Kijiwe cha vijana late 20s ( is our future bright? )

Kijiwe cha vijana late 20s ( is our future bright? )

shaurimbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
1,915
Reaction score
2,339
habari za wekend wadau?

vijana wenzangu late 20s na early 30s.. mnaojitegemea kimaisha, mlio ajiriwa na mliojiajiri karubuni tupige story na ku share experience tofauti..

kwa hali ya maisha inavyoenda kwa kila mmoja wetu.. je future yetu ipo bright kweli..


binafsi nipo 28, nimeajiriwa somewhere.. nina mke na mtoto mmoja.. ( bado sijahalalisha kanisani)...

nawaza sana nikifikiria future yangu na familia yangu kwa ujumla.. mshahara kiduchu, ajira ngumu, kujiajiri changamoto kibao..

kuna muda nawaza niache kazi nikajaribu maisha ughaibuni.. napo kunatisha hakueleweki siku hizi..


gharama za maisha zinazidi kupanda kila kukicha..

waajiri wengi wa kibongo wanalipa hand to mouth salaries..

ni vizuri tubadilishane mawazo kwa ujumla kila mtu alivyojipanga kuhakikisha bright future inakuwepo..


kama vyeti nina imani wengi wetu tunavyo, nia tunayo na uthubutu pia tunao..

karibuni wadau
 
Asikudanganye mtu hata siku moja kuwa kuna mjadala utakaokubadili mawazo na kukukwamua.

Kutakachokukwamua ni hasira ulizo nazo, maarifa na juhudi.

Usipoteze muda kwenye mijadala, identify opportunities and make use of them. Kama wapo waliofanikiwa hakuna uhalali wa wewe kushindwa. Watu wanatoka China kuja kuuza karanga na mahindi ya kuchoma Tanzania kudhihirisha kuwa mtanzania fursa anazo ila hazitumii ipasavyo.

Kazi kwako...
 
huku twaongelea mapenzi tu. hayo mambo ya kazi peleka jukwaa la kazi sawa sawa ? (kwa lafudhi ya kipemba)
 
Deal kushika bunduki tu kumi nje kumi ndani
 
Mapenzi yameisha siku izi?????? mmu ni mapenzi mahaba urafiki..... haya ya maisha na kazi peleka kwa wana uchumi huko
 
maisha magipumu sio siri acha tu.....NIKIKUTABA NA MARIOO NATAMANI NIMCHAPE RISASI YA USO
 
Idea nzuri ,tatizo timing...na hizi likizo humu watajaa teenagers kukuharibia uzi,..mimi nasubiri likizo iishe nitarudi tena kuchangai mambo serious
 
shule sikusoma ila sio kwa kudhamiria/
kuja kushtuka ndio kichwa cha familia/

Jitihada kubwa mafanikio hakuna/
sikukuu ikifika watoto wa kike wanataka skuna/

hii ni nyimbo kaimba wa kuitwa nikki mbishi
 
maisha magumu ndio maana nakasirishwa sana na mafisadi maana mie hadi leo moja haikai, mbili haikai, tatu inazima yaani daaahhh.
Nimeamua kurudi shule, niongeze elimu labda hali itabadilika kidogo.
Ila yote ni katika kuongeza silaha katika kupambana na maisha.
 
Daaah maisha magumu aisee ajira ngumu kujiajiri mtihani....yan ni shidaa
 
Back
Top Bottom