Elections 2010 Kikwete alitukuta hivi, katuleta hapa; atatuachaje 2015?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
520
Tunapoelekea 2015; ni vema kutathmini na kuweka kumbukumbu sawa kwa Rais wetu Kikwete tangu alipoingia madarakani 2005 hadi sasa anapoelekea mwisho. Tujikite kwenye Uchumi, Miundombinu/ Ujenzi, na siasa.

Thamani ya shingi:
2005, Usd 1=Tsh 600, leo usd 1 ni sh. 1,600/-.

Bei za bidhaa
2005; Sukari kg. 600/-, leo ni shs 2,000/-
Mkate gm 250, shs. 300/-, leo ni shs 1,000/- . Wenye takwimu endeleeni kutupa data.
 

Buyengwa

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,159
10,290
2005----kilo moja ya maharage tsh. 500-600, leo ni tsh. 1300-1500!!
2005----kilo moja ya mchele tsh. 600-800, leo ni tsh. 1200-1600!!


 

conversant

Member
Jul 12, 2011
60
7
Mkuu kwenye exchange rate umedanganya kwa uthibitisho ingia kwenye website ya bot wanazorecords za 2005 duh! Usitumie uongo mkuu kuelezea dukuduku lako ni Kweli mambo sio mazuri bt jaribu kutumia ukweli 'you cant bring a solution without understanding a real problem' mkuu inaonyesha uelewa wako baado kabisa
 

mzalendofungo

Member
Feb 15, 2011
46
4
Tatizo watanzania wengi hatuko tayari kuelewa, na hii nchi itauzwa na watu wake wote.
Hali ni mbaya sana na hakuna mtetezi, Mungu ibariki Tanzania.
 

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,470
9,013
jipe moyo mkuu maana uwepo wa JK una maana kubwa sana kwa Watz zaidi ya unavyodhani.
Si unajua mwanafunzi akiwa anajiandaa na mtihani kwa ajili ya maisha mazuri ya mbeleni ni lazima akeshe macho na kujinyima sana wakati wa maandalizi.
Pia chukulia mchezaji anayetaka kuwa bora ni lazima apande milima sana na kufanya mazoezi kwa ajili ya hizo dakika 90 tu!
hivyo hivyo jk amekuwepo kwa ajili ya kutupitisha katika hicho kipindi (epoch) cha uzoefu na ndio maana miaka hii sita wananchi wanaelewa kutafuta hata takwimu kama hivi na kulinganisha na wana (wameongeza) upeo mkubwa sana wa kuchanganua mambo ya siasa na mengineyo kwa upana zaidi ya hizo siku zilizopita, wanaelewa makosa na kupatia, uongo na ukweli nk. Naamini kabisa pamoja na ujio wa technology inayotuwezesha kujua 'wasinziaji' kwenye mikutano na uelewa mdogo wa sheria walizoapa kuzilinda kama Mh. Mkuchika, kuna vitu vingi tumevijua kama wananchi ambavyo bila ujio wa JK labda ungesubiria mtu aliye similar naye ambayo ingekuwa nadra!
"Jikaze mkuu na tuombe uzima" (ndiyo statement iliyobakia kwa Mtz kama mimi ...na wewe!??)
 

gmosha48

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,400
1,468
1) Mfumuko wa Bei ( Inflation) December 2005= 5.9%, Sasa hivi August 2011= 14.1%, Maana yake; kila shilingi 100 tuliyokuwa tunatumia mwaka 2005, shilingi sita zilikuwa sababu ya mfumuko wa bei lakini sasa tunalipa shilinggi 14 zaidi sababu ya mfumuko wa bei.

2) Nakisi ya bajeti ya serikali ukilinganisha na pato la taifa 2005= -3.0, 2010= -6.9 maana yake : serikali ya sasa inatumia kuliko inavyoweza kukusanya mapato na misaada. Matkeo yake: Deni la taifa linaongezeka kwa kasi kubwa!
 

Capitani

Member
Sep 7, 2011
79
14
2005 ufisadi,wezi wa mali ya uma kwa njia yoyote ile ilikuwa 5% leo hii hayo hayo ni 50%. je mwanachi mwadilifu asiye kuwa na (access)uwezo wa yakuyafikia maslahi ya taifa hali yake ikoje. kipimo unacho mwenyewe. Kila eneo limejaa wizi, ulaghai,ujanjaujanja,tu. Imani za watu zimekwisha wapo wachache saana walibakia na wanajaribu kupigania kurdisha maadili mema lakin bado kuna kazi kwelikweli. Hapa ndipo tulipo.
 

shaluu

Member
Jul 17, 2011
11
1
Kikwete amefanya kazi bora kwa kuimarisha amani nchini Tanzania kwa miaka hiyo yote.;)


Jamani kama ni suala la amani JK alitukuta nayo wala hajaongeza chochote...sanasana naona anaongeza chuki kutokana na kubebabeba watu ovyo, kama kuteua ma RC walioshindwa Ubunge
 

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
520
Mkuu kwenye exchange rate umedanganya kwa uthibitisho ingia kwenye website ya bot wanazorecords za 2005 duh! Usitumie uongo mkuu kuelezea dukuduku lako ni Kweli mambo sio mazuri bt jaribu kutumia ukweli 'you cant bring a solution without understanding a real problem' mkuu inaonyesha uelewa wako baado kabisa

Heri yako unayechenji dola zako BOT, njoo huku kwetu tunaotumia Bureau de changre uone. Ukienda CRDB au NMB, utakimbia maana utakuta dola 1=tsh 1660/-! Heri Bureau
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,669
30,117
Tunapoelekea 2015; ni vema kutathmini na kuweka kumbukumbu sawa kwa Rais wetu Kikwete tangu alipoingia madarakani 2005 hadi sasa anapoelekea mwisho. Tujikite kwenye Uchumi, Miundombinu/ Ujenzi, na siasa.

Thamani ya shingi:
2005, Usd 1=Tsh 600, leo usd 1 ni sh. 1,600/-.

Bei za bidhaa
2005; Sukari kg. 600/-, leo ni shs 2,000/-
Mkate gm 250, shs. 300/-, leo ni shs 1,000/- . Wenye takwimu endeleeni kutupa data.
sikumchagua so hainiumi.
 

sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
20
Mwenye bei ya nyama tafadhali atusaidie,pia na mafuta(diesel na petrol)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom