Kikwete amkemea DC Makonda

Kikwete amkemea DC Makonda

Niliitazama ile taarifa na namna walivyokuwa wanajibishana. Kwa mtazamo wangu hata yeye ana matatizo.

Ningekuwa mimi ndiye yeye Rais maelekezo na maagizo yangu yangekuwa "nawapa masaa 48 maji yote yaliyotuwana na kukosa outlet yawe yametafutiwa njia ya kutokea na kila mmoja kwa nafasi yake atekeleze majibu wake na nitarudi tena kuangalia utekekezaji huu na kuwaondolea wananchi adha na mateso wanayoyapata"..

Lakini tulichokiona jana ni malumbano kati ya Rais na watu wanaotekeleza majukumu na wajibu wake kama kiongozi wa nchi na serikali!!
 
Ni baada ya dc Makonda kushindwa kujibu swali aliloulizwa na Rais kwamba ni hatua gani amechukua kushughulikia tatizo la mafuriko pale basihaya Tegeta. DC alisema wanapanga mipango ya muda mrefu ndipo Rais kwa hasira akamwambia yeye anataka utafutwe ufumbuzi wa haraka kwani waathirika wanateseka sana.

Chanzo: chanel ten Habari

Mkuu hapo amemkemea wapi?
 
Usanii huo.. makonda yeye ni kada wa chama, Amuulize mambo ya Magambani,mambo ya mafuriko waachiwe watendaji!!
 
Mmh.. ningekuwa kuwa mimi ndege anayenong'ona ningemnong'oneza Makonda amuulize "Kwani wewe umefanya nini?"

MM halafu akale wapi?Hapo kibarua hicho kukipata ilibidi kumtia adabu Mzee Warioba ndiyo kukipata sasa akiweke kitumbua mchanga Mh!!!!!!!!!!!!!
 
Sasa kama raisi anashindwa kutoa amri kwa viongozi waliopo chini yake unategemea nini .Makonda yule amepewa kazi ambayo ipo juu ya uwezo wake.
 
Du heading imetisha kuliko uhalisia
hebu kaangalie tena hiyo taarifa ya habari,
Mkuu akisisitiza majukumu ndio KUFOKA?
Kwani Makonda ndio kaleta mafuriko?
chuki utazijua tu

Achukiwe ana nini cha zaidi huyo?
wacha kudanganya watu


Du heading imetisha kuliko uhalisia
hebu kaangalie tena hiyo taarifa ya habari,
Mkuu akisisitiza majukumu ndio KUFOKA?
Kwani Makonda ndio kaleta mafuriko?
chuki utazijua tu
 
Paul Makonda alitishia hadi mamlaka iliyomteua kwa kutangaza mgomo wa madereva ikiwa matakwa yao hayatatimizwa. Ndipo nikajiuliza Makonda anawakilisha taasisi gani?
Akishiriki mgomo anamshinikiza nani?
Wananchi wakiteseka kwa ajili ya mgomo, yeye ni kiongozi wa nani?
 
hivikukemea ndio iko hivyo hahahaha
Yule hakukemea chochote. We utakemeaje wakati huo huo una cheka cheka. Body language na alichokuwa anatamka haviendani kabisa. Alikuwa anaongea nao kama washkaji vile. Sasa unakemea halafu wakati huo huo unacheka?
 
Mkuu hapo amemkemea wapi?
Mkuu DC amekemewa ili 'pepo' wa mipango ya muda mrefu amtoke na badala yake achukue hatua za HARAKA kuwanusuru waathirika wale wa mafuriko. Kuna tofauti KUBWA kati ya 'kukemea' na 'kukaripia', teh teh! mjulishe na Simiyu yetu.
 
Nadhani Makonda anafaa sana kwenye mambo ya burudani si mmeona anavyosapoti sekta hiyo? Ameanza na kusaka vipaji Kinondoni, kusapoti Zari All White Party kwa kuwa mmoja wa wahudhuriaji (nahisi alilipia ile ticketi ya 3M pengine akatoa na ofa kwa watu kadhaa). Hayo ya miundombinu sijui wayashughulikie mainjinia wa wilaya bana.

Jitu Kubwa aache uonezi..... kwiikwiiikwiii
 
Anashindwa kutoa maagizo yanayotekelezeka anambana DC mbumbu kwenye uhandisi wa miundo mbinu, yeye mwenyewe kama rais hana jibu sembuse DC...poor me.

DC ana uwezo wa kupata majibu kutoka kwa wahandisi wa manispaa, they are at his disposal!!!

Suala ni udhaifu tu wa team yake...
 
Makonda sasa atatoa wapi fund za dharura kukabili hali hiyo kama sio udhaifu wa mfumo pamaoja na kwamba simkubali makonda lakini kwa hili mtendeeni haki
 
Back
Top Bottom