Kijiji hatari cha Wachawi Tanzania

Kijiji hatari cha Wachawi Tanzania

Kipo km 75 kutoka kahama mjini, kinaitwa ilogi, maana ya neno ilogi ni mchawi, ni neno la kabila la kisukuma, chanzo cha kuitwa jina hilo ni kwamba, takribani miaka 60 iliyopita, kijiji hicho kilikuwa ni makazi ya Wachawi tu,hali hiyo hadi leo inaendelea.

Kila baada ya miezi miwili ama mitatu ilogi lazima azikwe mtu na hasa watoto wadogo na wachanga, ni kijiji kidogo tu ila misiba haikatiki, Nilibahatika kutembelea kijiji hicho na kujionea mambo ya kutisha Sana.

Nilishuhudia msiba wa mtoto mwenyewe umri wa miaka 9 ambaye alifariki ktk mazingira ya utata Sana pasi na kuugua ugonjwa wowote na baadae maiti yake ikawa inaamka na kukohoa, walisubiri wakidhani maiti ingepata uhai lakini ndo kwanza vituko vikazidi baada ya maiti ile kuanza kubadilika hadi sura.

Baada ya kusubiria Kwa Siku tatu Hatimae waliamua kuzika . Nyumba niliyokuwa nimefikia ilikuwa na choo cha shimo ambamo ndani yake Choo kile shimoni alikuwa akiishi ndege mweusi na mwingine aina ya katyente.

Ndege wale walikuwa wakitoka usiku tu, cha ajabu hata ukifunga tundu la Choo kesho yake ukifungua ni lazima ndege wale watoke na sijui ni muda gani walikuwa wanaingia.

Kuna sehemu moja ktk maeneo ya nyumba za wafanyakazi wa mgodi ilikuwa si rahisi kukatiza, ukipita maeneo hayo ni lazima usikie vishindo vya mtu akikufuata nyuma hasa nyakati za usiku.

Ninapoandika hapa bado ilogi ni sehemu hatari Sana.


Mandhali ya kijiji cha ilogi

= Mandhari
 
kwenye picha naona kuku ana mguu mmoja - haha mambo ya ilogi hayo😀
 
Ilogi naifahamu sana hayo uliyoyasema labda ilikuwa zamani.Mimi nimekuwa namtembelea jamaa yangu yupo Ilogi anafanya kazi mgodini sikusikia hiyo kitu.Gamboshi ndiyo inakimbiza kwa haya mambo.
 
mkuu zamani ilipokuwa mji wa wachawi tu nini kikatokea mpaka sasa siyo kijiji cha wachawi pekee?

Au ile mada ya mshana Jr ihusike hapa kuwa wakianza kujaribiana atakayeshindwa kama hajafa huokoka?
 
Kuna sehemu Tz hii nilisikia kusafiri na Begi mchana ni marufuku wakikuona tu imekula kwako!
 
Nakumbuka sana maswahibu ya Ilogi, nilienda kumsalimu brother aliyekuwa anafanya kazi Bulya na kufikia quarter zao za Ilogi; kwa kweli niliyeseka sana kwani siku moja usiku nilipotoka nje kujisaidia nilikutana na Mtu wa ajabu akiwa anawaka kama moto kwa mstuko nilipiga kelele na kuzirai baada ya lisaa nilipopata fahamu nikaeleza walionizunguka wakasema kama umekuja huna hata Chale mwilini hapa huwezi ishi, nilikimbia ILOGI mpk Leo ninapaheshimu kwa ULOGI

Hapo ndiyo mimi napataka halogwi mtu wala hatishwi mtu kama kuna pesa niambieni nikajichukulie mwanaume gani unatishwa na mazingaombwe?
 
Nakumbuka sana maswahibu ya Ilogi, nilienda kumsalimu brother aliyekuwa anafanya kazi Bulya na kufikia quarter zao za Ilogi; kwa kweli niliyeseka sana kwani siku moja usiku nilipotoka nje kujisaidia nilikutana na Mtu wa ajabu akiwa anawaka kama moto kwa mstuko nilipiga kelele na kuzirai baada ya lisaa nilipopata fahamu nikaeleza walionizunguka wakasema kama umekuja huna hata Chale mwilini hapa huwezi ishi, nilikimbia ILOGI mpk Leo ninapaheshimu kwa ULOGI

Ulitakiwa umuone kwanza mshana jnr au ufanye maombi kabla ya kwenda gaza strip hata hivyo wewe ni mchovu sana unatishwa kidogo tu chali yaani umenichekesha saaana.
 
Back
Top Bottom