Kikwete ajisafisha Dowans

rais kuongea maneno ya namna hii ni mpumbafu na ujinga wa hali ya juu...asifanye watu watoto hapa na majibu yake ya hovyohovyo...kwanza nani kamuuliza mpaka anaanza kufafanua ...stupid

Umeyasikia au unatoa comments bila ya kufanya tathmini? Naona kama unaropokwa vile!
 
As usual no specifics, not objective but suitable to the intended listeners (CCM and the apologists). Just one thing in mind JK asije kuruka haya aliyoyasema na kutuambia ilikuwa ni maoni yake binafsi!!!!
 
Hi siku ile alionguka jukwaani pale jangwani ilikuwa tarehe ngapi vile?labda zinarelate na hii ya leo
 

Hivi wewe umefarijika kwa lipi.Mimi ningefarijika tu kama Kikwete na washirika wake wangefikishwa the Hague ingawa najua nayo ni mahakama ya kitapeli.
 
yaonekana umeisikiliza hotuba kwa umakini.kuna sehemu rais anakiri kwa kinywa chake kwamba hata ndugu zake wanafahamu kuwa yeye ni msema hovyo.utuwekee ile hotuba ambayo haijahaririwa!
Bahati mbaya hotuba inayosambazwa ni ile official transcript ambayo imekuwa whitewashed. Ni kweli kasema yeye ni "msema ovyo" hata kwenye Baraza la Mawaziri.
 
Raisi wangu na Mwenyekiti wa Chama Cha CCM ametamka, ametoa kauli ambayo ilikuwa itolewe zaidi ya miezi mitatu sasa. Hii hotuba na hasa kipengele kinachohusu Dowans ilitakiwa mwishoni mwa 2010. Aliogopa nini kusema kama kwa dhati kabisa aliyosema sasa ndio msimamo wake?

Napata mashaka na Raisi wangu anapokimbilia 'akutakanaye hakuchaguliwi tusi'. Sidhani kuna mtu anayekuwa na msimamo tofauti eti kwa kuwa anamtukana Rais. Sidhani kupingana na hoja ni kumtukana mtu. Naogopa tunaelekea mahali tukibishiwa hoja tunaichukulia chuki, tunaona ni tusi badala ya kufikiria jinsi ya kuijibu. Tena wakati mwingine tunapaswa kuwa wanyenyekevu, tukiri pale hoja inatuonyesha tulikuwa tumekosa.

Naamini safari bado, na ninaamini kina Msekwa na wazee wengine humo CCM, wanayo bado nafasi ya kurekebisha hizi hisia, maana naona ndio chanzocha kutoelewana kwa taifa. Kiongozi asiyepingwa! Kiongozi ASIYEPINGWA! Tafsiri yake nipeni! Je kiongozi asiyekuwa tayari kupingwa anaitwa nani?
 
Umefahamika Mwenyekiti...

Yaani hii ni kali kiongozi anasikilizia kwanza, anavizia na baadae anakurupuka eti hata yeye alikuwa sahihi. Wakati juzi tu hapa kuna magazeti walianza kumpamba eti yuko kimya kwa sababu suala hilo liko mahakamani. No wonder why hilo linchi ni kuongea ongea tu na hakuna hatua zinazochukuliwa. Your guy is just an empty suit period!!!!!!!!!
 
"...Naomba kila mkoa na wilaya watuletee orodha ya yale tuliyoaahidi ili tuyatengenezee mipango ya utekelezaji..."
 
hii prepared transcript sicho alichokisema
 

Mtu anyetoa majibu ya kihuni naye ni mhuni..Nina hitimisha, Jakaya mrisho kikwete naye ni mhuni kwa majibu yake ya kihuni.
 
"...Naomba kila mkoa na wilaya watuletee orodha ya yale tuliyoaahidi ili tuyatengenezee mipango ya utekelezaji..."

Wenzio wanawaza uchaguzi 2015 sasa zile ahadi zitaongezwa zingine usijali!
 

Just another proof that the guy is incompetent!!!!!!
 
"Kwa maneno mengine, Chama cha Mapinduzi kiige tabia ya nyoka ya kila baada ya muda fulani hujivua gamba lake na kupata jipya. Hatuna budi kufanya hivyo na kufanya hivyo sasa."

mytake:
Mwenyekiti keshashauri wawe na tabia ya nyoka mjanja kuliko sasa walivyo kama nyoka mjinga ambaye anang'ata hovyohovyo... Yaani walete DOWANS ingine lakini katika sura mpya kabisa, ufisadi ufanyike kwa njia za kisasa, wezi walindwe kitaaalamu zaidi na CCM iendelee kuwazuga wananchi kuwa wanawasaidia kwa danganya toto tuu lakini NYOKA NI YULEYULE JANA LEO NA HATA MILELE KWA NGUVU,ARI, KASI ILEILE JAPO KWA KUZUGA ZAIDI!!
 
Kweli sasa tuhakikishe JK akimbia nchi tuweke warrant yake na kufanya kila kitu kumkamata. Wewe kama kiongozi wa nchi na Tanzania ina watu millioni 42, wanachama wa CCM let say 200,000 na hapo hapo unashikilia jeshi la polisi, upelelezi, jeshi la ulinzi na hapo hapo pia unashikilia Bunge. Unajua JK na CCM wanafikiri Watanzania wa leo ni ignorant na wavivu kama wale waliokuwepo enzi za Azimio la Arusha. Hatua gani alichukua baada ya Bunge kuchunguza Richmond na kujua hii ni kampuni fake? Kwanini Kikikwete alimlazimisha Lowasa ajiudhuru? Kwanini alihusika katika maamuzi ya kupeleka Dowans ICC badala ya criminal court? Kwanini alikaa kama mwenyekiti wa Kamati Kuu na kuhidhinisha kwa mara nyingine tena Dowans walipwe wakati 99% ya wananchi hawataki serikali ilipe wezi CCM? Mpaka sasa tunaweza kusummarize yafuatayo:
1. JK anaongea sasa kudanganya wananchi ili donors waendelee kumwamini na kumpa funds zaidi ili waendelee kuiba na kujitajirisha. Hili Wananchi tutafanya kila njia kuzuia JK na CCM kujisafisha haraka haraka
2. JK anaongea sasa kwa sababu CCM na tawi lao CCM wanajua kuna maandamano makubwa yanakuja na mengi yamepangwa mwezi huu kumfukuza yeye na chama chake. Katika hili sijui kama JK na CCM wamefanikiwa lolote

"Uchafu ni Uchafu siku zote hata kama ukijaribu kuusafisha na kuupamba hautabadilika. CCM na JK ni wachafu kupindukia"
 

Chochote kinachotoka kwa huyu jamaa hakistahili hata kukisikiliza maana siku zote ni ..... TUPU! Eti chaguo la Mungu! Mungu hawezi kutuchukia Watanzania kiasi hiki na kutupa the so called kiongozi ambaye ameshindwa kwenye kila kitu pamoja na madaraka makubwa tuliyomkabidhi.
 
Mbona cc ya ccm ilisema wanawategemea wanaharakati waliopeleka suala la kukataa kuilipa dowans mahakama kuu,leo jk anasema wanasheria wa serikali na wa tanesco ndio wanaofuatilia suala hilo?hapo nimechanganyikiwa
 

Tatizo la Rais wetu ni ndumilakuwili au popo haijulikani yupo kundi gani.Kwani akiwa kwa mafisadi anasema hivi na akija kwa wanainchi anasema lile.Tatizo anataka kupendwa na pande zote huku akijua wanainchi wanaumia.SI HUYU ALIMPIGIA KAMPENI MRAMBA mnakumbuka alisemaje?Fanya wewe kosa kama la Mramba kama hujafia jela! INAUMIZA SANA Katika hii demokrasia yetu hapa Tz.TUNGEOMBA RAIS Awe Specific ili tujue yuko wapi sio kutuzunguka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…