Kikao cha CCM, UKAWA chavunjika

Kikao cha CCM, UKAWA chavunjika

Kama muafaka hamna rais vunja bunge la katiba maana halitakuwa na sababu ya kuendelea. Katiba itapatikana baadae ikiwepo taasisi makini ya urais.
 
Ccm wanawabembeleza ukawa kwa vile wametambulishwa kuwa ktb haiwezi patikana bila ukawa kuwepo. Na shida kubwa ni Zanzibar ndo walioshikilia kura ya turufu.
 
Ccm wanaogopa kurudi kwa wtz kuwauliza juu ya muundo wa serikali uweje kwa vile znz watamaliza ubishi wote.
 
Ukawa inatakiwa ikomae na maswala ya kujiandikisha kupiga kura na maswala ya kura sasa hivi..
 
Sheriti moja tu na liko wazi, kujadili rasimu iliyosilishwa na Walioba, iliyobeba maoni yetu wananchi, kinyume na hapo hakuna kurudi bungeni, kweli ccm ni mashetani, wanashindwa kuheshimu roho ya nchi.

Sema rasimu iliyobeba Maoni ya baadhi ya Wananchi na siyo Wananchi wote. Kama wewe ulihojiwa mimi sikupata nafasi hiyo.
 
hii ni kwasababu kikao hicho ni sehemu ya bunge la katiba seif hamadi kayasema hayo source:mwananchi

Sasa naanza kuhisi ukawa hauna tofauti na Boko Haramu, Al Shabab na vingine vingi kama Hamas
 
Sema rasimu iliyobeba Maoni ya baadhi ya Wananchi na siyo Wananchi wote. Kama wewe ulihojiwa mimi sikupata nafasi hiyo.

Mkuu,jitahidi angalau uendane na hadhi yako maana wewe hapa jukwaani ni JF Senior Expert Member Maana Hiyo hoja yako mbona ilishatolewa mjibu na ufafanuzi siku nyingi tena wa Ki-Sayansi?????
 
nakubaliana na wewe ni kweli ccm hawana nia ya dhati ya kutuletea katiba mpya ila kuhusu kurithishana vyeo chadema imevunja rekodi, angalia akina kristina lissu, lucy uweya na wifi yake, joyce nkya, rose kamili, na sasa josephine anakuja kwa kasi.
kwa kifupi chadema-saccos bora waache kabisa kuiongelea hii dhana ya kurithishana vyeo maana ina waacha uchi kabisa.


Ccm hawana dhamira ya kuwapatia wananchi Katiba mpya,tusitumie nguvu kubwa katika kujibisha nao,Bali tufsnye


Ccm hawana dhamira ya kuwapatia wanachi katiba mpya,tupeleke ujumbe mzito kwa wananchi kuwa maisha magumu tunayoishi Ni kwa sababu ya ccm,elimu nbovu Ni kwa ajili ya ccm,huduma mbovu za hospital Ni kwa ajili ya ccm,kurithishana madaraka watoto WA viongozi Ni kwa ajili ya ccm.
 
Naunga mkono maamuzi haya ya UKAWA, mwenye mamlaka ya kukwamua mkwamo huu ni jk na si mtu mwingine yeyote! Jk ndo aliyeunda tume, aliyeweka msimamo wa chama chake wa kuchakachua maoni ya wananchi, kina sitta na wengine ni wafuasi tu wa kushadidia hoja ya jk. Katiba ni sheria mama, ccm iachane na maslahi binafsi ya chama, iheshimu maoni ya wananchi, taifa litadumu daima, lakini chama kinaweza sambaratika wakati wowote! Tunawapongeza wana UKAWA kwa kutanguliza maslai ya nchi kwanza!
 
Kosa kubwa lililofanywa na kikwete ni kuanzisha mchakato wa katiba mpya wakati hakujipanga, afadhali angefanya tu marekebisho kwenye katiba yetu ya sasa! Atakumbukwa kwa kuanzisha mchakato wa katiba mpya na kuuvuruga kwa mikono yake mwenyewe! Katiba sio jambo la chama, bali la watanzania wote wenye vyama na wasio navyo!
 
msiposhiriki bunge la BMK na uchaguzi inapidi vyama vyenu vifutwe
mkuu sema msiposhiriki mkutano mkuu maalumu wa ccm wa uchakachuaji maoni ya wananchi mkuu, pale dodoma hakuna bunge la katiba, bali genge la wachakachuaji maoni ya wananchi!
 
Naunga mkono hoja. Waende kwa wananchi waachie ccm posho wale then watazitapika 2015
 
ukawa komaeni mpaka magamba wajikojolee hovyo hovyo
teh teh, mkuu maccm yamekwama! Ukawa wako upande sahihi wa wananchi, katiba ni kwa ajili ya watanzania wote wenye vyama na wasio navyo, eti ccm wanang'ang'ania serikali 2 kisa ni sera ya chama chao, hivi katiba ni ya chama? Watanzania tuamke toka usingizini mara moja!
 
Sema rasimu iliyobeba Maoni ya baadhi ya Wananchi na siyo Wananchi wote. Kama wewe ulihojiwa mimi sikupata nafasi hiyo.

Hili ni tatizo la kushikiwa akili kama mwenyekiti wako alivyoshikiwa akili na kina Mzee wa tembo na Mzee wa Ntwara aliyekimbilia mafichoni kule Ushoto.
 
Back
Top Bottom