Kikwete amkemea DC Makonda

Kikwete amkemea DC Makonda

DC ana uwezo wa kupata majibu kutoka kwa wahandisi wa manispaa, they are at his disposal!!!

Suala ni udhaifu tu wa team yake...
Sahihi kabisa ulichokiandika lakini unadhani kabla ya rais kufanya ziara hana washauri? kama DC alitakiwa kuwa na majibu kwa nini hakuwa nayo? Nani aliemteua kwenye nafasi hiyo!!!... mwisho wa siku nani anabeba uzembe wa DCn au team yake?
 
Ki Ukweli Ingetakiwa uongozi wa wilaya, madiwani , mbunge na wahandisi wa wilaya wawe wameshafanya tathmini nini kinahitajika na Kutoa mapendekezo nini kinahitajika kufanyika kwa mpango wa muda mfupi na muda mrefu. Udhaifu wa viongozi wa mccm ndiyo umemfanya jk atamke yote hayo.

Mkuu sikiliza, baadhi ya wakazi wa jiji ni wazi kabisa wamejenga kwenye mikondo ya maji kwa hiyo wamezuia mtiririko huru na sahihi wa maji. Kuna ujenzi horera wa kutia aibu katika hilohilo jiji na mbaya zaidi ujenzi uko mpaka mabondeni eneo ambalo lilihitaji kuwa huru kwa mapokeo ya maji hasa nyakati kama hizi. Wakubwa wanalijua hili na hakuna mwenye uthubutu wa kuondoa tatizo hilo. Mpango wowote wa dharura ni sawa na kuzuia mafuriko kwa kiganja. Je, hali hiyo ni mara ya kwanza kujitokeza?
 
Kunawatu wajinga kweli sasa hapo kamkemea wapi akili za kibavicha bana shida sana.
Mtia NIA ni kwamba 'kukemea' ni tofauti kabisa na 'kukaripia' sasa kwakuwa wewe ni mtu wa 'KIENYEJI' nikusaidie tu kukemea ni kama 'kupunga!' kwa huko kwenu.
 
wewe ulitaka amwambieje? Angeongea taratibu mgesema hana mahamuzi mazito, wabongo bwana kazi kwelikweli!.
 
sasa hapo amemkemea wapi?! mbona ni viongozi wote tu wako hivyo.

Nilipata bahati ya kuona Rais akizungumza na viongozi wa Kinondoni kuhusu mafuriko. Mimi binafsi sijawahi kumwona Rais Kikwete akiwa katika sura ya kuchukia kama jana, mara zote huwa anaongea huku anacheka ndiyo maana huwezi ukajua ni wakati gani amechukia, lakini jana alionekana dhahiri amechukia kwa sababu majibu ya maswali yake hayakuridhisha yalikuwa na ubabaishaji mwingi kama kawaida yao.
 
Wanajamii wenzangu,mimi sikushangaa kumuona mh.rais anampa makavu makonda,kila siku tunasema viongozi wengi serikarini hawana ubunifu,hayo ndio matokeo yake.suala la kutafuta mashine ya kunyonya maji hadi aje raisi akwambie kweli????.wao wanachokijua kila siku ni mipango mikakati tuuuu,saa hizi bil 3 utazipata wapi??madudu ni mengi mno,watendaji mmemwangusha JK sana.mfano uchafu dar es salaam ni haibu kubwa lakini leo hii hadi JK atoe amri ndio viongozi washtuke.kwenye hili la mafuriko viongozi wa dsm mmekosa UBUNIFU kabisa.Wahandisi wa jiji hili HAIBU yenu.
 
JK kwa mashushu watamkoma ... Makonda asahau kurejea katika siasa za Tanzania ....
 
DC aaibisha kabisa, utazani mshona viatu, hajui hili wale lile, walidhani uDC ni mchezo, watu wanaangamia unasema unapanga mipangoi ya muda mrefu huyu kweli hamnazo

Hahaha comment flani so amazing ,chukua like za kutosha
 
simiyu yetu, zimeganda kiasi hata mkikemewa hamtambui? kaangalie tena TV huenda kuna marudio ya taarifa ya habari utaona, na kuelewa kakemewa, vinginevyo sio kosa letu kama huwezi kuelewa kitu on first hearing.
 
Back
Top Bottom