SEAL Team 6
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 655
- 118
JK na Membe wameaibika kweli. wanajishaua ni jinsi gani watafanya kwa sababu kunatetesi kwamba wao ndiyo wanaomhifadhi Gadaffi.
Tanzania haiwezi kutambua serikali ya waasi ambao hawajaapishwa wala hawana mihimili mitatu ya dola.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kiongozi wa Serikali ya Mpito ya Libya,
Mustafa Abdel-Jalil , jijini New York, Marekani,
ambako wote wanahudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa.
Wiki chache zilizopita serikali ya Tanzania kupitia waziri wa mambo ya nchi za nje Membe ilisema haitambui serikali ya mpito ya Libya na kumshinikiza balozi wa Libya nchini kutoendelea na zoezi la kuipeperusha bendera ya serikali mpya mlingotini, bali bendera la Gadafi ndiyo inayotambuliwa,
Je, serikali yetu itarudishaje kauli yake ya kutoitambua serikali mpya ya Libya wakati kiongozi wake kapokelewa umoja wa mataifa?
Candid Scope, Tanganyika hakuna serikali kuna makundi ya majambazi tu ambayo sifa yao kubwa ni kugombana mchana lakini usiku wote wanakuwa wahalifu. Ukifuatilia resolution za Kikwete utakuwa chizi
Lao moja,hawezi kukataa kuitambua nchi bila Rais kuamua,mimi uwa hainisumbui kufuatilia kauli za serikali,uwa ni kama vile the comedy,jambo moja linaweza kutolewa kauli hata tano tofauti,cha msingi elewa kuwa Tanzania ni bendera fuata upepo katika masuala ya kimataifa,masuala ya ndani ni kuangalia aliyesema yupo kundi gani!zaidi ya hapo utaumiza kichwa tu.Hayo yalikuwa ni maneno ya Membe, na si Kikwete. Hamjui serikali yetu kila mmoja anafanya lake?
Uvivu wa kufikiri. Mazingira hubadilika kutoka na maendeleo on the ground. Hawa NTC sasa wameunda serikali ya mpito na hata wameunda baraza la mawaziri na sasa hiyo ni serikali tofauti na wakati ule. Hata serikali yetu ikiwatambua leo watakuwa wamefanya linalostahili kwa wakati huu. lakini ulidhani kwamba kama mtu humtambui basi hata salamu usimpe?