Kikwete alitumia uchawi gani?

Kikwete alitumia uchawi gani?

Kama una akili timamu jiulize japo hata kidogo....hivyo vyuo vilikuwa na ubora gani kielimu? Barabara zilikuwa zinajengwa baada ya wiki mbili kwisha zinaharibika kwa rasharasha ya manyunyu ya mvua na rais bado tu anachekelea makandarasi. Kaingia Magufuli na wataalam wake, makandarasi kibao wamefutiwa leseni kutokana na kugundulika kuwa fake. Majengo mengi ya ghorofa na ya kisasa kabisa yaliporomoshwa chini ya kiwango na rais bado tu alikuwa anacheka. Vihiyo na wajinga wengi ndiyo walikuwa wafanya kazi katika idara nyeti serikalini na ufanisi wa kazi ulikuwa hakuna kutokana na watu kutokuwa na ujuzi wa kazi. Almashauri zilishindwa kufuatiliwa, bandari ndiyo usiseme. Jiji lilizidi kuwa chafu wakati rais anachekelea tu kuona uchafu umezagaa mjini. Ufisadi ulikithiri huku wanafunzi ambao ni taifa la kesho wakizidi kukaa chini ya minazi na miembe kusoma, rais anacheka tu na kudanganya wadanganyika kuwa hii nchi ni masikini sana huku yeye na genge lake wakizidi kuneemeka. Mungu aliona mateso wapatayo watanzania na kuhamua kutuletea Magufuli. Kwa vyovyote vile, vihiyo na wabangaizaji wengi watalia na kulalama juu ya hili. Mwenye akili hawezi kamwe kumlaumu Magufuli kwani afanyayo yeye si mageni duniani ila hapa Bongo tunaona mageni na unyanyasaji kwa sababu watu walizoea kubangaiza na kutopenda kufanya kazi.
Well said. ...usiwaamshe walio lala waache wabaki hivyo hivyo. .....MUELIMISHE MWENYE HEKIMA AZIDI KUPATA HEKIMA. ...very powerful word!
 
JK alikuwa sio mpenda sifa, alikuwa na hekima na busara, alisaidia kukua kwa demokrasia ila huyu mpenda sifa ni janga la kitaifa

Usiongee kwa hasira baada ya kunyimwa tonge. Mla ndezi (Mkere) aliyumbisha sana hili taifa na kama angeendelea kutawala basi tungefirisika zaidi. Mla ndezi hakufaa kabisa kutawala hii nchi ama nchi yeyote ile kwani alikuwa hana dira ya maendeleo bali hasara tu. Alidumaza akili za watanzania wengi na kuona kuwa Ikulu ni sehemu ya kwenda kupunga upepo na kula maandazi as they wished. Matokeo yake sasa, watanzani wengi walizidi kuwa wajinga na mpaka sasa bado hawajahamka. Kikwete inabidi akamatwe na kushitakiwa, hakufaa kuwa rais wetu.
 
Utakuwa wa Gwajima , maana nyie ndo mlikuwa mnaimbishwa kila siku ubaya wa JK kanisani kwenu! hii nchi haitokuja kukaa ipate a very smart president kama JK! subiri maisha yazidi kuwapiga ndo utajua JK alikuwa mchumi alojua jinsi ya kuutricle down uchumi ili kila mtu aishi maisha ya kiutu!
 
Unataka kutwambia JPM hakuifanya kazi yake vizuri?, maana yeye ndo alikuwa bosi na msimamizi mkuu wa hayo mabarabara

Ndiyo, na alivunjwa moyo na mkuu wake kwani alikuwa si mfuatiliaji wa vitu. Yeye alitaka tu watanzania wafaidike kwa fursa no matter the cost.
 
Wote tulilaumu ufisadi

Kodi zilikuwa hazilipwi?

Rais aliitwa dhaifu kwa kutokuwa mkali!

Wana ccm wakabadili gia Dodoma na kuhama!

Rais alikuwa anasafiri karibu kila mwezi

Lakini barabara zilijengwa, Vyuo vikuu na shule nchi nzima.

Majengo ya kisasa na upanuzi mkubwa wa miji wenye majengo ya kisasa kabisa!

Watumishi wa umma na wafanyabiashara walineemeka!

Na Rais wetu alikuwa full kutabasamu, urais kwake ilikuwa kitu kidogo kama ukiranja wa zamu tu!

Leo sasa!

Kila kitu kimerekebishwa, na rais hacheki cheki!

Lakini Mambo yamezidi kuwa magumu, na hata mwenyewe amesikika akisema anajutia uamuzi wake wa kukitaka kikombe hiki!

Je, ni wakati wa kurejea kupata semina elekezi toka kwa "mkwere"?

Au Mkuu apitie tu kisirisiri hadidu za rejea za serikali ya "mkwere" ili mambo yasiende mrama!
MTAFUTENI MCHUNGAJI TANZANIA ANAJUA YOTE NA YALE USIYOPATA KUSIKIA BADO
 
Chini ya Kikwete deni la taifa lilifika trl 40. Mambo uliyotaja yalifanywa kwa mikopo badala ya mapato ya ndani na kwa kua uthibiti ulikua mdaifu mikopo mingine iliishia mifukoni mwa watu. Ndio maana Tanzania inaitwa shamba la bibi kwa kuwa wajanja wachache walitafuna fedha ya ndani kwa kutolipa kodi.
trilion 40 toka trilion ngapi?,
kwani sasa mnajenga reli kwa pesa zipi,za ndani au za mkopo?
 
Utakuwa Msukule wa Gwajima , maana nyie ndo mlikuwa mnaimbishwa kila siku ubaya wa JK kanisani kwenu! hii nchi haitokuja kukaa ipate a very smart president kama JK! subiri maisha yazidi kuwapiga ndo utajua JK alikuwa mchumi alojua jinsi ya kuutricle down uchumi ili kila mtu aishi maisha ya kiutu!

Bado uko usingizini, pole kwa kukurupuka kujibu bila kusoma. Nobody has to tell me or Mtanzania yeyote yule juu ya utawala mbovu wa Kikwete. Mawaziri wake tu walikuwa wanamdharau na kumcheka na ndiyo maana they never worked because alikuwa si mfuatiliaji wa vitu. Mimi sina shaka na utawala wa JPM because nimesoma na ninafanya kazi kihalali hivyo sina shaka kutumbuliwa. Vyeti vyangu ni halali na siogopi kufanya kazi because ninajiamini kutokana na elimu yangu. Vihiyo mtalia sana mwaka huu na msipo angalia mtakuj kujiua.
 
Huo unafiki wenu wabongo hautaisha aliyepondwa jana leo anasifiwa...anayesifiwa leo huenda kesho akapondwa.
Na hayo yanafanywa kwa sababu jana hakugusa maslahi yake, leo ameyagusa.
Magufuli anaongoza nchi kwa maslahi mapana ya umma na sikufurahisha na kuneemesha kikundi cha watu na wazalendo wa kweli wanayaona mazuri aliyoyafanya kwa muda mfupi aliokaa madarakani na wapi anatupeleka kama Taifa.
Lakini kikubwa tufanyeni kazi, riziki zitapatikana katika kufanya kazi na si kwa kuchonga deal kama tulivyokuwa tumezoea.
kama kazi gani labda?,ambayo sasa watu hawaifanyi na inatakiwa ifanywe ili mambo yawe mazuri?
 
Uliza deni la taifa lilifikia sh. ngapi?

Uliza mikataba iliyo sainiwa (juu ya malia asili) leo bado inakunufaisha?

ILIKUWA FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE. JE TUENDELEE NA STYLE KAMA HIYO?
Kwani huyu wasasa kalipa deni aliloacha mwenzie?
 
kama kazi gani labda?,ambayo sasa watu hawaifanyi na inatakiwa ifanywe ili mambo yawe mazuri?
Wewe unataka yawe mazuri kivipi nje ya kipato chako halali.
Mafanikio duniani wakati mwingine hutegemea na mungu amekupangia nini fanya kazi huku ukimtanguliza mungu kama wewe ni wa mafanikio utafanikiwa tu
 
Uliza deni la taifa lilifikia sh. ngapi?

Uliza mikataba iliyo sainiwa (juu ya malia asili) leo bado inakunufaisha?

ILIKUWA FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE. JE TUENDELEE NA STYLE KAMA HIYO?

Bajeti ya kwanza ya Magufuli amekopa trilion 7 kwa ajili ya kuendesha nchi.
Wachina wakaja kuongeza deni la trilion 15.
Matumizi yake huruhusiwi kuhoji, utaishia ndani kama Lissu.
 
Wewe unataka yawe mazuri kivipi nje ya kipato chako halali.
Mafanikio duniani wakati mwingine hutegemea na mungu amekupangia nini fanya kazi huku ukimtanguliza mungu kama wewe ni wa mafanikio utafanikiwa tu
kwahiyo tusubiri majaliwa ya mungu siyo?.
 
Uliza deni la taifa lilifikia sh. ngapi?

Uliza mikataba iliyo sainiwa (juu ya malia asili) leo bado inakunufaisha?

ILIKUWA FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE. JE TUENDELEE NA STYLE KAMA HIYO?
Unaongea pumba tupu umesoma budget ya mwaka huu??? Ndugu amekopa zaidi ya mkwere tukubali tukatae hali ni ngumu tunapoelekea hatukujui mbaya zaidi tunabahatisha hatuna strategy yeyote ya maana ya kututoa hapa tulipo zaidi ya blah blah tupu.
 
Hebu mwenye kuelewa mipango kàmili ya awamu ya tano aje hapa na atuelimishe sisi vile.aza!
  1. Wizara ya elimu inamikakati gani na imeandaliwaje?
  2. Nyumba na makazi wao wana mpango gani, na tunaanza lini na hatua za utekelezaji zipoje?
  3. Afya wana mikakati gani na utekelezaji umepangwaje?
  4. Je, bajeti hii ya 2016/17 imereflect hayo yanayosemwa?
Ugomvi wetu wengine upo padogo tu! Hatukubali serikali iendeshwe kwa imani tu! Yes raisi anadhamira njema kuliko yeyote labda hata zaidi ya Nyerere, lakini dhamira yake inakuwa reflected vipi katika mipango yake!
Mfano! Katazo la ada, lilibaki kuwa dhamira tu lakini kumbe halikuwa na mikakati thabiti! Zuio la uingizwaji wa sukari nalo ni katazo tu halikuwa na contingent plans!
Sasa na hii nchi ya ahadi hatuwezi kuifikia kwa imani tu, tunataka mipango!
Hebu leteni hiyo mikakati ya wizara hizo tatu naahidi nitakaa kimya milele kuhusu utendaji wa serikali!
 
Bado uko usingizini, pole kwa kukurupuka kujibu bila kusoma. Nobody has to tell me or Mtanzania yeyote yule juu ya utawala mbovu wa Kikwete. Mawaziri wake tu walikuwa wanamdharau na kumcheka na ndiyo maana they never worked because alikuwa si mfuatiliaji wa vitu. Mimi sina shaka na utawala wa JPM because nimesoma na ninafanya kazi kihalali hivyo sina shaka kutumbuliwa. Vyeti vyangu ni halali na siogopi kufanya kazi because ninajiamini kutokana na elimu yangu. Vihiyo mtalia sana mwaka huu na msipo angalia mtakuj kujiua.
NILITAKA NIPITE TUU BILA KUSEMA NENO.
Ki - UKWELI JK alikuwa Rais Bora. Aliheshimu utawala wa sheria na uhuru wa mahakama. we felt proud of being Tanzanian. Kwa kiasi aliheshimu uhuru wa bunge na kufanyia kazi maazimia mengi ya Bunge.

Mimi bado nashangaa suala la Kuhamia Dodoma. HIVI BAJETI YAKE IMEPITISHWA NA BUNGE LIPI???
 
Best management style: MANAGE YOURSELF BY HEAD AND MANAGE OTHERS BY HEART.

What if you manage others by head? JPM style - you will lead without concrete development plans!
 
Rais aliitwa dhaifu kwa kutokuwa mkali!

No. Mimi naona alikuwa mkali sana na alikuwa anasikiliza sana utashi wa wananchi. Alichukua maamuzi magumu ... ya kuwapumzisha wateule wake wengi tu ... akina Lowassa, Mkulo, Mulugo, Tibaijuka, Ngereja, Muhongo, Nchimbi, Matayo, n.k.

Kodi zilikuwa hazilipwi?

Ongezeko makusanyo unaoonekana sasa hivi ni fake ... kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu ya kushuka kwa thamani ya TSh (ilikuwa 1700 October mwaka jana; sasa hivi ni 2200). JPM na genge lake wamefanya mud-sliding mno. Kodi zilikuwa zinalipwa tu, kama ni ukwepaji haukuwa mkubwa kiasi hicho.
 
Wote tulilaumu ufisadi

Kodi zilikuwa hazilipwi?

Rais aliitwa dhaifu kwa kutokuwa mkali!

Wana ccm wakabadili gia Dodoma na kuhama!

Rais alikuwa anasafiri karibu kila mwezi

Lakini barabara zilijengwa, Vyuo vikuu na shule nchi nzima.

Majengo ya kisasa na upanuzi mkubwa wa miji wenye majengo ya kisasa kabisa!

Watumishi wa umma na wafanyabiashara walineemeka!

Na Rais wetu alikuwa full kutabasamu, urais kwake ilikuwa kitu kidogo kama ukiranja wa zamu tu!

Leo sasa!

Kila kitu kimerekebishwa, na rais hacheki cheki!

Lakini Mambo yamezidi kuwa magumu, na hata mwenyewe amesikika akisema anajutia uamuzi wake wa kukitaka kikombe hiki!

Je, ni wakati wa kurejea kupata semina elekezi toka kwa "mkwere"?

Au Mkuu apitie tu kisirisiri hadidu za rejea za serikali ya "mkwere" ili mambo yasiende mrama!

uko serious? haujui ni mikopo ile??
 
Back
Top Bottom