figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 27,607
- 62,370
TAARIFA KWA UMMA
KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CHADEMA
KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CHADEMA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawataarifu wanachama, viongozi na umma kwa ujumla kuwa Kamati Kuu ya Chama itafanya kikao maalum kesho, Jumamosi tarehe 29 Agosti 2026.
Kikao hicho kitafanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Chama, Edwin Mtei House, Mikocheni, Dar es Salaam, na kitaongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, Mhe. John Heche.
Katika Kikao hiki kamati kuu itapokea taarifa ya Sekretarieti kuhusiana na maandalizi ya Baraza kuu na kitaiadili hali na uelekeo wa kisiasa nchini.
Imetolewa leo ljumaa, tarehe 28 Agosti, 2026