Makala: Nyerere asiwagombeza Maaskofu-Haishangazi Kardinali Pengo Kujiuzulu-01

Paschal Matubi

JF-Expert Member
Sep 15, 2008
235
303
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
SOURCE: RAIA MWEMA, APRIL 18, 2018, pg. 12

Ujumbe wa kwaresima umesababisha Polycarp Kardinali Pengo akanukuliwa hivi, “Moja tu ni kwamba barua nzima imechanganya vitu viwili. Mwalimu angekuwepo angepiga kelele na kusema Maaskofu msichanganye dini na siasa, angepiga kelele sana…Katika waraka ule zinachanganywa dini na siasa, hii si kazi ya maaskofu ni kazi yenu wanasiasa CHADEMA, CCM…”: {TUMAINI LETU: Aprili 05, 2018, uk. 02, aya ya nane}.

Oktoba 16, 1970, Rais Julius Nyerere akiwa jijini New York, aliwatembelea masista wa Maryknoll. Walimuomba kuzungumza akatoa hotuba ya kiingereza inayoitwa “The Church and Society”. Sehemu ya hotuba nimeitafsiri hivi,

Kwa karne nyingi, Kanisa, limekubali watu kutumikishwa kwa mabavu, kuteswa, unyonyaji na watawala kutoka nje wala kanisa halikukemea. Hata sasa, Kanisa limekataa kukemea ugandamizaji wa serikali nchini Msumbiji, Angola, Guinea Bissau. Ni kweli miezi iliyopita, Papa ameongea na wapigania uhuru watatu, lakini huu ni mwanzo tu. Bila kukemea kwa sauti na vitendo, Kanisa Katoliki litaendelea kuonekana limekumbatia serikali za kikandamizaji”: {Freedom and Development | Uhuru na Maendeleo, ISBN: 9976400179, uk. 223, aya ya kwanza}.

Rais Nyerere akaendelea kusema, maaskofu wanapokemea ukandamizaji wasiogope “kusingiziwa” kuwa wametumwa na wapinzani, ninanukuu, “Sometimes it will mean the Church leaders involving themselves in nationalist freedom movements and being part of those movements... sometimes it will mean working in opposition to establish authority and power”: {uk. 221, aya ya mwisho}.

Rais Nyerere akaendelea kusema, ziko nchi ambako kanisa lilipokemea ukandamizaji wapo mapadri na maaskofu waliuawa, walifungwa magerezani, waliteswa, walinyanyaswa, walifukuzwa kwenye nchi. Rais Nyerere akasema, wote hao walijitoa sadaka kudumisha sifa kwamba kanisa katoliki lazima litetee haki hata kwa gharama, ninanukuu, “Some of these priests have been assassinated, some have been imprisoned, some have been tortured; some, unfortunately, have been dismissed or re-located by the Church hierarchy.”: {uk. 222, aya ya pili}.

Februari 10, 1981, Rais Julius Nyerere, alihutubia wamisionari wakatoliki waitwao “CIDSE” jijini D’Salaam, akasema,

where the church remained identified with colonial regime to the bitter end, as in Mozambique, it experiences difficult now. Where it was able to identify with politics aspirations of its members and community at large, it has usually been able to avoid conflict with authorrities”: {aya ya 08}.

Hapa Rais Nyerere anasema, “mahali ambapo kanisa liliegemea upande wa serikali kama Msumbiji, sasa baada ya ukoloni limeishia kuchukiwa na serikali, na pale lilipounga mkono siasa za wengi halikuchukiwa na serikali mpya”.

Utafiti wa Frieder Ludwig umeeleza Rais Julius Nyerere alivyoupenda waraka wa askofu Helder Camara wa jimbo katoliki la “Olinda e Recife” nchini Brazil. Waraka huo uliitwa “Gospel and Revolution” yaani “Injili na Mapinduzi” aliutoa askofu Camara kwenye jimbo lake wakati Brazil bado inatawaliwa kijeshi.

Frieder anasema, ilipokaribia Krismas ya mwaka 1973 Rais Nyerere aliusambaza waraka huo kwa maaskofu wa Tanzania na marafiki zake wa nje: {Church and State in Tanzania: Aspects of Changing in Relationships, 1961-1994, ISBN: 9789004115064, uk. 106, aya ya mwisho}.

Hivyo, kufikiria kwamba Julius Nyerere angewakemea maaskofu ni utabiri mgumu kuukubali ukisoma historia.

Sasa tuone matukio ya ukatoliki na siasa za Tanzania. Wamisionari waliwasili Bamagoyo Machi 04, 1868 wakakuta siasa za watawala kuuza binadamu wenzao.

Wamisionari pia walikuta ujinga mwingi unaothibitishwa na watawala walivyosaini mikataba kuuza nchi. Hivyo, walijikita kuokoa watumwa na kufuta ujinga kwa kujenga shule.

Vita ya “Maji Maji” ilianza Julai 31, 1905. Serikali ya gavana iliwatesa kwa njaa walikojificha porini, wakafa takriban watu 300,000: {Scramble for Africa, ISBN: 9780349104492, uk. 622, aya ya tatu}.

Kanisa halikutoa waraka kwa ukatili wa “Maji Maji” kwani wamisionari walipeleka Ujerumani ripoti ya ukatili huo. Wabunge wa chama cha upinzani kiitwacho “Social Democrats” wakaipokea ile ripoti na wakaitetea kwenye bunge la Ujerumani liitwalo “Reichstag”: {The Catholic Church in Tanzania, ISBN: 9976631933, uk. 52, aya ya tatu}.

Mjadala bungeni (Reichstag) kuhusu ukatili wa “Maji Maji” ulisababisha bunge likavunjwa Desemba 13, 1906: {Scramble for Africa, uk. 616-628}.

Machi 25, 1953, Papa Pius XII kwa mara ya kwanza aliipa Tanganyika majimbo 13 na akayateulia maaskofu siku hiyohiyo. Mwaka huohuo maaskofu hao wakatoa waraka wa kwanza nchini, ulioitwa “Africans and the Christian Way of Life” yaani “Waafrika na Njia ya Kikristo ya maisha”.

Waraka huo ulitoka kwa kiingereza na kiswahili, ulielekeza wakatoliki masuala ya siasa. Pia ukafundisha maneno demokrasia, haki za binadamu, dola (state), utaifa, uchumi: {The Catholic Church in Tanganyika, uk. 39-40}.

Hivyo, hao maaskofu, tena wazungu wote kasoro Laurean Rugambwa, walifundisha siasa hizi mwaka 1953 kabla hata TANU haijazaliwa. Kumbe, kutoa waraka unaogusa siasa, ndiyo kazi ya kwanza ya maaskofu wa Tanganyika walipopewa majimbo.

Krismas ya mwaka 1960, maaskofu hao wakatoa waraka ulioitwa “Uhuru na Umoja katika Tanganyika mpya”.

Waraka huo uliwaagiza wakatoliki wajiandae kuisaidia serikali mpya inayokuja ya taifa jipya la Tanganyika, ninanukuu, “All Catholics shall try to help build a soundly Tanganyika, with ever growing dedication and ethuthiasm: {The Catholic Church in Tanzania, uk. 40 na 59}. Hii ni historia fupi ya kanisa na siasa katika Tanganyika.

Msomaji, mkatoliki amefundishwa “Katekism ya Kanisa Katoliki”. “Katekism” ina sura inayoanzia ibara ya 1877 hadi 1948, inayoitwa “Jamii ya Binadamu”.

Hizi “barua” mnazoziita “nyaraka” zinapotolewa na askofu mmoja kama ile ya askofu Helder Camara, au wengi kama ya kwaresima iliyopita, ni maelekezo kutoka hii sura na zingine.

Licha ya “kateskim” Papa John Paul II alileta mwogozo unaoitwa “Compendium of the Social Doctrine of the Church’, kwa kifupi humu ninauita “compendium”. Mwongozo huu ulizinduliwa na Renato Kardinali Martino, Aprili 02, 2004 pale Vatican.

Mkatoliki amefundishwa neno “politic”, yaani “siasa” kwani limetokea kwenye hiyo “compendium” mara 257.

Mkatoliki amefundishwa neno “siasa” kwani limetajwa kwenye “katekism” mara 17 kwenye ibara zifuatazo, {407, 439, 596, 676, 782, 899, 1740, 2108, 2109, 2211, 2237, 2239, 2242, 2243, 2244, 2245 na 2246}.

Mkatoliki amefundishwa neno “demokrasia” kwani limetajwa kwenye “compendium” kwenye ibara 24 zifuatazo, {103, 158, 169, 176, 187, 190, 233, 321, 339, 356, 395, 406, 407, 408, 411, 413, 414, 417, 418, 419, 424, 567, 569 na 572}.

Mkatoliki amefundishwa neno “haki za binadamu” kwani limetajwa kwenye “compendium” kwenye ibara 28 zifuatazo: {152, 153, 154, 155, 157, 158, 159, 166, 187, 270, 283, 319, 365, 366, 388, 389, 399, 402, 404, 407, 443, 485, 494, 496, 505, 506, 514 na 571}.

Msomaji, tuone mifano michache ya ibara hizo. Kama unaifahamu migomo halali ya wafanyakazi basi moja ya ibara zinazomfundisha mkatoliki haki ya kugoma ni ibara ya 304 ya “compendium”.

Ibara ya 400 na 401 ya “compendium” zinaitwa “right to resist” yaani zinamfundisha mkatoliki haki ya kupinga sheria kama hiyo sheria inakiuka kanuni za uadilifu.

Ukiona padre au askofu duniani kahubiri au katoa waraka kuhusu “uhuru wa kupata habari” au tukio kuonyeshwa “live”, basi huyo ametekeleza tulichofundishwa wakatoliki katika ibara ya 414 hadi 416 ya “compendium”.

Ukiona askofu kahimiza nchi kuwekewa vikwazo vya uchumi, basi huyo ametekeleza wakatoliki tulivyofundishwa uhalali wa vikwazo hivyo kwenye ibara ya 507 ya “compendium”.

Ibara ya 398 ya “compendium” inamfundisha mkatoliki kwamba inapotungwa sheria isiyo na mantiki (reason), basi kamwe haiwi sheria, sanasana inageuka tu kuwa tamko la vurugu, ninanunkuu, “When, however, a law is contrary to reason, it is called an unjust law; in such a case it ceases to be law and becomes instead an act of violence”.

Wakatoliki ambao ni wanaiasa upo mwongozo wao alioupitisha Papa John Paul II mnamo Novemba 21, 2002 ukatangazwa na Joseph Kardinali Ratzinger mnamo Novemba 24, 2002 humu nauita “Wakatoliki katika Siasa”.

Ibara ya kwanza ya mwongozo huo inaelekeza kwamba ukishakuwa mwanasiasa uige mfano wa Mtakatifu Thomas More aliyekataa kukiuka haki na maadili.

Msomaji, nimetaja makusudi ili usome “katekism”, “compendium” na mwongozo wa “Wakatoliki katika Siasa”. Nimetaja ibara chache zikuonyeshe kile tunachofundishwa wakatoliki duniani.

Ukizisoma utaona kumbe maaskofu wanapotoa matamko au nyaraka hutawalaumu kirahisi. Sanasana unaweza kuwalaumu kwa nini masuala mengine tunayofundishwa wakatoliki hawayatamki na wanasababisha yanapotamkwa yaonekane kama ni mageni.

Hivyo, Rais Nyerere alivyoshutumu woga wa maaskofu, kama wale wa Msumbiji, hakuleta hoja mpya, kwani kukemea siasa za kikandamizaji ndivyo mkatoliki kafundishwa kama zisemavyo ibara chache nilizotaja.

Maaskofu wa Msumbiji walipoacha woga kanisa likafaulu kupatanisha chama tawala FRELIMO na cha upinzani RENAMO kupitia “wamisionari” waitwao “Sant’egidio” mwaka 1992.

Sasa tuone taarifa ya “instagram” na “facebook” ya mtu aitwaye “Mange Kimambi”, ninainukuu, “..Na nasikia Kadinali Pengo ametakiwa na Vatican kujiuzulu ukadinali. Kwahiyo siku yoyote kuanzia sasa Pengo anavuliwa ukadinali..”, (www.instagram.com/p/BhE6mW-lFWl/?taken-by=mangekimambi_).

Hii “instagram” hii imewafurahisha (“likes”) zaidi ya 22,469. Tusijdangaye. Mange tayari ameshatanguliza mazingira ya mjadala itakapotangazwa Kardinali Pengo kajiuzulu, ndiyo sababu nimeandika makala hii.

Kanisa katoliki lina sheria ziitwazo “Code of Canon Laws”, nitaziita “sheria za kanisa”. Ibara ya 455(4) ya “sheria za kanisa” inasema unapotokea utata kwenye baraza la maaskofu, basi askofu mmoja anaweza kuchukua msimamo tofauti, wala baraza zima au rais wa baraza la maaskofu hana mamlaka kumzuia.

Lakini pia ibara hii inasema askofu anaweza kuwakatalia wenzake kama hoja haina maelekezo ya kanisa. Sasa, je walichohubiri kwenye ujumbe wa kwaresima, hakimo kwenye maelekezo ya kanisa?

Mimi naamini kimo ukisoma ibara za “katekism”, “compendium” na mwongozo wa “Wakatoliki katika Siasa” nilizotaja humu.

Turejee hoja ya kujiuzulu. “Askofu msaidizi” aitwaye “coadjutor” anapoletwa, huashiria kwamba askofu aliyeko madarakani anakaribia kujiuzulu.

Polycarp Pengo alipohamishiwa D’Salaam akawa “coadjutor”, ndipo ikajulikana Laurean Kardinali Rugambwa atajiuzulu siku yoyote, japo ilichukua miaka miwili hadi alipojiuzulu.

Kardinali Pengo hajapata “askofu msaidizi” aitwaye “coadjutor”, ambaye wengine humuita “askofu mwandamizi”. Hivyo, bado ni vigumu kutabiri atajiuzulu lini na nani atamrithi.

Je, askofu huondokaje madarakani? Ibara ya 401(1) ya “sheria za kanisa” inamtaka askofu akifikisha umri wa miaka 75 amuombe Papa ruhusa ya kujiuzulu.

Agosti 05, 2019, Kardinali Pengo atatimiza umri wa miaka 75, hivyo ni kweli kujiuzulu kumekaribia kwani siku 475 zilizobaki, siyo nyingi.

Lakini hata atakapoomba, bado hatutajua ataondoka lini kwani kujiuzulu huanza siku Papa anakapokubali ombi lile.

January 01, 2016, askofu Marc Chengula alitimiza miaka 75, lakini Papa hajaruhusu aondoke jimboni Mbeya. Hivyo, D’Salaam inaweza kubaki na Kardinali Pengo kama Kardinali Rugambwa alivyofikisha miaka 80 ndipo akajiuzulu.

Lakini pia askofu yeyote anaweza kujiuzulu chini ya miaka 75 kama ibara ya 401(2) ya “sheria za kanisa” inavyoelekeza na kama ilivyotokea kwa askofu Wendelin Mtega (miaka 67.7) wa Songea au Fortunatus Lukanima (miaka 57.6) wa Arusha.

Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo, ni kweli na wala haishangazi kwamba anaweza kujiuzulu, ama kwa kutumia ibara ya 401(2) yaani siku yoyote, au kwa kutumia ibara ya 401(1) yaani baada ya Agosti 05, 2019.

Mitandaoni nimeona kambi inapenda Kardinali Pengo aondoke hata dakika hii na nyingine haipendi. Nimeeleza utaratibu ulivyo ili unayependa na usiyependa ujiandae kisaikolojia kwa lolote na siku yoyote.

Sasa, kwa nini kanisani hatutumii neno “retire” yaani “kustaafu”? Kazi ya kanisa ni kutangaza imani. Kitendo cha kusikilizwa kinaitwa “professio” kwa kilatini na anayetangaza anaitwa “professor”, kwa kiswahili “profesa”.

Sasa, “profesa” yaani “askofu” anapotingwa na mambo mengine, hayaondoi utaalamu wake. Hivyo, akitingwa na uzembe au ugonjwa au umri “anajiuzulu”.

Kardinali Pengo alipoongea na wazee alitumia lugha hii, “Hakuna popote ambapo Mungu amewahi kumstaafisha mwanadamu, ila mwanadamu atastaafu akishafika mbunguni”: {KIONGOZI: Februari 02, 2018, uk. 03, aya ya tatu}.

Hivyo, kanisa katoliki halina kitendo cha “kustaafu” au “to retire”, bali lina kitendo cha “kujiuzulu” yaani “ to resign”. Hivyo, kila askofu “atajiuzulu” itakapohitajika.

Ibara ya 402(1) ya “sheria za kanisa” inasema, askofu akishajiuzulu ataitwa “bishop emeritus”. Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo akijiuzulu ataitwa “archbishop emeritus” kama anavyoitwa sasa askofu Louis Lebulu wa Arusha au askofu Wendelin Mtega wa Songea. Sijui neno “emeritus” kwa kiswahili japo wapo wanaopendekeza neno “veterani”.

Lakini kanisa lina njia zingine kumuondoa askofu ofisini, moja ni ile ya kumpa jimbo linaitwa “titular”, yaani jimbo lisilo na muumini hata mmoja.

Askofu Jacques Gaillot wa Évreux, Ufaransa, alitofautiana kila mara na baraza la maaskofu la Ufaransa. Ikiandikwa historia ya maaskofu waliosumbua wenzao, hutamwacha huyu askofu Jacques. Hivyo mwaka 1996 Papa John Paul II alipomuondoa madarakani jimboni Évreux alimpa jimbo liitwalo Partenia ambalo ni “titular”.

George Weigel, hakupenda upole wa Papa John Paul II wa kuchelewa kuwaondoa maaskofu kama hawa: {Pope Benedict XVI and the future of the Catholic Church, ISBN: 9780066213316, pg. 252, aya ya kwanza}.

Je, Polycarp Pengo atajiuzulu “ukardinali”? Maana ya “ukardinali” tutaiona wiki ijayo ambapo tutaona kwamba “ukardinali” ni hali ya kuhesabika uko jimboni Roma.

Kitendo cha kujiuzulu “ukardinali” hakitokei sana kwani hakuna aliyejiuzulu “ukardinali” tangu “mjesuit” padri Louis Billot alipojiuzulu Septemba 21, 1927.

Huyu wa RC nae ni wa kusamehe bure, kwanza anajiona bora kuliko wenzake wakati wote wana hadhi sawa ya ki-askofu.
Walitumwa na Yesu kuwa waende kuhubiri injili wao wanahubiri katiiba ,denokrasia na vyama vingi waanzishe tu chama cha siasa tujue nao ni wanasiasa.Malasusa alikuwa sahihi .Halafu hilo linalojiita Baraza la maaskofu wa KKKT ni matapeli katiiba ya KKKT Haina kitu kama hicho wanajaribu kuiga Baraza la maaskofu katoliki ambalo lipo kisheria na kikatiba ya kanisa katoliki.Hilo baraza lililojitia kufanya maamuzi maamuzi yake batili ya kihuni na yako kinyume na katiiba ya KKKT
Mungu Jehova hawezi kuongea na maaskofu kama hawa!labda baali!
Hebu tuuweke waraka kama umeandikwa na kkkt/chadema/cuf n.k Je yaliyoandikwa ndani ya waraka ule yana ukweli? Na yana akisi maisha/hali za watanzania katika kipindi hichi?
Huyo askofu Shoo wa waraka, mchana ni askofu usiku ni kamanda.
 
Karibuni na huku,

Tuseme mara ngapi kuwa Pengo hana ukuu wa Kanisa Katoliki Tz....???
Mimi siwezi kukurupuka Otorong'ongo - mimi nina zero percent emotional approach on these dramas! Siwezi angalia watu wanapiga kelele Pengo katukanwa, wakati mwenzie walikuwa na mahusiano ya kiutendaji. Ila wamekorofishana na sasa Gwajima anamshitaki kwenye mahakama ya wananchi - upuuzi mtupuuuu! Watu wameingizwa kwenye migogoro binafsi, kupigana vita ya Gwajima na Pengo !!!!!!!!!!!

Ninasisitiza - Pengo agangamale!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Yehodaya mungu huwa hapendi unafiki au kuwa chui aliyejivika ngozi ya kondoo. Kifupi Mtu muongo hana haki mbele ya Mungu kwa kuwa amemkubali shetani. Kumbuka aliyoyafanya Askofu Malasusa hayana tofauti na alichokifanya Muadhama kadinali Pengo ya kukana waraka aliosaini baada ya kukamilika kikao cha TEC, na tayari Vatican wanayo taarifa ya tendo ovu alilotenda na maamuzi yaliyoamuliwa yalizingatia muda wake mchache uliosalia. Sijui wewe ni dhehebu gani lakini RC ni dhehebu lenye msimamo mkali na huwa haiogopi serikali hata iwe na ukatili wa kiasi gani wao wanasimama penye ukweli na Magufuri analijua hili. Sasa jiulize kwenye hoja yako mbona kuna Maaskofu na hata Mapadri wa RC ambao ni jeuri kwa serikali lakini bado mnateua waumini wakatoliki? Je huu ni utaratibu unaokubalika au ameutengeneza Magu kwenye awamu hii? Je upande wa Bakwata wameteuliwa waislamu wangapi baada ya viongozi wa Taasisi hii kuwasaliti waumini wao?
Paroko msaidizi

Sijui CCM itaenda wapi hakiyamungu maana wakatoliki tayari wamemuwashia hazad pengo .waislam hawaeleweki. Wa KKKT ngoma imebuma . weraweraaaaa
.....pamoja na mwenzake Pengo!!!hawa watu kuwa viongozi wa dini wali-force tu hawakutakiwa kabisa.
Unaota katoliki Yuko bosi wao Kardinali Pengo
Niliwahi kusema huku kwamba serekali inajichanganya kwa kudhani Pengo ni boss wa wakatoliki hapa nchini, au Pengo anatumia huo mkanganyiko kuwaingiza serekali mjini kwa kuwaambia yeye ni boss wa wakatoliki. Kama mnampa Pengo shavu mpeni lakini sio boss wa wakatoliki hapa nchini.
 
Paschal Matubi nakushukuru kwa dondoo zako. Wanaopinga waje na fact zao vile vile siyo kuongea kwa mihemko. Nchi nyingi zimekombolewa tokana na matamko ya maaskofu wa kikatoliki. Wengine walipoteza maisha sababu ya misimamo yao. Uganda Idd Amin aliona maaskofu ni mwiba akawaua. Bravo Paschal.
 
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
SOURCE: RAIA MWEMA, APRIL 18, 2018, pg. 12
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Ujumbe wa kwaresima umesababisha Polycarp Kardinali Pengo akanukuliwa hivi, “Moja tu ni kwamba barua nzima imechanganya vitu viwili. Mwalimu angekuwepo angepiga kelele na kusema Maaskofu msichanganye dini na siasa, angepiga kelele sana…Katika waraka ule zinachanganywa dini na siasa, hii si kazi ya maaskofu ni kazi yenu wanasiasa CHADEMA, CCM…”: {TUMAINI LETU: Aprili 05, 2018, uk. 02, aya ya nane}.

Oktoba 16, 1970, Rais Julius Nyerere akiwa jijini New York, aliwatembelea masista wa Maryknoll. Walimuomba kuzungumza akatoa hotuba ya kiingereza inayoitwa “The Church and Society”. Sehemu ya hotuba nimeitafsiri hivi,

Kwa karne nyingi, Kanisa, limekubali watu kutumikishwa kwa mabavu, kuteswa, unyonyaji na watawala kutoka nje wala kanisa halikukemea. Hata sasa, Kanisa limekataa kukemea ugandamizaji wa serikali nchini Msumbiji, Angola, Guinea Bissau. Ni kweli miezi iliyopita, Papa ameongea na wapigania uhuru watatu, lakini huu ni mwanzo tu. Bila kukemea kwa sauti na vitendo, Kanisa Katoliki litaendelea kuonekana limekumbatia serikali za kikandamizaji”: {Freedom and Development | Uhuru na Maendeleo, ISBN: 9976400179, uk. 223, aya ya kwanza}.

Rais Nyerere akaendelea kusema, maaskofu wanapokemea ukandamizaji wasiogope “kusingiziwa” kuwa wametumwa na wapinzani, ninanukuu, “Sometimes it will mean the Church leaders involving themselves in nationalist freedom movements and being part of those movements... sometimes it will mean working in opposition to establish authority and power”: {uk. 221, aya ya mwisho}.

Rais Nyerere akaendelea kusema, ziko nchi ambako kanisa lilipokemea ukandamizaji wapo mapadri na maaskofu waliuawa, walifungwa magerezani, waliteswa, walinyanyaswa, walifukuzwa kwenye nchi. Rais Nyerere akasema, wote hao walijitoa sadaka kudumisha sifa kwamba kanisa katoliki lazima litetee haki hata kwa gharama, ninanukuu, “Some of these priests have been assassinated, some have been imprisoned, some have been tortured; some, unfortunately, have been dismissed or re-located by the Church hierarchy.”: {uk. 222, aya ya pili}.

Februari 10, 1981, Rais Julius Nyerere, alihutubia wamisionari wakatoliki waitwao “CIDSE” jijini D’Salaam, akasema,

where the church remained identified with colonial regime to the bitter end, as in Mozambique, it experiences difficult now. Where it was able to identify with politics aspirations of its members and community at large, it has usually been able to avoid conflict with authorrities”: {aya ya 08}.

Hapa Rais Nyerere anasema, “mahali ambapo kanisa liliegemea upande wa serikali kama Msumbiji, sasa baada ya ukoloni limeishia kuchukiwa na serikali, na pale lilipounga mkono siasa za wengi halikuchukiwa na serikali mpya”.

Utafiti wa Frieder Ludwig umeeleza Rais Julius Nyerere alivyoupenda waraka wa askofu Helder Camara wa jimbo katoliki la “Olinda e Recife” nchini Brazil. Waraka huo uliitwa “Gospel and Revolution” yaani “Injili na Mapinduzi” aliutoa askofu Camara kwenye jimbo lake wakati Brazil bado inatawaliwa kijeshi.

Frieder anasema, ilipokaribia Krismas ya mwaka 1973 Rais Nyerere aliusambaza waraka huo kwa maaskofu wa Tanzania na marafiki zake wa nje: {Church and State in Tanzania: Aspects of Changing in Relationships, 1961-1994, ISBN: 9789004115064, uk. 106, aya ya mwisho}.

Hivyo, kufikiria kwamba Julius Nyerere angewakemea maaskofu ni utabiri mgumu kuukubali ukisoma historia.

Sasa tuone matukio ya ukatoliki na siasa za Tanzania. Wamisionari waliwasili Bamagoyo Machi 04, 1868 wakakuta siasa za watawala kuuza binadamu wenzao.

Wamisionari pia walikuta ujinga mwingi unaothibitishwa na watawala walivyosaini mikataba kuuza nchi. Hivyo, walijikita kuokoa watumwa na kufuta ujinga kwa kujenga shule.

Vita ya “Maji Maji” ilianza Julai 31, 1905. Serikali ya gavana iliwatesa kwa njaa walikojificha porini, wakafa takriban watu 300,000: {Scramble for Africa, ISBN: 9780349104492, uk. 622, aya ya tatu}.

Kanisa halikutoa waraka kwa ukatili wa “Maji Maji” kwani wamisionari walipeleka Ujerumani ripoti ya ukatili huo. Wabunge wa chama cha upinzani kiitwacho “Social Democrats” wakaipokea ile ripoti na wakaitetea kwenye bunge la Ujerumani liitwalo “Reichstag”: {The Catholic Church in Tanzania, ISBN: 9976631933, uk. 52, aya ya tatu}.

Mjadala bungeni (Reichstag) kuhusu ukatili wa “Maji Maji” ulisababisha bunge likavunjwa Desemba 13, 1906: {Scramble for Africa, uk. 616-628}.

Machi 25, 1953, Papa Pius XII kwa mara ya kwanza aliipa Tanganyika majimbo 13 na akayateulia maaskofu siku hiyohiyo. Mwaka huohuo maaskofu hao wakatoa waraka wa kwanza nchini, ulioitwa “Africans and the Christian Way of Life” yaani “Waafrika na Njia ya Kikristo ya maisha”.

Waraka huo ulitoka kwa kiingereza na kiswahili, ulielekeza wakatoliki masuala ya siasa. Pia ukafundisha maneno demokrasia, haki za binadamu, dola (state), utaifa, uchumi: {The Catholic Church in Tanganyika, uk. 39-40}.

Hivyo, hao maaskofu, tena wazungu wote kasoro Laurean Rugambwa, walifundisha siasa hizi mwaka 1953 kabla hata TANU haijazaliwa. Kumbe, kutoa waraka unaogusa siasa, ndiyo kazi ya kwanza ya maaskofu wa Tanganyika walipopewa majimbo.

Krismas ya mwaka 1960, maaskofu hao wakatoa waraka ulioitwa “Uhuru na Umoja katika Tanganyika mpya”.

Waraka huo uliwaagiza wakatoliki wajiandae kuisaidia serikali mpya inayokuja ya taifa jipya la Tanganyika, ninanukuu, “All Catholics shall try to help build a soundly Tanganyika, with ever growing dedication and ethuthiasm: {The Catholic Church in Tanzania, uk. 40 na 59}. Hii ni historia fupi ya kanisa na siasa katika Tanganyika.

Msomaji, mkatoliki amefundishwa “Katekism ya Kanisa Katoliki”. “Katekism” ina sura inayoanzia ibara ya 1877 hadi 1948, inayoitwa “Jamii ya Binadamu”.

Hizi “barua” mnazoziita “nyaraka” zinapotolewa na askofu mmoja kama ile ya askofu Helder Camara, au wengi kama ya kwaresima iliyopita, ni maelekezo kutoka hii sura na zingine.

Licha ya “kateskim” Papa John Paul II alileta mwogozo unaoitwa “Compendium of the Social Doctrine of the Church’, kwa kifupi humu ninauita “compendium”. Mwongozo huu ulizinduliwa na Renato Kardinali Martino, Aprili 02, 2004 pale Vatican.

Mkatoliki amefundishwa neno “politic”, yaani “siasa” kwani limetokea kwenye hiyo “compendium” mara 257.

Mkatoliki amefundishwa neno “siasa” kwani limetajwa kwenye “katekism” mara 17 kwenye ibara zifuatazo, {407, 439, 596, 676, 782, 899, 1740, 2108, 2109, 2211, 2237, 2239, 2242, 2243, 2244, 2245 na 2246}.

Mkatoliki amefundishwa neno “demokrasia” kwani limetajwa kwenye “compendium” kwenye ibara 24 zifuatazo, {103, 158, 169, 176, 187, 190, 233, 321, 339, 356, 395, 406, 407, 408, 411, 413, 414, 417, 418, 419, 424, 567, 569 na 572}.

Mkatoliki amefundishwa neno “haki za binadamu” kwani limetajwa kwenye “compendium” kwenye ibara 28 zifuatazo: {152, 153, 154, 155, 157, 158, 159, 166, 187, 270, 283, 319, 365, 366, 388, 389, 399, 402, 404, 407, 443, 485, 494, 496, 505, 506, 514 na 571}.

Msomaji, tuone mifano michache ya ibara hizo. Kama unaifahamu migomo halali ya wafanyakazi basi moja ya ibara zinazomfundisha mkatoliki haki ya kugoma ni ibara ya 304 ya “compendium”.

Ibara ya 400 na 401 ya “compendium” zinaitwa “right to resist” yaani zinamfundisha mkatoliki haki ya kupinga sheria kama hiyo sheria inakiuka kanuni za uadilifu.

Ukiona padre au askofu duniani kahubiri au katoa waraka kuhusu “uhuru wa kupata habari” au tukio kuonyeshwa “live”, basi huyo ametekeleza tulichofundishwa wakatoliki katika ibara ya 414 hadi 416 ya “compendium”.

Ukiona askofu kahimiza nchi kuwekewa vikwazo vya uchumi, basi huyo ametekeleza wakatoliki tulivyofundishwa uhalali wa vikwazo hivyo kwenye ibara ya 507 ya “compendium”.

Ibara ya 398 ya “compendium” inamfundisha mkatoliki kwamba inapotungwa sheria isiyo na mantiki (reason), basi kamwe haiwi sheria, sanasana inageuka tu kuwa tamko la vurugu, ninanunkuu, “When, however, a law is contrary to reason, it is called an unjust law; in such a case it ceases to be law and becomes instead an act of violence”.

Wakatoliki ambao ni wanaiasa upo mwongozo wao alioupitisha Papa John Paul II mnamo Novemba 21, 2002 ukatangazwa na Joseph Kardinali Ratzinger mnamo Novemba 24, 2002 humu nauita “Wakatoliki katika Siasa”.

Ibara ya kwanza ya mwongozo huo inaelekeza kwamba ukishakuwa mwanasiasa uige mfano wa Mtakatifu Thomas More aliyekataa kukiuka haki na maadili.

Msomaji, nimetaja makusudi ili usome “katekism”, “compendium” na mwongozo wa “Wakatoliki katika Siasa”. Nimetaja ibara chache zikuonyeshe kile tunachofundishwa wakatoliki duniani.

Ukizisoma utaona kumbe maaskofu wanapotoa matamko au nyaraka hutawalaumu kirahisi. Sanasana unaweza kuwalaumu kwa nini masuala mengine tunayofundishwa wakatoliki hawayatamki na wanasababisha yanapotamkwa yaonekane kama ni mageni.

Hivyo, Rais Nyerere alivyoshutumu woga wa maaskofu, kama wale wa Msumbiji, hakuleta hoja mpya, kwani kukemea siasa za kikandamizaji ndivyo mkatoliki kafundishwa kama zisemavyo ibara chache nilizotaja.

Maaskofu wa Msumbiji walipoacha woga kanisa likafaulu kupatanisha chama tawala FRELIMO na cha upinzani RENAMO kupitia “wamisionari” waitwao “Sant’egidio” mwaka 1992.

Sasa tuone taarifa ya “instagram” na “facebook” ya mtu aitwaye “Mange Kimambi”, ninainukuu, “..Na nasikia Kadinali Pengo ametakiwa na Vatican kujiuzulu ukadinali. Kwahiyo siku yoyote kuanzia sasa Pengo anavuliwa ukadinali..”, (www.instagram.com/p/BhE6mW-lFWl/?taken-by=mangekimambi_).

Hii “instagram” hii imewafurahisha (“likes”) zaidi ya 22,469. Tusijdangaye. Mange tayari ameshatanguliza mazingira ya mjadala itakapotangazwa Kardinali Pengo kajiuzulu, ndiyo sababu nimeandika makala hii.

Kanisa katoliki lina sheria ziitwazo “Code of Canon Laws”, nitaziita “sheria za kanisa”. Ibara ya 455(4) ya “sheria za kanisa” inasema unapotokea utata kwenye baraza la maaskofu, basi askofu mmoja anaweza kuchukua msimamo tofauti, wala baraza zima au rais wa baraza la maaskofu hana mamlaka kumzuia.

Lakini pia ibara hii inasema askofu anaweza kuwakatalia wenzake kama hoja haina maelekezo ya kanisa. Sasa, je walichohubiri kwenye ujumbe wa kwaresima, hakimo kwenye maelekezo ya kanisa?

Mimi naamini kimo ukisoma ibara za “katekism”, “compendium” na mwongozo wa “Wakatoliki katika Siasa” nilizotaja humu.

Turejee hoja ya kujiuzulu. “Askofu msaidizi” aitwaye “coadjutor” anapoletwa, huashiria kwamba askofu aliyeko madarakani anakaribia kujiuzulu.

Polycarp Pengo alipohamishiwa D’Salaam akawa “coadjutor”, ndipo ikajulikana Laurean Kardinali Rugambwa atajiuzulu siku yoyote, japo ilichukua miaka miwili hadi alipojiuzulu.

Kardinali Pengo hajapata “askofu msaidizi” aitwaye “coadjutor”, ambaye wengine humuita “askofu mwandamizi”. Hivyo, bado ni vigumu kutabiri atajiuzulu lini na nani atamrithi.

Je, askofu huondokaje madarakani? Ibara ya 401(1) ya “sheria za kanisa” inamtaka askofu akifikisha umri wa miaka 75 amuombe Papa ruhusa ya kujiuzulu.

Agosti 05, 2019, Kardinali Pengo atatimiza umri wa miaka 75, hivyo ni kweli kujiuzulu kumekaribia kwani siku 475 zilizobaki, siyo nyingi.

Lakini hata atakapoomba, bado hatutajua ataondoka lini kwani kujiuzulu huanza siku Papa anakapokubali ombi lile.

January 01, 2016, askofu Marc Chengula alitimiza miaka 75, lakini Papa hajaruhusu aondoke jimboni Mbeya. Hivyo, D’Salaam inaweza kubaki na Kardinali Pengo kama Kardinali Rugambwa alivyofikisha miaka 80 ndipo akajiuzulu.

Lakini pia askofu yeyote anaweza kujiuzulu chini ya miaka 75 kama ibara ya 401(2) ya “sheria za kanisa” inavyoelekeza na kama ilivyotokea kwa askofu Wendelin Mtega (miaka 67.7) wa Songea au Fortunatus Lukanima (miaka 57.6) wa Arusha.

Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo, ni kweli na wala haishangazi kwamba anaweza kujiuzulu, ama kwa kutumia ibara ya 401(2) yaani siku yoyote, au kwa kutumia ibara ya 401(1) yaani baada ya Agosti 05, 2019.

Mitandaoni nimeona kambi inapenda Kardinali Pengo aondoke hata dakika hii na nyingine haipendi. Nimeeleza utaratibu ulivyo ili unayependa na usiyependa ujiandae kisaikolojia kwa lolote na siku yoyote.

Sasa, kwa nini kanisani hatutumii neno “retire” yaani “kustaafu”? Kazi ya kanisa ni kutangaza imani. Kitendo cha kusikilizwa kinaitwa “professio” kwa kilatini na anayetangaza anaitwa “professor”, kwa kiswahili “profesa”.

Sasa, “profesa” yaani “askofu” anapotingwa na mambo mengine, hayaondoi utaalamu wake. Hivyo, akitingwa na uzembe au ugonjwa au umri “anajiuzulu”.

Kardinali Pengo alipoongea na wazee alitumia lugha hii, “Hakuna popote ambapo Mungu amewahi kumstaafisha mwanadamu, ila mwanadamu atastaafu akishafika mbunguni”: {KIONGOZI: Februari 02, 2018, uk. 03, aya ya tatu}.

Hivyo, kanisa katoliki halina kitendo cha “kustaafu” au “to retire”, bali lina kitendo cha “kujiuzulu” yaani “ to resign”. Hivyo, kila askofu “atajiuzulu” itakapohitajika.

Ibara ya 402(1) ya “sheria za kanisa” inasema, askofu akishajiuzulu ataitwa “bishop emeritus”. Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo akijiuzulu ataitwa “archbishop emeritus” kama anavyoitwa sasa askofu Louis Lebulu wa Arusha au askofu Wendelin Mtega wa Songea. Sijui neno “emeritus” kwa kiswahili japo wapo wanaopendekeza neno “veterani”.

Lakini kanisa lina njia zingine kumuondoa askofu ofisini, moja ni ile ya kumpa jimbo linaitwa “titular”, yaani jimbo lisilo na muumini hata mmoja.

Askofu Jacques Gaillot wa Évreux, Ufaransa, alitofautiana kila mara na baraza la maaskofu la Ufaransa. Ikiandikwa historia ya maaskofu waliosumbua wenzao, hutamwacha huyu askofu Jacques. Hivyo mwaka 1996 Papa John Paul II alipomuondoa madarakani jimboni Évreux alimpa jimbo liitwalo Partenia ambalo ni “titular”.

George Weigel, hakupenda upole wa Papa John Paul II wa kuchelewa kuwaondoa maaskofu kama hawa: {Pope Benedict XVI and the future of the Catholic Church, ISBN: 9780066213316, pg. 252, aya ya kwanza}.

Je, Polycarp Pengo atajiuzulu “ukardinali”? Maana ya “ukardinali” tutaiona wiki ijayo ambapo tutaona kwamba “ukardinali” ni hali ya kuhesabika uko jimboni Roma.

Kitendo cha kujiuzulu “ukardinali” hakitokei sana kwani hakuna aliyejiuzulu “ukardinali” tangu “mjesuit” padri Louis Billot alipojiuzulu Septemba 21, 1927.
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
umecop n paste andiko langu mbona umefuta contacts zangu chini?
 
Sisi tuna Vipofu na Waweka Pamba Masikioni
 
Maisha ya Bwana Yesu Kristo hapa duniani yalijihusidha vipi na siasa za wanadamu? Maana huyo ndio kioo cha kanisa na hawa viongozi wake Maaskofu.
 
Back
Top Bottom