Tafadhalini wanaume piteni hapa

Tafadhalini wanaume piteni hapa

TAI DUME

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
11,173
Reaction score
30,655
Wazee wenzangu wa kiumeni leo tutete yetu. Ujue kuna wakati unafika inabidi uchukue japo time kidogo kujithaminisha jinsi unavoishi ukilinganisha na umri. Me huwa nakereka sana sana mwanaume wa late 30s au early 40s anaishi kiajabu ajabu tu kama janki wa early 20s.

Yaani jitu zima linakaa kubishana au kujisifia idadi ya mademu aliowapitia over the wkend utazani ndio yupo kwenye balehe ya kwanza, Au unakuta janaume kubwa hilo lakini linashindana kukesha baa mpka kulala nje utafikiri fagio la chelewa. Bora hata mafagio ya chooni yana heshimika kuliko mwaume unaekesha baa tena kwa ushindani wa kijinga wa kuonyesha washkaji picha za mabaamedi uliotembea nao.

Sina ugomvi na pombe lakini kwa nini uendekeze mpaka unafkia hatua ya kuweka bondi ofer ya kiwanja! Mwanaume simamia mipango yako kikamilifu ukiamka asubui una hang over ya mafanikio sio ya mipombe ebo? Ujue hakuna ugonjwa mbaya mbaya kama wa kuregretia bata za ujanani ukubwani sio?

Yaani umeshakongoloka ndio unaanza kujipanga eti utengeneze maisha wakati huna nguvu, yah lazima magonjwa nyemelezi yote yakuandame. Hizi bata za kipuuzi kutaka sifa kwa watoto wa kike hazina mpango kwanza watoto wa kike wenyewe siku ukiona wanakushobokea ujue washakuona Lofa tu ----- mtozeni.

TENA HAPA NGOJA NIWA PESTIE ILE CONCEPT YA LIFE BEGIN AT 40s

Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international skul nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living.

Hapo ndo unawaza kufuga ng'ombe wa maziwa kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu 12 kwa 15! Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha bness in Australia.

Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 300M! Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 5M kimyakimya.

Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watakujua! Halafu unashangaa wanazidi kuinuliwa. Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... (Malizia) Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET.

Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime.

Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You?

NI HAYO TU KWA SASA, kwa ushauri zaidi inbox
 
Kwa hiyo sisi wenye 25-30 tunaruhusiwa Kula bata!
 
mipasho au ushauri???

Nenda taarabu ukatunge wimbo!!! ukimaliza uje ushauri!!!!
 
15- 25 fanya hili hapa
1381858_502878706516263_2742203064345397451_n.jpg
25 - 30
oa ...olewa

30 -40
wekeza

40 plus saidia
 
mipasho au ushauri???

Nenda taarabu ukatunge wimbo!!! ukimaliza uje ushauri!!!!

Tusi haliwi tusi mpka mtusishaji atakapoamua kukutusisha na mtuswaji akatusika. Kama utaona mipasho au ushauri ni mtazamo tu
 
Mmh wengine tumeanza kuwekeza tangu kabla hatujafikisha miaka 25..nafikiri uwekezaji inabidi ufanyike mapema sana na inasaidia kuweka msingi mzuri wa kujiimarisha kiuchumi.

Hilo ndilo la msingi pia usijifanye mtu wa bata kisa tu umri wako bado mdogo maana unaweza ukawa umepitiwa na mzunguuko wa fedha kwa muda alafu ukikata utajuta, uzi wa jamaa umetulia ila sometimes tusiishi sana kwa formula kwa kuwa kuna changamoto nyingi zinawakuta watu katika umri wa chini
 
Back
Top Bottom