KIPWA/CHIPWA: Kijiji ambacho kilikuwa katika dunia ya peke yake. Shukrani kwa Mama Samia.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,213
22,270
KIPWA/CHIPWA: Kijiji ambacho kilikuwa katika dunia ya peke yake. Shukrani kwa Mama Samia.

Tarehe 15/10/2020 ni siku niliyotembelea kijiji cha Kipwa, kilometa 85 kutoka Sumbawanga mjini, mpakani mwa Tanzania na Zambia, ikabidi nijiambie kwamba hiki ni kijiji katika ulimwengu wake. Kwa Watanzania inaandikwa Kipwa lakini kwa Wazambia inaandikwa Chipwa lakini matamshi ni yale yale. Ni kijiji kinachopakana na Ziwa Tanganyika kiasi kwamba naweza kusema wananchi walijenga kwenye hifadhi ya ziwa hilo. Kwenye pande zilizobaki kuna milima mikubwa. Usipopata bodaboda itabidi upande milima mpaka utokee upande wa pili wa kijiji cha Mpombwe ambako utalala hadi kesho yake saa 11 alfajiri utakapopanda basi kwenda Sumbawanga. Ukitazama baadhi ya picha, utaona kwamba nilipiga nikiwa juu ya kilele cha mlima.

Wakati huo hapakuwa na barabara ya kuingia kijijini na mtandao pekee wa simu za mkononi ulikuwa Halotel na Zamtel, Zambia. Ukitaka kusafiri wakati huo, unaweza kutembea kwa miguu, BODABODA au kutumia boti hadi Kasanga ambapo utapata basi la kwenda Sumbawanga. Mahitaji muhimu ya wanakijiji yanapatikana katika mji mdogo wa Mpulungu upande wa Zambia. Na usafiri wa kufika Mpulungu ni boti kwenye Ziwa Tanganyika.

Kwa Kipwa unaweza kutumia Shilingi ya Tanzania au Kwacha ya Zambia. Zote zinakubalika. Watu wa Kipwa ni watu wema na wakarimu sana. Kwa bahati mbaya, mwanzoni mwa 2021, kijiji cha Kipwa kilifunikwa na maji, na kusababisha shida kubwa kwa wakazi wa hapo. Maji hayo yaliharibu nyumba za watu na mali zao, pia kulikuwa na matukio ya mamba kujeruhi watu. Kulikuwa na mwanamke fulani ambaye alikatwa mkono na mamba.

Naishukuru sana serikali ya Tanzania kwa kuwahamisha wanavijiji katika maeneo ya juu na kujenga upya shule na hospitali. Ujenzi unaendelea. Pia kuna barabara ambayo tayari imejengwa kutoka kijiji cha Mpombwe hadi Kipwa. Kwa kweli, serikali ya Mama Samia inafanya kazi yake bora.

Kwa wale wanaopanga kutembelea Kalambo Falls wanaweza kupita Kipwa na kujionea kazi iliyofanyika. Kwa sasa, Kipwa haiko tena katika ulimwengu wake... inafikika na ina huduma zote muhimu chini ya serikali ya sasa ya awamu ya sita chini ya Rais Mama Samia Suluhu.
 

Attachments

  • P9264237.jpg
    P9264237.jpg
    33.8 KB · Views: 12
  • 20201014_161914.jpg
    20201014_161914.jpg
    406.7 KB · Views: 11
  • 20201015_123210.jpg
    20201015_123210.jpg
    358.9 KB · Views: 12
  • 20201015_123746.jpg
    20201015_123746.jpg
    422.3 KB · Views: 7
  • 20201015_133928.jpg
    20201015_133928.jpg
    364.8 KB · Views: 9
  • 20201015_140848_1.jpg
    20201015_140848_1.jpg
    459.6 KB · Views: 8
  • 20201015_133923.jpg
    20201015_133923.jpg
    551.4 KB · Views: 8
  • IMG_0278.jpg
    IMG_0278.jpg
    164.4 KB · Views: 8
  • IMG_0214.jpg
    IMG_0214.jpg
    183.3 KB · Views: 9
  • sddefault.jpg
    sddefault.jpg
    30.1 KB · Views: 8
  • IMG-20220812-WA0008.jpg
    IMG-20220812-WA0008.jpg
    64 KB · Views: 9
  • IMG-20220812-WA0010.jpg
    IMG-20220812-WA0010.jpg
    36.4 KB · Views: 9
  • IMG-20220812-WA0009.jpg
    IMG-20220812-WA0009.jpg
    43.6 KB · Views: 8
Nchi kubwa hii
Hivi kwenye hizi kona zetu za mipaka na sehemu nyengine za misitu mikubwa na milima ambapo bado makazi hayajapita hivi wanadhibiti uvamizi na uhamiaji haramu kwa wageni wa nchi nyingine tunazopakana nazo ? Na kama wanadhibiti wanazibiti vipi ? Ni sehemu zote wanazibiti?
 
Tunamshukuru sana Mama Samia kwa kuwasaidia wananchi wa Rufiji kama alivyofanya kwa wanakijiji wa Kipwa.
 
Back
Top Bottom