GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

GE2010 Kikwete aanguka ghafla Jangwani...!

Mkuu, sikumbaliani na wewe 100% kila wakati ila unanichekesha sana.... na hii clip naona ndo "kichaa kapewa rungu!"
On a more serious note: inatisha sana kuangalia mkuu wa nchi ana-collapse hivi, haipendezi! Inabidi kweli akapumzike.... na wapambe aachane nao maana wao wanataka kuendeleza ulaji they do not have his best interest at heart.
 
Unajua sikuamini macho yangu! Yaani mjamaa anadondoka tu kama...... na bado anang'ang'ana kwenda mjengoni. Kuna nini kule?
 
Warekebishe sheria ya uchaguzi kwa kuweka kipengele cha kumdisqualify mgombea ambaye ataonyesha tabia ya kuanguka katika majukwaa ya kampeni -- tehe tehe tehe!!!!
 
Sheikh Yahya:Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete

September 15, 2010 na Mwandishi: Raiamwema:

  • Asema hahitaji ruksa ya CCM, serikali
  • LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kumkana, Mnajimu maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein, ameibuka na kusema kwamba hahitaji kibali katika kumwekea "ulinzi wa majini" mtu anayempenda - Rais Jakaya Kikwete.
  • "Sheikh alisema binafsi hahitaji kumshirikisha mtu katika hili. Serikali iendelee na ulinzi wake na yeye atatoa ulinzi wake. Mbona hao walinzi walikuwapo lakini akaanguka? Matatizo yale si ya kiafya. Sheikh anafanya kwa kuwa anampenda na hutasikia tena anaanguka."
  • Awali Sheikh Yahya alinukuliwa katika taarifa yake akisema kwamba atatoa ulinzi usioonekana kwa macho kumkinga Rais Kikwete ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia ‘mchezo' wowote kama ilivyotokea Jangwani.
    Endelea kusoma hii link Sheikh Yahya:Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete
 
Huko Arusha vipi jee huyu mjamaa. hajadondoka? Nasikia ni spana mkononi!
 
Hivi hakuna angle nyingine ya video ya kuonyesha jinsi mjamaa alivyodondoka? Hii haionyeshi vizuri kwani wapambe waliwahi kumuekea kinga! Mwenye nayo atuwekee hapa!
 
Huko Arusha vipi jee huyu mjamaa. hajadondoka? Nasikia ni spana mkononi!

Tokea yamkute yale ya Jangwani siku hizi misafala yake yote ina ambulance isiyokuwa ya kawaida is more like mobile intensive care unit!
 
Jamani hebu nijuzeni -- hivi ni kweli katika helikopta zile tatu moja ni full ambulance kutoka Afrika ya kusini?
 
Dr. Slaa,
if proved to be true, wala usiogope, waeleze wananchi ukweli kwamba mpinzani wako analazimika kutembea na chopa kadhaa mojawapo ni ambulance!!
Huyu bwana asilazimishe, anatakiwa ang'atuka sasa.
 
Halafu nasikiavyo haruhusiwi kuhutubia zaidi ya dak 20 katika mkutano wowote wa kampeni, kutokana naushauri wa madaktari. Wanaogopa akizidisha tu huenda akalamba mchanga!
 
Halafu nasikiavyo haruhusiwi kuhutubia zaidi ya dak 20 katika mkutano wowote wa kampeni, kutokana naushauri wa madaktari. Wanaogopa akizidisha tu huenda akalamba mchanga!

Nami pia nimesikia hivyo. Watu hawa wanaomzunguka wana wasiwasi wakaja kumkosa mtu wa kuwalinda na ufisadi wao in the next 5 yrs!!!!
 
Jamani hebu nijuzeni -- hivi ni kweli katika helikopta zile tatu moja ni full ambulance kutoka Afrika ya kusini?

Jana hiyo helikopta ilikuwa na hitilafu na JK akashauriwa a-cancel mikutano miwili huko mkoa wa Dom. Walimwambia si vyema kusafiri bila ambulance.
 
Back
Top Bottom