Kikwete, akutukanaye hakuchagulii tusi!

o9.jpg

Picha hii weka maneno yako mwenyewe kuhusiana na Kanada kumpa zawadi ya jezi rais Jakaya Kikwete.

Bora nijipe tu moyo kuwa amebadilishana zawadi kwa yeye kutoa hilo sanduku la Zanzibar na kupewa hiyo jezi. Mtu ukijifanya kufikiria zaidi utaugua kwa hasira na aibu bure. Its just a photo no more no less!
 
Mkuu yaani tunashangilia Presidaaa wetu kupewa jezi yenye jina lake halafu tunanyamaza wakati wao wakija kuchukua madini na gesi yetu kwa bei ya kutupa..! Halafu wanasema ati wanamuenzi Nyerere..?
Dah,huyu jamaa ni janga la kitaifa wallah...yaani anapewa pampasi anakenua menooooo.
 
Sijawahi fedheheka kiasi hiki, sijui kwa nini leo nimejisikia vibaya juu ya hii picha hata ikiwa kwamba nimezoea mambo ya huyu Mheshimiwa lakini hii hapana.

Pole ndugu yangu, tutafanyaje sasa. Hii ndio style yake.
 
Viongozi wa ulaya wanapo kuja hapa kwetu alafu sisi tunawapa vibyago wakati wao wameleta mabilioni ya hela za msaada hapa inakuwaje?
Vinyago vibyago tu vya Masai kashika mkuki n.k.
Hii ni aje!

Jezi hio ni symbolic tu, acheni chuki za kifala hizo.
 
Zawadi inatakiwa isiwe kitu chenye thamani( itakuwa ni hongo)
Zawadi inatakiwa ka kitu kadogo tu ku show appreciation( hili ndo la msingi) hapa.

APPRECIATION Ndo msingi sio value ya zawadi. Alafu mnachaguaje zawadi ya kupewa? Nyie vipi?
 
Kama tumelogwa vile, sasa kwenye shughuli hii ya kiserikali hatutajadili nini kama taifa tume-ji-commit kwa Canada au nini kama Taifa tumepata, au yapi yamejadili yanayotuhusu.... real bad.
 
hapo tafsiri yake ni kwamba: KIKWETE ni kati ya wachezaji waliyosajiliwa kwa mkopo katika timu ya kuimarisha UCHUMI wa Canada, timu hiyo inao wachezaji ambao ni viongozi legelege na vibaraka wa nchi zinazoendelea "wazee wa ndiyo mzee" kwa kila kitu wanachoambiwa na wenye timu. Natamani ningekuwa na muda ningekupangia first eleven ya hiyo timu, pamoja na rizevu. Tumekwisha kudadadadadadeeeeeeekkkhi. Si walishamjua ni easy come easy go?
 
Back
Top Bottom