03:05
By Bilal Abdul-Aziz, Dodoma

The government has said it would now recover billions of money it disbursed to individuals, companies and institutions under the Commodity Import Support (CIS) programme through the Tanzania Investment Bank (TIB) and a broker.

Finance and Economic Affairs deputy minister Jeremiah Sumari issued the statement on Monday when responding to a supplementary question by Charles Keenja (Ubungo, CCM), who had demanded to know measures taken by the government to recover money loaned to individuals, companies and public institutions under the CIS arrangement.

``We have charged TIB with the duty of collecting all debts which previously were being followed up by the treasury, and also engaged a broker for stepping up efforts in recovering the debts,`` he told the House.

Responding to a follow-up question to the supplementary question by Anne Kilango (Same, CCM) on stern measures taken to recover the money, Sumari said TIB and the broker would now be tougher on defaulters.

``Following expiry of the agreed time to pay back the loans, TIB and the broker will now push them to pay back according to contracts they signed with the treasury…this will involve foreclosing their collaterals,`` he said.

Responding to the principal question posed by Keenja, Sumari said the government was on course in recovering the money and would apply all means possible to achieve the same.

Keenja, among other things, had wanted to know the total amount issued and collected so far, as well as problems encountered in recovering the debts.

``The amount allocated to the Commodity Import Support programme is 220,195,002,930/- ….and by September 2007, a total of 980 individuals, private companies and public institutions had benefited from the CIS loans,`` he said.

However, Sumari said the total amount recovered so far was 199,221,222,212/-, dismissing claims that problems encountered in recovering the CIS loans were similar to those faced in the recovery of the loot from the Bank of Tanzania's external payment arrears (EPA) account.

It's understood that under EPA, dishonest businesspeople and public officials plundered about 133bn/- through dubious deals involving phony companies. The government was still making efforts to recover the money.

``Under CIS, loans were issued to those who met required conditions and prescriptions. The treasury invited applications through newspapers and applicants were required to apply for loans under specific sectors,`` explained Sumari.

He mentioned the sectors involved as including agriculture, industry, trade, mining, transport, construction and energy.

SOURCE: Guardian
 
I love Tanzania. Long live king maker. RA ametuma ujumbe kwa Mengi kuwa yeye ndo Rais wa nchi hii...
 
Back
Top Bottom