Kikwete aitambua serikali ya mpito Libya?

JK na Membe wameaibika kweli. wanajishaua ni jinsi gani watafanya kwa sababu kunatetesi kwamba wao ndiyo wanaomhifadhi Gadaffi.
 
Jamani msisahau na kuumiza vichwa ile saaana,kwani ya Madagascar na Rajoriena ilikuwaje?Afrika haiweza hamua chochote katika mambo yakimataifa.We are followers and recipient.It will take centuries to stand on our own thinking and decisions.
 
09_11_wv3b4y.jpg

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kiongozi wa Serikali ya Mpito ya Libya,
Mustafa Abdel-Jalil , jijini New York, Marekani,
ambako wote wanahudhuria mkutano wa 66 wa Umoja wa Mataifa.​



Wiki chache zilizopita serikali ya Tanzania kupitia waziri wa mambo ya nchi za nje Membe ilisema haitambui serikali ya mpito ya Libya na kumshinikiza balozi wa Libya nchini kutoendelea na zoezi la kuipeperusha bendera ya serikali mpya mlingotini, bali bendera la Gadafi ndiyo inayotambuliwa,

Je, serikali yetu itarudishaje kauli yake ya kutoitambua serikali mpya ya Libya wakati kiongozi wake kapokelewa umoja wa mataifa?

Sasa ule msikiti na magari aliyohongwa atarudisha?
 
Kitu sijajuwa ni iwapo aibu ni ya Membe na Kakae au ni yetu sote watanzania!
 
Kauli za Membe Ni upuuzi mtupu! Membe na wenzake hata wasipoitambua serikali ya NTC Libya hawabadilishi chochote! Ghadaf kwisha pigwa dafurao. Alafu upuuzi mwingine ni kauli kuwa seriakali haiwezi kupinduliwa kwa pick up kasahau hata manati na mashoka yanapindua serikali achilia mbali hizo pick up. Najua Membe kilaza hata Mapinduzi ya Zanzibar kayasahau. Isue sio pick up bali serikali kupoteza uhalali wa kutawala na hatimaye kuondolewa hata ingekuwa kupigwa teke. Acha wasiitambue. Lakini kesho utamkuta Membe anawalamba viatu wale alosema hawtambui.
 
Serikali yetu ya kishenzi tu tena haina maana yoyote kabisa ktk macho ya kimataifa wanatucheka. Membe juzi tu kasema na kukemea balozi wetu wa libya aliyekuwa ameshajua nini kinaendelea eti ashushe bendera mpya serikali zinazoongea ili zionekane zipo hatuna serikali kabisa
 
Hayo yalikuwa ni maneno ya Membe, na si Kikwete. Hamjui serikali yetu kila mmoja anafanya lake?
 
Candid Scope, Tanganyika hakuna serikali kuna makundi ya majambazi tu ambayo sifa yao kubwa ni kugombana mchana lakini usiku wote wanakuwa wahalifu. Ukifuatilia resolution za Kikwete utakuwa chizi

Uvivu wa kufikiri. Mazingira hubadilika kutoka na maendeleo on the ground. Hawa NTC sasa wameunda serikali ya mpito na hata wameunda baraza la mawaziri na sasa hiyo ni serikali tofauti na wakati ule. Hata serikali yetu ikiwatambua leo watakuwa wamefanya linalostahili kwa wakati huu. lakini ulidhani kwamba kama mtu humtambui basi hata salamu usimpe?
 
Hayo yalikuwa ni maneno ya Membe, na si Kikwete. Hamjui serikali yetu kila mmoja anafanya lake?
Lao moja,hawezi kukataa kuitambua nchi bila Rais kuamua,mimi uwa hainisumbui kufuatilia kauli za serikali,uwa ni kama vile the comedy,jambo moja linaweza kutolewa kauli hata tano tofauti,cha msingi elewa kuwa Tanzania ni bendera fuata upepo katika masuala ya kimataifa,masuala ya ndani ni kuangalia aliyesema yupo kundi gani!zaidi ya hapo utaumiza kichwa tu.
 
Hata kama haitambui ana mbadala!?
Kwa utaratibu wetu wa kuwasubiri 'wakubwa' waanze kusema ndipo na sisi tusema tutazidi kupata shida!
Wale ambao tumewafanya kuwa wasemaji wetu wanapochelewa kusema, tunashindwa kujibu maswali ya wale 'wenye kimbele mbele!'
 
Uvivu wa kufikiri. Mazingira hubadilika kutoka na maendeleo on the ground. Hawa NTC sasa wameunda serikali ya mpito na hata wameunda baraza la mawaziri na sasa hiyo ni serikali tofauti na wakati ule. Hata serikali yetu ikiwatambua leo watakuwa wamefanya linalostahili kwa wakati huu. lakini ulidhani kwamba kama mtu humtambui basi hata salamu usimpe?

Sometimes kukubali makosa ni uungwana!!!!! Mabosi wako na wewe mlichemka wakati ule, na kama mlilijua hili la mazingira kubadilika basi majibu yenu yangekuwa na busara zaidi. You can not be flip flopping continuously na kutengezeza visingizio!!!!!
 
yaani hili jukwaa huwa laniharibia siku.. siasa za kipuuzi... uharo..
 
Back
Top Bottom