Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 132
- 541
ZITTO KABWE: MIAKA MINNE YA MAGUFULI DENI LA TAIFA LIMEONGEZEKA SAWA NA MIAKA 10 YA KIKWETE.
Na: Suphian Juma
Wakati Serikali ya Magufuli inajinasibu kuwa ya wanyonge na kwamba Rais Magufuli ndiye Rais pekee kupata kutokea tangu tupate Uhuru na kwamba kama kuna tatizo kubwa la kitaifa halijatatuliwa na yeye awali hii, hapatatokea Rais mwingine atakayekuwa na ubavu wa kulitatua; Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT wazalendo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hususani Twitter ameonesha takwimu na hivyo kusikitishwa na ongezeko la Deni la Taifa lisilomithilika.
Hapa nimewasogezea mtiririko wa 'tweets' (posts) nne ambazo Zitto ameziandika kupitia Twitter leo Sept 27, 2019.
1. Deni lote la Taifa ( Ndani na Nje ) limeongezeka kutoka shilingi Trilioni 43 mwaka 2015 Wakati Rais Magufuli anaingia madarakani mpaka shilingi Trilioni 65 mwezi Julai 2019! Ongezeko la Deni kiasi cha shilingi Trilioni 22, sawa na kukopa 5.5tr/mwaka, 0.5tr/mwezi, 17bn/Siku.
2. Serikali ya Awamu ya Tano imefikisha Deni la Nje USD 22 bilioni ndani ya miaka 4 tangu iingie madarakani. Serikali ya Rais John Magufuli katika miaka 4 imeliingiza Taifa katika Deni la USD 7 bilioni sawasawa na Deni lote lililokopwa katika miaka 10 ya Rais Jakaya Kikwete.
3. Serikali ya Awamu ya 4 ilipoingia Madarakani Deni la Taifa la Nje lilikuwa USD 8 billioni ( Novemba 2005 ). Wakati inaondoka madarakani, miaka 10 baadaye, Deni la Nje lilikuwa limefikia USD 15 bilioni ( Novemba 2015 ). Ongezeko la USD 7 bilioni.
4. Septemba 2015 gharama ya mishahara ya Wafanyakazi ilikuwa shs 523 bilioni. Mwaka 2016 na 2017 wakaondolewa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki. Gharama ya mishahara July 2019 ni shs 566 bilioni. Hakuna ajira mpya kiivo. Hakuna nyongeza ya mishahara kisheria, wafanyakazi wanalia kila siku. Wanaopanda vyeo hawalipwi mishahara ya vyeo vyeo vipya ( wafanyakazi wa Umma wanalia kila siku ). Masikini waliostaafu miaka 2 iliyopita mpaka leo hawajalipwa. HATUDANGANYIKI.
Kwakuwa Watanzania sio wajinga, nadhani ni vyema sasa tukatafakari kwa kina suala hili, tukizingatia tunavyozidi kuwa maskini kila uchwao tofauti na miaka iliyopita kabla ya 2015. Na kwamba kama dhumuni la kuwa na Serikali na Rais Mpya ni kuwa na maisha bora, na dhumuni hili halijatimia, je bado tutamchagua tena Magufuli 2020 au badala yake tutahakikisha tumchagua Rais Mpya, Serikali Mpya na Chama kimya Ikulu ili kuirejesha NCHI kwenye MISINGI ya MATUMAINI kwa VITENDO?
TUTAFAKARI.
ACT wazalendo tupo nanyi DAIMA!
Suphian Juma
Sept 27, 2019
Singida.