.. huyo mama aliyeinamisha kichwa kidogo afanane na festiledi? Ila hicho kitambaa ambacho kina uso wa mheshimiwa ikiwa inaelekea pembeni na inachekelea kwa furaha inaleta 'disturbing picture sana' hizi sare za CCM hazivutii sijui kwa nini :confused2:
Ila kwa mawazo yangu:
Mama aliyeinama lazima aliwaza "Mungu wangu! Not again! Je tutafika?"
Mama kushoto aliyefumba macho: "Aiseee!" alikuwa anaogopa hajui mheshimiwa amedondoka sababu gani ie kazirai au kibaya zaidi...
Mama wa pili kulia anayehangaika na begi "Sijui simu yangu nimeiweka wapi? Hii lazima nipige picha!"
Mama kulia kabisa "Mtajiju!" keshachoka kuona sinema inarudiwarudiwa
Jamaa mwenye pete (Edwin?): "Aiseeee! Nakwambia ni mpaka chini!"
:smile-big: