Kiki za Konde Boy si mchezo

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,053
4,595
Katika pitapita yangu kwenye mitandao nikakutana na kichwa cha habari Hamornize Kujaza Uwanja wa O2 Arena. Nikamsikiliza akiongea na akasema amemalizia malipo.

Kwa kuweka mambo sawa O2 Arena siyo Uwanja bali ni Ukumbi mkubwa una sitting capacity ya watu 20000. Gharama za kuukodi huu ukumbi siyo lelemama. Na uwezo wa kuujaza huu ukumbi sina uhakika kama Msanii kama mdogo kimataifa kama Harmonize ana huo uwezo. Hapo kuna wasanii wenye majina wana perform. Na mara nyingi ticket za mwakani mwezi January zimeshaanza kuuzwa.

UK kodi ni kubwa sana. Chukulia miaka 10 iliyopita Mwanariadha mashuhuri wa mbio fupi za Jamaica Usain Bolt alikataa kushiriki mashindano yote yaliyofanyika UK kwasababu ya Tax Laws zao. Mwaka 2012 wakati wa Olympic serikali ilibidi ifanye exemption ndiyo akakubali kuja kushiriki. Hivyo unless anataka kujifilisi sina hakika kwanini afanye mwenyewe bila kupata wadhamini wa maana.

Siyo lengo langu kumdharau bali ni maoni yangu tu. Aendelee na style za wenzake kina Diamond Twanga pepeta n.k za kupigia vichochoroni Northampton Milton Keynes Reading Leicester hata London kwenye kumbi za uswahilini kama Manzese.

Screenshot_20200221-091839.png
Screenshot_20200221-091822.png
 
Kumbi gani ya uchochoroni diamond amefanya tuanzie hapo kwanza?kabla atujaenda Kwenye hoja yako
Mkuu mimi naongelea mambo ya Ulaya. Sasa wewe niambie ukumbi wa maana ambao Diamond ama Sugu bora Mr Nice mwaka 2005 alipelekwa kwenye ukumbi wa maana Milton Keynes ambako hata kina Neyo waliwahi kupiga hata hivyo hamuwekwa kwenye ukumbi wenyewe bali sebure ya ukumbi.
 
We kila kitu ni kupinga pinga tu, Diamond anapiga uchochorini acha ubishi
Twanga pepeta walienda England wakapiga bar moja inaitwa Element Milton Keynes walipokuja bongo wakadai walikua London. Mr Ebo alipelekwa Frames Milton Keynes hiyo bar ni sawa na Delux Magomeni. Ni uongo tu wa kujisifu. Halafu visa zao siyo za biashara ndiyo maana wanaishiaga uchochoroni na BBC swahili. Usidanganye wstu tunaojua mpaka hizo kumbi.

Hakuna msanii bongo flava aliyepiga katika ukumbi wenye akili UK.
Hamornize nimemuuliza kwenye inbox yake tarehe gani anapiga. Wiki sasa hajaninibu. Angalia website ya 02 Majina ya wasanii wanaopiga hapo pamoja na boxing Legends waliozipiga hapo.

Nb kama kweli Hamo atapiga hapo atakua mwanamuziki wa kwanza Africa Mashariki na kati hata kongo kupiga hapo
 
Kumbi gani ya uchochoroni diamond amefanya tuanzie hapo kwanza?kabla atujaenda Kwenye hoja yako
Element MK, Maharaja alipopiga Matonya. Wewe nieleze ukumbi wa maana unaoujua wewe uliotumiwa na msanii wa kibongo. Ma promoter wao hawana uwezo wa kukodi hizo kumbi. Waulize kina Madjojo na Domokaya walishindwa kuwaweka mpaka hotelini. Wakaishia kuwekwa nyumbani kwa watu na kulipwa £400 show zote. Unadhani Juma Nature mjinga kukataa show za Ulaya?
 
Mkuu mimi naongelea mambo ya Ulaya. Sasa wewe niambie ukumbi wa maana ambao Diamond ama Sugu bora Mr Nice mwaka 2005 alipelekwa kwenye ukumbi wa maana Milton Keynes ambako hata kina Neyo waliwahi kupiga hata hivyo hamuwekwa kwenye ukumbi wenyewe bali sebure ya ukumbi.
Diamond 2019 kapita show Germany ,Venue Columbia Halle,Capacity 3500 tickets sold out.Ukumbi huu watu walio wahi kupiga Tyga 2019,Boyz II men 2012,J Cole 2011.

Screenshot_20200221-142920.png

Screenshot_20200221-145351.png
 
Mkuu mimi naongelea mambo ya Ulaya. Sasa wewe niambie ukumbi wa maana ambao Diamond ama Sugu bora Mr Nice mwaka 2005 alipelekwa kwenye ukumbi wa maana Milton Keynes ambako hata kina Neyo waliwahi kupiga hata hivyo hamuwekwa kwenye ukumbi wenyewe bali sebure ya ukumbi.
hawezi kukutajia bali anaenda ku google. kisha atakuja kusema wewe ni hater
 
joseph1989,
Sijaishi Ujeruman hivyo sijui kama huo ukumbi unafanana na 20000 capacity ya O2? Nimezungumzia UK. Sijamsikia Usain Bolt akikataa kukimbia Germany. Nimezeka kodi ya UK ni kizungumkuti. Sijasikia msanii yeyote akipiga kwenye ukumbi wa maana
 
Tatizo hujui hata ulicho maanisha,Germany sio ulaya.

"Mkuu mimi naongelea mambo ya Ulaya. Sasa wewe niambie ukumbi wa maana ambao Diamond ama Sugu bora Mr Nice mwaka 2005 alipelekwa kwenye ukumbi wa maana Milton Keynes ambako hata kina Neyo waliwahi kupiga hata hivyo hamuwekwa kwenye ukumbi wenyewe bali sebure ya ukumbi."
 
We kweli zuzu yani harmonize akujibu text inbox
[/QUOTE]
Sababu nilimwambia ni muongo nimecheki slot katika website ya O2 hakuna hicho kitu. Siku hizi huwezi kudanganya watu kama zamani za magazeti matatu.

Nisemapo inbox ya hamo nina maana management yake.
 
Tatizo hujui hata ulicho maanisha,Germany sio ulaya.

"Mkuu mimi naongelea mambo ya Ulaya. Sasa wewe niambie ukumbi wa maana ambao Diamond ama Sugu bora Mr Nice mwaka 2005 alipelekwa kwenye ukumbi wa maana Milton Keynes ambako hata kina Neyo waliwahi kupiga hata hivyo hamuwekwa kwenye ukumbi wenyewe bali sebure ya ukumbi."
Soma hapo mpaka ukifika kwa 2face. Diamond kajaza wabongo zaidi ya 1000 kesho yake Mnigeria kajaza full house. Sasa narudi kusema wasanii wetu wanajaza mashabiki kutoka TZ . Imagine kama Diamond ambaye ni King kwasasa Eadt Africa kashindwa kujaza kaukumbi ka 3500 seats huyu Mmakonde huo ubavu wa kujaza 20000 ukumbi maarufu ujulikanao dunia nzima. Huo wa Berlin sijawahi kuusikia maana Ujerumani mpaka leo uliponiambia. Lakini O2 unajulikana duniani kote kwasababu ya events zake.
 
Attachments

  • Screenshot_20200221-120505.png
    Screenshot_20200221-120505.png
    269 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200221-120313.png
    Screenshot_20200221-120313.png
    80.4 KB · Views: 1
  • Screenshot_20200221-120229.png
    Screenshot_20200221-120229.png
    179.5 KB · Views: 1
Mwacheni jeshi apambane huo ndo uanaume akianguka atajifunza kitu na kusonga mbele.
Life is all about hustling hard!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakuunga mkono kwa hilo lakini kwa management yake huyu konde ambaye anadaiwa na Diamond kufanya arrangement za O2. Aanzie kumbi ndogo. Tatizo lake ni moja sifa zitamponza. Ni kijana mzuri sana nampenda kwa jinsi alivyojituma na kufika hapo alipo.
 
Back
Top Bottom