Utalii ndani ya maporomoko ya maji Kinukamori Marangu, Moshi-Kilimanjaro

Funa the Great

Senior Member
Aug 1, 2022
160
271
KINUKAMORI MARANGU, MOSHI KILIMANJARO

Unapozungumzia maeneo yenye mandhari mazuri kwa ajili ya utalii ndani ya mkoa wa Kilimanjaro basi wilaya ya Moshi imebarikiwa sana. Maporomoko ya maji yaliyopo ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Moshi eneo la Marangu.

Ndani ya eneo ilo kuna sanamu nyingi zinazoelezea historia mbalimbali juu ya viongozi wa kichaga waliokuwa wakitawala kwenye maeneo mbalimbali na mfumo mzima wa maisha yao hadi umauti ulivyowapata.

Hakika kuna simulizi nyingi zenye kusisimua utakazozipata kutoka kwa wabobezi wenye historia nyingi juu ya kabila la wachaga. Hautoishia hapo tu bali kuna mandhari mazuri yaliyotunzwa na kupangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu zaidi yatakayokufanya ufurahi na kutojutia kufika ndani ya eneo hilo.

Nilichokipenda zaidi juu ya eneo ilo ni kwamba limetengenezwa kwa mfumo wa kisasa zaidi kwa kuwekewa ngazi maalumu zitakazokusaidia kushuka na kupanda utakapokuwa unatemebelea eneo la maporomoko ya maji. Zao la kahawa ni miongoni mwa mazao yaliopo ndani ya eneo ilo. Hususani kahawa aina ya ARABIC.

Kwa huduma za safari za kutembelea vivutio vya utalii wasilana nami +255622174613.

Safari za marafiki, familia, kiofisi, shule/vyuo, wapenzi (couple) n.k
IMG_20231011_202408.jpg
IMG_20231011_202308.jpg
IMG_20231011_154011.jpg
IMG_20231027_182816_272.jpg
 
Back
Top Bottom