Kikwete, akutukanaye hakuchagulii tusi!

Kikwete, akutukanaye hakuchagulii tusi!

o9.jpg

Picha hii weka maneno yako mwenyewe kuhusiana na Kanada kumpa zawadi ya jezi rais Jakaya Kikwete.

Nakumbuka kwa mara ya mwisho Waziri Mkuu wa Canada Bw. Halper kuja nchini kilikuwa ni kipindi ambacho JK ametangaza kufanya reviews za mikataba yote ya madini na akaunda tume ya Bomani aliyoipa kazi ya kuchunguza nini tatizo kwenye sekta ya madini na kwa nini kama taifa hatufaidi. Hakuna kilichofanyika yuko kimya. Dkt. Muhongo anajing'ata amekwama. Zitto kelele zake zimeenda na maji. Wote tuko gizani hatujui kitu.Gas na mafuta yanatafitiwa na hata vzimba vimeshagawiwa bila sera, sheria wala mpango mkakati wowote.

Alipokuja Halper (Sitaki hata kukumbuka mwaka), watoto wa shule hapa nchini walipangishwa foleni wakiwa wameshika bendera ndogo za Canada, nakumbuka sana. JK alifanya naye mazungumzo Ikulu na mara moja JK alinukuliwa akiwa South Africa baada ya kukabwa na waandishi akisema kuwa, kamwe hatutavunja mikataba iliyopo ya madini ikiwemo ya Barrick. Kipindi hicho kulikuwa pia na maandamano ya kuipinga Barrick almost Ulimwengu mzima kutokana na maafa ya kiuchumi na kimazingira inayosababisha kwenye sekta ya madini. Latin America, Barrick ilikuwa inapingwa kwa maandamano.

Sasa awamu hii JK karudi kwa Halper Canada, kapanda Punda na kapewa jezi isiyo ya 1st Eleven. Tutegemee gas na mafuta kuchotwa na Wacanada. Hakika, miaka hii miwili na ushee iliyobaki ya JK ni jehanamu kwetu. Halper anataka gas na mafuta baada ya Barrick kuchota kila kitu kinachoitwa madini nchini. Ni pembe nne inayotengenezwa na JK ya kutafuna rasilimali za nchi.

Nililijiuliza maswali mengi sana. Membe alikuwa Marekani kwa nini JK hakumtuma majukumu hayo yanayompeleka sasa huko? Ina maana Membe angetibua michongo ya JK? Nashindwa kupata majibu. Ina maana msafara wa JK alioenda nao huko Marekani na Canada haujui kabisa nini JK kafuata huko? Hawawezi kutumegea hata kidogo? Ni kweli JK kaenda kupanda punda na kupewa jezi tuu? Hapana. Tusubili tuone kitakachojiri. Siamini.
 
Wanamsanifu kuwa yeye ni "playboy", kumbuka pia alipewa jezi ya chicago bulls na rais bush, wameshamjua huyu
 
hebu cheki hii exhange
jk canada marekani
gold jezi jezi
gesi .? vyandarua,
mikataba umeme vyandarua
 
Mtusaidie wengine mambo ya soka yametupita kando, hii ni jezi ya timu ya taifa ya Canada?
 
Nilikuwa nimeacha Laptop Mezani, akaja First born (8 years old) wangu kuichezea chezea, Bahat Mbaya ndo kwaanza nilikuwa nimefungua hii Thread, ile kuona hiyo Picha ya Mkwe.re na Jezi akauliza Baba huyo ndo Mafisango na Kocha wao Mpya????
Nimejisikia aibu saaaaaana japo Simkubali Mkwe.re na CCM
 
Tusubiri Akienda Oman Sijui watampa nini?Coz ndiyo safari inayofuata.Tutakoma mpaka amalizime muda wake tutakuwa tumebaki nyakakanya
 
Kiwete kapewa jezi ya kichina wakati yeye katoa sanduku exclusvely handmade lenye nakshi za dhahabu

Wenzetu hawafikirii zawadi kwa mintaraf ya kima chake cha fedha, isipokuwa kima cha hisia 'emotional value' Ni kweli JK ametoa chest yenye thamani lakini Herper ataivallue kwa nakshi yake na labda aina ya mti. Hatauliza ni dola ngapi hii.
 
Nilikuwa nimeacha Laptop Mezani, akaja First born (8 years old) wangu kuichezea chezea, Bahat Mbaya ndo kwaanza nilikuwa nimefungua hii Thread, ile kuona hiyo Picha ya Mkwe.re na Jezi akauliza Baba huyo ndo Mafisango na Kocha wao Mpya????
Nimejisikia aibu saaaaaana japo Simkubali Mkwe.re na CCM

Yaani 8 years hajui picha ya Rais wake? anasoma shule?
 
Wenzetu wanatucheka kwa jinsi tunavyojipendekeza kwao na kugawa mali zetu huku tukiishia kuwa ombaomba bila sababu. We simply just need president with just common sense.
 
Zawadi ni zawadi, watu wanaokota majani ya maua yaliyoanguka una appreciate na kulizika.
Masikini hupenda zawadi za gharama kubwa, wakati tajiri anapenda zawadi ya ku appericiate jinsi ulivyotumia mda na kufikiri kuwandalia zawadi.

Kisaikolojia hiyo zawadi ni zawadi murua kabisa, maana hai demand any return, ama ku- compromise sensitive decisions .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom