Kikwete amefanya nini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amefanya nini??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TumainiEl, Feb 23, 2010.

 1. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 3,059
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  Nikiwa kama mtanzania mwenye kuwa na uhuru wakutoa mawazo napenda kutumia fursa hii kutaka kuujuwa ukweli. Nimesikitishwa na utafiti ulio fanywa na Synovate nakusema eti kikwete ana ng'a kwa kupendwa na watanzania. Mim nadhani hawa ni makada wa ccm. Kwa mtu mwenye akili timamu sii rahisi kuamini uwongo huu. Kikwete amefanya nini? Kikwete huyu anayejifanya mtu wa kutaka amani na waujumu uchumi? Kikwete huyu alie tuletea Richmond na atimae kuangushwa baraza la mawaziri? Kikwete huyu alie kuwa Rais wakwanza kuwa na budget kubwa yenye matumizi makubwa ya serikali, Kikwete huyu anae ruka nje kila kukicha nakuacha nchi pasipo muelekeo, Kikwete huyu alie jaza marafiki ktk idara Muhimu huku wakiaribu na yeye kanyamaza kimya, Kikwete huyu anae shindwa kuwa nyooshea kidole viongoz wa Zanzibar wanao utikisa Muungano, Kikwete huyu mwenye maneno mazuri lakin utekelezaji hakuna. Kikwete huyu ambaye ameshindwa hata kuboresha sekta ya elimu, Afya na sekta nyingine binafsi, kikwete huyu ambaye amezid kufanya pengo kati ya masikin na tajir kuzid kuwa kubwa. SHAME UPON SYNOVATE. Naimani tukimpata Rais mwingine after Kikwete basi uwenda ataburutwa maakamani. Anazo kesi zakujibu kutokana na uzembe ktk serikal yake. Hata hvyo nazipongeza idara za usalama wa Taifa, jesh la polisi na JWTZ. Shime Mwamnyange. Mungu ibarik Tanzania.
   
 2. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Kikwete amefanya vyote ulivyovisema na vingine usivyovijua,kwani wee ulitaka afanye nini?
   
 3. I

  Inviolata Member

  #3
  Feb 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You are boring! Kwani mpaka uchangie kama huna la kusema???
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,457
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  We ulitaka watanzania wasemeje?

  Nafikiri wananchi mnawaonea kwa kuwalaumu, au umesahau Makamba juzi Dodoma kasema Kikwete anakubalika kwa 80% kuliko hata chama cha CCM kinachokubalika kwa 65%!

  Hata ukiitishwa uchaguzi leo, bado Kikwete ataongoza pengine hata kwa 98% au zaidi...niulize kwa nini?

  Nafikiri umesikia au umesoma kwamba kwa mara ya kwanza tangu Tanzania iingie kwenye mfumo wa vyama vingi, uchaguzi mkuu wa mwaka huu utashirikisha mgombea mmoja wa nafasi ya Urais ambaye ni Mh. Jakaya mrisho wa Kikwete.

  Jiulize kina Mbowe, Lipumba, Cheyo, Mrema, n.k. mbona wamekimbia msimu huu??? Wanaogopa nini? Tafsiri ya kawaida isiyoitaji sayansi ya kurusha roketi wala utafiti wa redet ni kwamba kila mmoja anaonekana either kukubali utendaji wa Kikwete na ndio maana awaoni haja ya kujitokeza kugombea (yanini kugombea kama aliyeko madarakani anafanya kazi zake kwa ufanisi 'uliotukuka') au wanaogopa kushindwa kwa aibu kwa kutokua na sera mbadala za kushindana na Kikwete.

  Juzi juzi hapa wanasiasa (wasioweza kuficha walionayo mwoyoni) waliowahi kugombea urais chaguzi zilizopita wamejitokeza kumsifia waziwazi Mh. Rais, huku wengine wakisema laiti kama angekuwa rais toka awamu ya pili, wasingehama CCM mfano A. Mrema na John Cheyo). Naamini mtizamo ni huo huo hata kwa viongozi wengine wa vyama vya upinzani (pengine ukiondoa comrade Mtikila), sema tofauti ya kina Lipumba/Mbowe ni kuwa wanaogopa kusema hadharani.

  Wananchi wengi wa Tanzania sio informed, uwezo wao wa kuchambua na kufuatilia mambo ni mdogo, achilia mbali hata kufuatilia utendaji wa Rais wao. Muda mwingi wanautumia ku hassle ili angalau familia zao zipata hata mlo mmoja kwa siku. Huku wenye bahati ya kuwa na luninga, wakiona Rais wao anatunukiwa degree za uzamivu (PhD) Kenya na Uturuki wanaona kwamba Rais wao anakuwa recognized kwa utumishi wake uliotukuka.....kumbe lol!!

  Pia nina maoni tofauti juu ya research methodology zinazotumiwa, ukiangalia aina na uelewa wa respondents napata shida kidogo. je hizo questionnaire ziliuliza maswali vipi? Je respondents waliulizwa rais amefanikiwa katika nyanja zipi? Isije ikawa kwa kumleta Maximo na ivory Coast!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,831
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni

  • unazungumzia hawahawa polisi wanaovunja sheria zote kuanzia barabarani, kwenye selo, mitaani na hata kukosa nidhamu? in a few weeks kumetokea mass murders 2??
  • Jeshi ni hilihili lenye maghala yaliyolipuka mwamunyange akiwa boss? tena bila ya tetemeko la ardhi? je likija hilo tetemeko?
  • yaani wwe hujawahi kuona polisi na wanajeshi wamelewa siku hizi?
  wacha nikushangae tu bana
   
 6. G

  Ghati Makamba Member

  #6
  Feb 23, 2010
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe juu ya uhuru wako wa kutoa mawazo kama raia huru. Ninachokuwa kinyume na wewe ni juu ya matumizi ya uhuru wako wa mawazo ukielekea upande mmoja. Pengine nifahamu unatoa mawazo yako kuonesha mapungufu ya Kikwete ama unautathimini utendaji wake yeye na serikali yake kwa ujumla? "Kwa tamabora zetu watanzania ni vigumu baba kuufahamu uzuri wa bintiye na kutamka hadharani, si kwa sababu haoni ila kwa sababu tu ya utaratibu wa maisha yetu" Subiri, tunaelekea uchaguzi, majirani wataleta posa na hapo utamsifia m-harusi.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...