Kijue Kijiji cha Ikola na watu wake

we nae umezidi kama season za kihindi dk 5 unasubiri muendelezo wiki iyayo
 
Itaendelea.....
 
we umemaliza?
 
Tunaendelea,,BALAA LA TANO,,Hapa kileji pamoja kuwa ni sehemu ndogo lakini Kuna sehemu ama kijiwe Cha starehe kinaitwa SHILAWADU aisee eneo Hilo sio powa .hapo vurugu zote kwanzia ulevi madawa ya kulevya ndo sehemu yake. ..Hilo eneo bangi Haina thamani,,sigara zenu za embasi,,sijui spoti na esiemu zinachukuliwa Kama takataka ..hapa ikola sigara maarufu na ya kijanja unaitwa SHIKATAA ,,aisee sio vijana sio wazee sio wakina mama sio wasichana wote wanakwambia sigara ni SHIKATAA,,sigara hiyo inatokea kongo huko mzigo huo ni zaidi ya mundende na vumbi la kongo unaambiwa ni BALAA..,,Hilo eneo la SHILAWADU ni noma usishangae kukutana na shangazi yako toka mkoani huko Arusha ,,songea,ama mwanza anajiuza ,,hapo warembo kutoka mikoa yote utawapata na gesti zote Kijiji kizima wamezikodi wao ..Kuna jamaa alikutana na mama yake mdogo kumbe anajiuza huku kwa wavuvi wakati nyumbani huko singida ameaga amekuja kufunga mzigo wa samaki,,hapo SHILAWADU ndani ya ikola pamoja na watu kupiga vinywaji vikali na vya gharama lakini pombe maarufu unaitwa TEVERE. ,,kunywa madude yako yooote Ila Kama hujanywa tevele watu wanakuona unaigiza ....ITAENDELEA.....
 
Aisee, SHIKATAA
 

Eeh hicho kijiji mbona kama nchi ya kusadikika!
 
DAH MDAU UNANIKUMBUSHA MBALI SANA
NIMIAKA 6 SASA TOKA NIONDOKE IKOLA NIMEKAA IKOLA MIEZI 15 KATIKA HARAKATI ZAMAISHA NAHIZI NDIO KUMBUKUMBU ZANGU:-

-:Wakazi wake niwakarimu sana

-:Mtu namkwewe hawapishani njia moja yn mmoja lazima abadili njia nakama itakua hakuna pakuchepuka yn nilazima wakutane basi kuna kitu wanaita KUSHESHA nihali yakupiga vkofi vdogo vdogo huku unaendelea kubonyea nchini had upige goti nakuna maneno wanaongea kwaunyenyekevu wahali yajuu cjui ndo kabila gan lile

-isco ilikua kila jumamos kuna mdau hapo juu amegusia kuhusu ujio wa braza k sasa akat nipo kule alikuja Pembe eeh huyu mchekeshaji mwene lilungu lake nawatu walijaa balaa

-:samaki migebuka utakula hadi watakukinahi utampika kila aina had kuchoma utachoma lkn watakukinahi tu kuna kupindi samaki wanavuliwa kwawingi sana yn kijiji kizima kinanuka samaki yn kila baada yanyunba mbili unakuta wanakausha samaki

-:kipindi natoka ikola umeme wa tanesco ulikua haujafika cjui kwasasa kama umefika, walikua wanatumia umeme wa sola,genereta nakuna jamaa alikua anafua umeme kwakutuma engene ile ya mashine zadiesel izi zakusagia unga ko alikua anaunganishia watu kwa pesa na alikua anawasha mtambo jioni kuanzia sa12 jion hadi sa4 usiku mtambo unazimwa.

-:Mvua zakule znaambatana naradi sana nazan nikwasababu yakuwa pembezoni mwa ziwa tanganyika.
-:kipindi nafika ikola basi lilikua moja tu kuna mdau amelitaja hapo liliitwa kalavashok ilikua inatoka ikola sa11 alfajir nakufika mpanda sa 4 asubuhi nakutoka tena mpanda sa 7,8 au 9 kurud ikola ila baadae iliongezeka haisi moja hiyo ilikua inapishana na basi yn yenyewe ilikua inalala mpanda nakutoka mpanda asubuhi ya sa2 nakufika ikola sa8 thn sa9 inaanza safar yakugeuka mpanda.

-:kipindi natoka ikola kulikua kumeshajegwa mwalo ila ulikua bado haujaanza kutumika cjajua kwasasa vp.

-:Mtandao ulikua washida sana nasikia sasahiv Halotel ndo mkombozi wao binafs nilikua napenda kwenda kupumzika ziwani kwanza kuna upepo mwanana pia kule ziwani ndo mtandao ulikua unashika vzr sana ndani ya Teckno P5 data ilikua inashika vzr sana ukitaka kudanlod au kuperuz kwakurelax bas weshuka ziwani..

-:Kuna mdau hapo amegusia supu ya dagaa ebhana hii kitu nitamu usipime pia ninzur sana kwetu akina baba mana wale dagaa ni orginal yn wanatoka ziwan wanaingia kwene sufuria bila kuingia kwene frij sasa iyo supu uipate asubuhi kwachapat ebhanaee uipige siku 5 bila hujapata pakupunguzia upwilu lazma uchafue mashuka sema uzur mabint wawatu kule hawana hiyana ila inabid uwe namwenyeji wakukusanua kua huyu nimke wamtu ama vp mana wazee wakule nimabingwa wakuoa vibint vidogo kuna mdau hapo juu amegusia kwahivyo hivyo vbint wake zawatu kuna jamaa alikua amekaa najamaa zake wanapiga story kikazuka kimvua cha kiaina tu ikapiga bonge la radi ikampiga jamaa makalioni..

-:Kuna msimu wa mavuno ya ufuta ebhana kipindi hiko ww nahela yako yambuzi utaonekana fala tu mana kuna wasukuma wanashuka huko namabunda yapesa baa zote wanatamba wao tu
Mtu

-:ligi yao kubwa niligi yang'ombe kuna mdau hapo juu amegusia sasa kuna kichekesho kilitokea kipindi nipo kule mzamini alitokomea kusikojulikana ilileta mtafaruku sana namwaka ule ligi ikasimamishwa wakaweka sheria kua mzamini ukitaka kuanzisha ligi shart ng'ombe aonekane kwanza

-:Kulikua na mgambo anaitwa Kagongo ebhana jamaa alikua anaogopeka huyo yn wanakijiji wanakuambia nibora ukutane na poti lakini sio Kagongo

-:watu waikola wanapenda sana midaharo yakidini baina ya waislam nawakristo cjui kama kwasasa wamebadilika
 
Eeh hicho kijiji mbona kama nchi ya kusadikika!
Hicho kijiji kipo mkuu yn nikijiji ila nazan kunahaja yakukipa hazi ya mji mdogo nisehemu imechangamka balaa mishe mishe zake pale sio zakibush bush nizamjini mjini hadi wadada wauzaji pale wapo kipindi chamavuno yampunga/ufuta au kipindi samak wanakufa sana bas nao wanatoka tabora,kigoma kuja kuuza ikola
 
Da ikola.. Nimepamis sana nakumbuka nilimtembelea rafiki yangu twaha wakati wa mavuno ya ufuta nilikua naenda kuuza mwanza.. Ila starehe za huko nilijikuta nakula mtaji wote na vidosho.. Hali ikawa mbaya hapo ndo nilijifunza kupiga makasia nikapata nauli ya kurudi kwetu.. Ila ipo siku ntarudi tena
 
ulikamata mkweso..pole Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…