Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

PHOTOCOPY.

Kwa wale waliokuwa wakubwa mtakumbuka kulikuwa na mashine zinaitwa za Kuburuza. Ninakumbuka kabisa katika shule ya Mwembeni pale mjini Musoma mwaka 1973 mitihani ya SHULE ZA MSINGI, ilikuwa ina 'buruzwa'.

Mwalimu anaanndika kwa mkono halafu zinatolewa nakala kwa kuburuza, sijui kwanini walikuwa wanaita kuburuza lakini Nimeona kwa macho yangu.

Shule za jirani kama Mkendo, Kamunyonge walikuwa wanapeleka kuburuza mitihani pale Mwembeni shule iliyokuwa inamilikiwa na Catholic church lakini ikawa ya serikali. Mwalimu maarufu aliyekuwa anaruburuza aliitwa Elisha Nyamaro.
 
Nakubaliana na wewe rev. kwamba ccm imeoza toka zamani ,huoni watu ni wa fitini sana kumsifia Nyerere kumbe ndo aliozesha mambo yote, hii ni kwa staili mleta maada.

Rev, sio ccm iliyooza ni watanzania karibu wote wenye umri fulani (sitautaja) wamefubaha (bakubhaga) regardless ya chama walichomo.

No! No! MkamaP,
Usifanye makosa kirahisi Mkuu. Tupo ambao tunamsifu Nyerere kuwa ni Baba wa Taifa ambaye kipindi chake cha kuanza kulikomboa na kiliongoza Taifa hili alipata changa moto kali sana kwa kuwa mfumo wa dunia wakati ule ulikuwa mgumu sana. Halafu nchi haikuwa na wasomi wa kuweza kuendesha nchi. Wakati mwingine wale ambao tunaelewa mambo yalivyokuwa hata kipindi cha miaka ya sabini tu wala si nyuma sana, mambo yalikuwa ovyo sana.

Halafu viongozi waliofuata baada ya Mwalimu ndiyo walitakiwa waendeleze kuliimarisha Taifa. Sasa badala yake wako katika juhudi za kuuza nchi. Kwa kifupi tunawiwa kumwonea huruma baba wa Taifa kuwa alitawala kipindi kilichokuwa kigumu sana, kuangalia wenzetu Afrika wakiteswa na kuuwawa, kubaguiliwa, na kudharauliwa kama wanyama.

Nakuhakikishia hilo lilitosha kumsamehe kabisa Nyerere. Wale waliosaidiwa na wanaofahamu maana ya uhuru leo hii watakuambia kuwa hawatamsahau Nyerere. Sisi hatukupitia kipindi kigumu kupigania uhuru wala hatukumwaga damu na kama ilitokea ni kidogo sana ukilinganisha na majirani zetu.

Viongozi waliofuata ndiyo wanaotakiwa kulaumiwa, maana walipoteza dira ya Taifa letu. Wamechafua muungano na umoja wa Kitaifa ambao Nyerere alijitahidi sana kuuunda. Baadhi yetu huwa bado wanabakia kulaumu sana, wapo wanaosema kuwa hakuwatendea waisalamu haki nk.

Wengine watakumbuka kuwa alituweka katika uhusiano mbaya na baadhi ya nchi kama Nigeria alipounga mkono uasi wa Biafra, wapo watakaomlaumu sana kwa kumpa support Savimbi, uhusiano wetu na Angola utaendelea kuwa mbaya kaisi kwa muda.

Lakini nataka tu uelewe kuwa Baba wa taifa aliliongoza Taifa letu kipindi kigumu sana cha siasa duniani. Kipindi cha vita baridi. Kiliendelea mpaka maraisi walioona kuwa hakuna manufaa kwa upande wowote wakaunda shirikisho la nchi zisizofungamana na upande wowote, lakini hata hilo halikusaidia sana.

Kwani nchi za magharibi zilikuwa na nguvu za kiuchumi na kisayansi waliendelea kutawala tena kwa nguvu na uhakika sana. Nchi moja baada ya nyingine zikawa zinaanguka na kuelekea upande wao. Kuanguka kwa Shirikisho la mataifa ya Kirusi kulihitimisha vita hiyo baridi duniani.

Baada ya jambo hili kila nchi duniani ilichukua mwelekeo wake, including China, ambayo mpaka leo hawajaweza kusema kama ni mfumo wa kibepari au la! Lakini nataka tu nifupishe maneno kuwa Nyerere hakustahili tena kubeba lawama za baada yake maana waliofuata walikuwa na wajibu wa kutafuta kwa haraka na umakini na kugundua wapi taifa lielekee. Utafiti huo ulitakiwa uwe wa kisayansi zaidi. Badala yake ukawa wa kichawi au kishirikina zaidi. Ndiyo maana tuko hapa tulipo.

Ndiyo maana unaanza kuona watu wanasema eti "hata yeye alishindwa". Sasa kama yeye alishindwa ndiyo ina maana na wewe ushindwe? Kwanini sasa uligombea uraisi? Maana anayegombea Uraisi wa nchi anatakiwa awe na lengo jema analotaka kulifanyia Taifa. Siyo tu kwenda pale Ikulu kufanya bishara binafsi kama alivyofanya Mwinyi, Mkapa na wanaoendeleza ufisadi.

Kipindi cha Nyerere mtanzania pamoja na umaskini watu tulikuwa tunajiskia vizuri. Kumbuka lile bango moja kwenye yale mazishi ya watu waliouwawa kwenye maandamano ya Arusha kuwa "Ni Bora kufa shujaa kuliko kuishi kwa aibu" Haya ni maneno mazito sana. Sijui kama viongozi wameyachukilia vipi maneno haya.

Kipindi chake Nyerere kilikuwa na mambo mengi sana yaliyolikumba Taifa, lakini hakukaa kimya mpaka kupelekea wananchi kuchanganyikiwa kwa kutopata majibu. Alikuwa na taratibu za kuhutubia Taifa kila jambo linapotokea na kutoa ufumbuzi na jambo jema sana kwake ni kwamba pale alipokosea alikiri tena wazi wazi au hadharani.

Tukizungumzia maswala ya uchumi, Nyerere was a complete failure. Hilo halina ubishi wala mjadala kabisa. Lakini pamoja na hilo ninakumbuka alipokataa kuanza kuchimba madini aina mbali mbali nchini kwa kuhofia wananchi kutopata faida ya madini ya nchi au ardhi yao. Hili mpaka leo tunaliona.

Viongozi wamefikiri kuwa wanatawala wakati muafaka kuchimba madini yaliyoko kwenye ardhi yetu lakini matokeo yake wawekezaji wanachukua zile almasi na dhahabu sisi wanatuonyesha vipande vya chupa na mabati kuwa ndivyo walivyopata tunabakia kuchekelea kama mazuzu! Hii ni pamoja na mikataba feki iliyokithiri serikalini. Si Mwinyi, si Mkapa na si Kiwete wataweza kukana hilo maana taifa limeendelea kudidimia kiuchumi baada ya kuanza kumilikisha wageni machimbo ya vito mbali mbali nchini.

MSAMEHENI NYERERE KUNA ALIYOKOSEA LAKINI ALILIPENDA TAIFA LAKE KWA MOYO WAKE WOTE NA AMELIFIA TAIFA. MPENI HESHIMA YAKE. HASWA BAADA YA KUONA WALIOMPOKEA WANAVYOBORONGA.

RIP MWALIMU.
 
Kwa hiyo unataka kusema hii miradi anayohodhi mkwere ni kujibu maumivu aliyokuwa anayapata kutoka kwa Sayore. Maana kama hapo nyuma kiongozi alikuwa anaruhusiwa kufanya kilimo na kuuzia jeshi kwa nini sasa hivi mkwere alipoleta RICHMOND/DOWANS kuzalisha umeme nyie watanzania mnaleta fitina?

Kwani Sayre alipokua akiuzia maziwa Chuo cha jeshi kulikua na athari gani kwa Taifa???
 
Mimi mtu wa fitna ni huyu anayekuja na stori hizi leo, kwanini hawakuzitoa 2005 hizi fitina? Tuseme tu jamaa ameshindwa kuongoza, badala ya kuanza kuingiza mambo ya ajabu ajabu kabisa.

If you don't know the past... you don't know the future....
 
PHP:
Basi huo ndiyo ukawa mwishi wa JK monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama...lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!! Hicho ndicho chanzo cha JK kumchikia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadileo! yeye humwita mzee nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita father of our nation, laikini ni pale napotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....

JK ni mtu wa visasi kwa hiyo hili halinishangazi hata kidogo....................................na JK humkuza sana Kawawa kwa kumbeba bila ya kujua hata kawawa alikuwa kwenye mbeleko za Nyerere.....................................
 
Hata wakati ambapo ujamaa ulikuwa umeshika kasi..mwalimu hakuwa na tatizo kabisa na viongozi waliokuwa wakijifugia au kulima kama familia....mwenyewe alikuwa akiwataka kila kiongozi kuwa na shamba la mfano kwenye ule mpango wa KILIMO CHA KUFA NA KUPONA.

Yeye mwenyewe alionesha mfano kwa kulima butiama ..na mkewe alifuga kuku wengi sana msasani ...akishirikiana na wanae....na kuku wale aliwauza kwenye mahoteli ya wakati huo.......

KAWAWA alikuwa na mashamba yake ya mahindi dodoma,na ruvuma [mtakanini] kama mashamba ya mfano ...waulizeni kina Vita....na mahindi ya kawawa aliyauza kwenye mashule .....yote hayo ilikuwa kuhakikisha viongozi hawawi makupe...kila mmoja anatakiwa kuwa na shamba la mfano.....

So naweza kumuelewa mwalimu kwanini hakuona mantiki kwa Kikwete kumtuhumu kiongozi anayeuza mazao ya shamba lake au mifugo........sasa mlitegemea Jeshi lisinunue chakula tu kwa sababu ni sayore......mwalimu hakufanya kosa kabisa ..kumwambia Msuguri wamalize wenyewe......[hakuwa na nia mbaya....alitaka waelezane kwenye vikao yaishe]

Musuguri alitumia aproach ambayo sio nzuri....kumpambanisha moja kwa moja JK na Sayore......labda ni katika ile imani ya jeshini kuwa Majungu hayatakiwi....na maatatizo yote yanatakiwa kuelezewa bila woga kwenye vikao vya kambi...Jk alikuwa na fursa hiyo na hakuitumia jambo ambalo liliashiria ana nia mbaya na mkuu wake..

Haata siku hizi nimepata kuongea na maafisa wengi wanasema jeshini sio ajabu kabisa kukuta mtu anapeleka mashtaka kwa siri ....kuitwa kwenye kikao na yule aliyemtuhumu kutakiwa aeleze wazi mbele yake....hawataki majungu kabisa...unless umepeleka taarifa inayohatarisha usalama wa nchi ie mapinduzi au uasi ..hapo mtoa taarifa hulindwa ..lakini haya majungu ya kawaida ..

You have to prove!!!
 
Kama kuna chumvi mno hii story!!

Haya mazungumzo btw JK na Sayore huwa yanafanyikia wapi jamani na wewe unakuwepo?Hilo ni moja.
Pili, hivi najaribu kuangalia jiografia.... Monduli hadi Usa river? Mtoa hoja unaijua Arusha vizuri? Mbona ni njia ambazo hazikutani ? Ungesema alitokea Monduli uchochoroni ( na sijui ni upi) maana ni Maasai plains hakuna hata misitu uje hadi Burka Coffee estate, ukatize uingie mjini Arusha..... uje hadi Usa River??..Haiji kabisa.....
WOS,

Kama umeelewa somo, tunaambiwa kwamba JK alitoroka kwenye kikao baada ya Mkuu SAYORE kugawa barua(ya FITNA)) kwenye kikao akiacha wazitazame, na yeye (sayore)kutoka nje.

JK alitambua ambacho kingefuatia... hivyo aliamua kutoroka KWA KUPITA NJIA ZAKUJIFICHA!(hapo ndio kwenye ishu)..
Asingeweza kufuata barabara, maana alijua angeshikwa, kama wewe umeshawahi kufika Monduli, utaijua ile barabara ya kutoka Monduli kikosini hadi kuikamata barabara kuu ilivyonyooka, na hivyo asingewahi kuimaliza angeshikwa fasta, na option ya kupanda gari ndio usiongelee, maana asingeenda mbali, lakini pia magari ya kule yote yalikuwa ni ya kijeshi(hasa kwa enzi zile).

Chakufanya ilikuwa ni kukatiza kwa njia za porini...Zipo njia nyingi san kutoka Monduli kwenda mjini Arusha bila kufuata barabara!
Na tunaposema porini, si lazima iwe MSITU....NI NJIA YOYOTE ISIYOKUWA OFFICIAL, hivyo usitafute msitu hapo.
LAKINI UKUMBUKE PIA JK alikuwa Mwanajeshi, hivyo ujue alikuwa amehitimu masomo ya kijeshi kama MM(Mbinu za Medani etc), ambapo KUTEMBEA PORINI NI ISHU KAMA CHAI TU, na sehemu kubwa ya mafunzo inafanyikia huko...Hivyo hakuna sababu ya njia ZOZOTE kukutana, kama unavyotaka wewe iwe, wajeshi hawahitaji njia nyoofu!

Hivyo sioni uzito wa hoja yako ya kushangaa jiografia ya Arusha na kutembea Porini.
 
Mimi mtu wa fitna ni huyu anayekuja na stori hizi leo, kwanini hawakuzitoa 2005 hizi fitina? Tuseme tu jamaa ameshindwa kuongoza, badala ya kuanza kuingiza mambo ya ajabu ajabu kabisa.

Nadhani historia kama hii ya huyu jamaa itatupatia mwanga kidogo wa swali la msingi la kwanini jamaa ameshindwa kuongoza. Wakati mwingine ni vizuri kurudi nyuma kwenye historia ya mtu ili uweze kumfahamu vizuri. Ni sawa tu na ambavyo daktari huwa wanauliza mpaka habari za magonjwa ya wazazi ili tu waweze kupata sababu za magonjwa yanayomsibu mgonjwa wanayemshughulikia.
 
Hata kama hatumpendi lakini Kikwete asingeweza kufanya ujinga huo. Mwalimu hakuwa kiongozi wa kuachia watu wayamalize wenyewe. Hiyo hufanywa na viongozi waoga aina ya Kikwete.
 
Bwana Phillemon, nimekupa thanks kwa sababu umegusia kiini cha kisa hiki. Katika professional army hakuna nafasi ya fitna na hata kama una malalamiko kuhusu mkuu wako kuna utaratibu wa kufuata huwezi kuandika barua kwa amri mkuu wa jeshi. Ila pia kama nafasi ilikuwepo ya kujieleza Kikwete angetumia nafasi hiyo badala ya kukimbia.
 
Hata wakati ambapo ujamaa ulikuwa umeshika kasi..mwalimu hakuwa na tatizo kabisa na viongozi waliokuwa wakijifugia au kulima kama familia....mwenyewe alikuwa akiwataka kila kiongozi kuwa na shamba la mfano kwenye ule mpango wa KILIMO CHA KUFA NA KUPONA.

Yeye mwenyewe alionesha mfano kwa kulima butiama ..na mkewe alifuga kuku wengi sana msasani ...akishirikiana na wanae....na kuku wale aliwauza kwenye mahoteli ya wakati huo.......

KAWAWA alikuwa na mashamba yake ya mahindi dodoma,na ruvuma [mtakanini] kama mashamba ya mfano ...waulizeni kina Vita....na mahindi ya kawawa aliyauza kwenye mashule .....yote hayo ilikuwa kuhakikisha viongozi hawawi makupe...kila mmoja anatakiwa kuwa na shamba la mfano.....

So naweza kumuelewa mwalimu kwanini hakuona mantiki kwa Kikwete kumtuhumu kiongozi anayeuza mazao ya shamba lake au mifugo........sasa mlitegemea Jeshi lisinunue chakula tu kwa sababu ni sayore......mwalimu hakufanya kosa kabisa ..kumwambia Msuguri wamalize wenyewe......[hakuwa na nia mbaya....alitaka waelezane kwenye vikao yaishe]

Musuguri alitumia aproach ambayo sio nzuri....kumpambanisha moja kwa moja JK na Sayore......labda ni katika ile imani ya jeshini kuwa Majungu hayatakiwi....na maatatizo yote yanatakiwa kuelezewa bila woga kwenye vikao vya kambi...Jk alikuwa na fursa hiyo na hakuitumia jambo ambalo liliashiria ana nia mbaya na mkuu wake..

Haata siku hizi nimepata kuongea na maafisa wengi wanasema jeshini sio ajabu kabisa kukuta mtu anapeleka mashtaka kwa siri ....kuitwa kwenye kikao na yule aliyemtuhumu kutakiwa aeleze wazi mbele yake....hawataki majungu kabisa...unless umepeleka taarifa inayohatarisha usalama wa nchi ie mapinduzi au uasi ..hapo mtoa taarifa hulindwa ..lakini haya majungu ya kawaida ..you have to prove!!!

Mantiki ipo ndugu yangu. Siku hizi tunaiita mgingano wa kimaslahi (conflict of interest). Mkuu wa chuo ana shamba la mifugo na kilimo halafu anauza mazao chuoni ambapo yeye ndiye anaamua bei atakayojilipa yeye mwenyewe.

Katika hali kama hii inatakiwa kuwe mchakato huru kuhakikisha kuwa huyu mkuu hatumii vibaya madaraka yake kujinufaisha kwa gharama za mwajiri wake.
 
Kwa iyo JK haugraduate monduli?
Sihitaji kufuatilia zaidi lazima itakuwa kweli
 
Mantiki ipo ndugu yangu. Siku hizi tunaiita mgingano wa kimaslahi (conflict of interest). Mkuu wa chuo ana shamba la mifugo na kilimo halafu anauza mazao chuoni ambapo yeye ndiye anaamua bei atakayojilipa yeye mwenyewe. Katika hali kama hii inatakiwa kuwe mchakato huru kuhakikisha kuwa huyu mkuu hatumii vibaya madaraka yake kujinufaisha kwa gharama za mwajiri wake.

Unachosema ni kweli mkuu lakini tatizo linabaki kuwa njia iliyotumika kuwasilisha malalamiko hayo na baadae kuchukua uamuzi wa kuingia mitini baada ya kuona siri imefichuka!!
 
Regardless of there is proof on not but that is how JK behave!! ni m2 wa visasi sana na wivu wa kutosha!! its very disgusting to have a president like this!!!
 
Watu wanasema siku ya kifo chake alikuwa na mazungumzo marefu na mwanae Adam - ya kuanzisha chama cha upinzani!

Kighoma alianzisha chama chake cha siasa [ NRM] ambacho kiliegemea sana kwenye dini yake; hata baada ya kifo chake mwanae huyu Adam aliendelea kuwa kiongozi wake !! Sasa hivi eti nae anajiita kada wa CCM na mkwere kampa unaibu waziri!! Pumba tupu.
 
aahaaha! aahaa! aahaa! Mkwere teh! teh! HII NI TRUE STORY Aisee! Copy zilikuwepo zile za kuburuza, hakuna cha kutilia shaka, nadhan km mwandishi alivyosema, naamin vituko vyake vingine vingi vimemiss teh! Mzee wa fitna hana swaga!
 
119 Reactions
Reply
Back
Top Bottom