Mzee Mwanakijiji,
Kwanza napenda nikupe hongera kwa kuja na wazo kama hili. Sikuzote nimekuwa nikisema inatupasa tuangalia ni namna gani ya kuwafikia watu wengine ambao wako nje ya Mtandao wa JF na hata wale ambao hawana access ya internet. Kwa Tanzania ni wengi sana. Njia za kuwafikia Watanzania hawa ni pamoja na:
- Mtandao
- Magazeti na Vijarida
- Radio
- TV
- Networking
Tumekuwa very effective so far katika Mtandao, lakini sasa umeonyesha njia kwa kuja na Kijarida cha "CHECHE ZA FIKRA". Safari na iendelee.
Jina la Kijarida ni zuri sana na hata mwonekano na mpangilio wa Kijarida ni mzuri. Images ziko so clear na maandishi yanasomeka bila taabu. Zaidi ya yote nimeona hoja nyingi ni hoja nzito sana.
Nina maoni machache ya kuboresha:
- Wakati wa Ku-Insert images ni vema ziwekwe vizuri. Katika baadhi ya sehemu flow ya maandishi si nzuri sana. km page ya mbele sehemu nyingine maandishi yanakatikia pabaya na mtu asipokuwa makini anapoteza flow.
- Pia nashauri kuwe na habari mbalimbali nyingine mbali na za kisiasa ambazo ndiyo zimesheheni, km habari za uwezeshaji kwa ujumla (unajua Watanzania wengi ni Masikini), habari za akina mama n.k.
- Katika kipindi kama hiki cha bunge, unaweza ukatuletea hoja ambazo ni nzito na zilizogusa wengi toka bungeni.
- La mwisho, kwa kuwa kiko katika PDF format, unaweza pia ukaki-upload hapa JF. Ni kweli mara kadhaa hata mimi nilishindwa kuki-download kwa ajili ya Pop-ups kama Mzalendo Mtanzania alivyosema.
Nakutakia kila la heri. I hope Cheche za Fikra zitasaidia kuchochea mabadiliko katika Jamii.