Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,697
Kipo km 75 kutoka kahama mjini, kinaitwa ilogi, maana ya neno ilogi ni mchawi, ni neno la kabila la kisukuma, chanzo cha kuitwa jina hilo ni kwamba, takribani miaka 60 iliyopita, kijiji hicho kilikuwa ni makazi ya Wachawi tu,hali hiyo hadi leo inaendelea.
Kila baada ya miezi miwili ama mitatu ilogi lazima azikwe mtu na hasa watoto wadogo na wachanga, ni kijiji kidogo tu ila misiba haikatiki, Nilibahatika kutembelea kijiji hicho na kujionea mambo ya kutisha Sana.
Nilishuhudia msiba wa mtoto mwenyewe umri wa miaka 9 ambaye alifariki ktk mazingira ya utata Sana pasi na kuugua ugonjwa wowote na baadae maiti yake ikawa inaamka na kukohoa, walisubiri wakidhani maiti ingepata uhai lakini ndo kwanza vituko vikazidi baada ya maiti ile kuanza kubadilika hadi sura.
Baada ya kusubiria Kwa Siku tatu Hatimae waliamua kuzika . Nyumba niliyokuwa nimefikia ilikuwa na choo cha shimo ambamo ndani yake Choo kile shimoni alikuwa akiishi ndege mweusi na mwingine aina ya katyente.
Ndege wale walikuwa wakitoka usiku tu, cha ajabu hata ukifunga tundu la Choo kesho yake ukifungua ni lazima ndege wale watoke na sijui ni muda gani walikuwa wanaingia.
Kuna sehemu moja ktk maeneo ya nyumba za wafanyakazi wa mgodi ilikuwa si rahisi kukatiza, ukipita maeneo hayo ni lazima usikie vishindo vya mtu akikufuata nyuma hasa nyakati za usiku.
Ninapoandika hapa bado ilogi ni sehemu hatari Sana.
Mandhali ya kijiji cha ilogi