Kikwete ammwagia sifa Lowassa

Kikwete ammwagia sifa Lowassa

Juhudi za kutunga uongo ni kubwa sana. Kama mgombea anafaa hunasababu ya kutunga uongo kuonyesha anafaa!! Huu unaofanyika na mwandishi wa stori hii ni ushambenga!

mkuu nape, tunashukuru kwa kukanusha huu udaku, lakini ni vyema ukatuwekea uhalisia wa kile kilichozungumzwa kwa faida ya jukwaa
 
mwananchi, tanzania daima are of certain political interest.. be careful you readers
 
Nape anasikia kichefuchefu Jk kamsifia lowasa,kazi ipo ndani ya ccm.....khs nape atafanya kazi gani lowasa akiingia mjengoni....hili sio la kujadili maana 2015 ni chadema magogoni hata nape anajua hilo so hana hofu na nguvu za lowasa.
 
Nape Nnauye; Sasa kutuambia hii habari ni ya kishambenga haitoshi, tuambie ukweli ni upi?
 
Last edited by a moderator:
Kikao hichi kilikuwa cha ndani kati ya Rais Kikwete na wabunge wa CCM.
Nape wewe sio mbunge wa CCM, sijui kama ulihudhuria hicho kikao, na kama ulihudhuria, ulikuwa kama nani?

Haya basi Nape tupe huo ukweli wako unaoujua kama kilichoandikwa na mwananchi ni Uongo.

nape ni kiongozi wa kitaifa tena mjumbe wa kamati kuu wa chama ambacho mwenyekiti wake amefanya kikao na wabunge wake...
 
Ndiyo maana kila siku ninasema kuwa Tasnia ya habari Tanzania kwa sasa IMEINGILIWA. The media is Politically motivated with network of corrupted journalists, reporters, editors and bloggers.

Hii sehemu ya habari imebeba habari nzima. Lakini ukiisoma paragraph kwa umakini utagundua kuwa huyu mwandishi wa habari alikuwa anachanganya UKWELI na UWONGO wa kiwango cha juu katika habari yake kiasi cha kushindwa kuziba mashimo ya mapungufu ya mzizi wa habari yake.

Test ndogo. Kuna sababu gani ya huyo mtu wa karibu kutokuandika jina lake kwa habari ambayo kwa mleta article niya kweli isiyohitaji analysis. Hii ni ishara tosha kuonyesha, nini kilichoko nyuma ya habari yenyewe.

Ngoma ikipigwa sana.....

Mpaka kufika 2015, tutaona na kusikia mengi.

Hakuna tatizo hapo mkuu. Lowassa kaulizwa akawajibu kupitia 'kurugenzi yake ya mawasiliano' tatizo liko wapi?

CC: Pasco
 
Last edited by a moderator:
ccm ni moja daima, watu wanalijua hili ila wanajipofusha na kuziba pamba masikioni
 
Juhudi za kutunga uongo ni kubwa sana. Kama mgombea anafaa hunasababu ya kutunga uongo kuonyesha anafaa!! Huu unaofanyika na mwandishi wa stori hii ni ushambenga!

Yeah_hebu funguka ukweli ni upi mkuu_just to clear up the doubt.
 
Rais Jakaya Kikwete amemwagia sifa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hatua ambayo inaweza kutafsiri mengi katika medani ya siasa nchini.

Akizungumza na wabunge wa CCM kwenye Ukumbi wa White House Dodoma juzi, Rais Kikwete ambaye pia mwenyekiti wa chama hicho, alisema nguvu za Lowassa pekee zinatosha kushinda uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.

Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli, ambako Lowassa amekuwa mbunge wake tangu mwaka 1995.

Habari za kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa Makuyuni, baada ya kuwa ametoa ruksa kwa makada wa chama hicho wanaotaka urais kuanza kujipitisha pitisha miongoni mwa wanachama wa chama hicho. Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa wanaCCM wanaotaka kumrithi Rais Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

"Sina tatizo na pale Makuyuni, najua muscles (misuli) za Mzee Lowassa zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?" alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM akimnukuu Rais Kikwete.

Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Makuyuni unaotarajiwa kufanyika Juni 16, mwaka huu, utakuwa wa ushindani mkali kati ya CCM na Chadema ambao historia yao kisiasa mkoani Arusha ni ya uhasama.

Katika uchaguzi huo, unaofanyika baada ya kifo cha Abdillah Warsama (CCM), chama hicho kitatetea nafasi yake kwa kumsimamisha Godluck Lerunya na Chadema ni Japhet Sironga.

Mbali na Kata ya Makuyuni, uchaguzi wa udiwani mkoani Arusha utafanyika pia katika Kata za Kaloleni, Themi, Kimandolu na Elerai, kutokana na waliokuwa madiwani wa kata hizo (Chadema), kufukuzwa na chama chao.

"Mnaweza kuchafuana leo, kesho mkapata mgombea mwenye nundu nyingi na mabandeji kila mahala, halafu mkapata shida kumnadi," alisema.

Siyo mara ya kwanza kwa Kikwete kumsifia Lowassa kwani aliwahi kufanya hivyo mwaka jana huko Longido wakati akikabidhi ng'ombe.

Pia aliwahi kumsifia wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2010 wakati Kikwete alipomwelezea Lowassa kama Mbunge makini na kuwaomba watu wa Monduli kumchagua tena.

Hata hivyo, alipoulizwa kama baada ya kuruhusiwa kuanza kujipitisha kwa wanaCCM kama anataka kuwania urais, Lowassa alijibu kupitia watu wake wa karibuni kuwa asingependa kuzungumzia suala hilo hasa baada ya Rais kutoa kauli hiyo.

Mwananchi
 
nape ni kiongozi wa kitaifa tena mjumbe wa kamati kuu wa chama ambacho mwenyekiti wake amefanya kikao na wabunge wake...
Bado hujajibu hoja.
Nape sio Mbunge, sasa anawezaje kuhudhuria kikao cha ndani kati ya rais Kikwete na wabunge wa CCM.

Kama issue ni cheo cha kiCCM alichonacho Nape, ndio kusema kamati kuu na secretariety yote ya CCM ilihudhuria au ilipaswa kuhudhuria?
 
Dodoma/Dar es Salaam.

"alisema nguvu za Lowassa pekee zinatosha kushinda uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.
Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli"

"Sina tatizo na pale Makuyuni, najua muscles (misuli) za Mzee Lowassa zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?" alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM akimnukuu Rais Kikwete.


CHANZO: MWANANCHI

...wanataka kumuaibisha huyu mzee ili wapunguze kasi yake ya kuwania uraisi kama walivyo muaibisha kwa Joshua Nasari,walimsifiaaaa akalamba mchanga na shemeji, hubu tungoje hiyo misuli wakati kamanda lema amesha wavua magamba takribani wanamagamba 700 juzi....
 
hofu yangu huyu mwandishi msije kumtoboa macho na kumnyonyoa kucha coz mkiambiwa ukweli mnateka waandishi
Juhudi za kutunga uongo
ni kubwa sana. Kama mgombea anafaa huna sababu ya kutunga uongo
kuonyesha anafaa!! Huu unaofanyika na mwandishi wa stori hii ni
ushambenga!
 
Lowassa ndio Kiongozi mtendaji ndani ya Nchi hii.
KISHINDO KIKUU----->2015
 
fematv.jpg
 
Back
Top Bottom