Kikwete amtembelea Kardinali Pengo Dubai

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
KIKWETE+PICHA.jpg


Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amemtembelea Mhadhama Polycarp Kardinali Pengo, nchini Dubai leo.


Kikwete ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter leo(Ijumaa) na kueleza kuwa amemkuta Kardinali Pengo akiwa mwenye siha njema.

Ingawa hajaeleza amemkuta Kardinali Pengo nyumbani au Hospitali lakini askofu huyo mkuu wa jimbo la Dar es Salaam, amewahi kuripotiwa kuwa yupo nje ya nchi kwa matibabu.

“Nikiwa Dubai safarini kwenda Canada, nimemtembelea asubuhi hii Mhadhama Polycarp Kadinali Pengo na nimefarijika kumkuta akiwa na siha njema.” Ameandika Kikwete

Kikwete amesema amemtembelea Kardinali Pengo wakati akiwa safarini kuelekea Canada.


Chanzo: Mwananchi
 

Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
2,952
2,000
Mara zote dagaa ndio wanakamatwa nchi yetu, wasababishaji wanadunda.
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,223
2,000
Ha ha haaaa

Naona mmepata lingine la kuongelea siku ya leo juu ya safari hiyo ya Canada.

Mimi yangu macho na masikio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom