Kijarida cha "Cheche za Fikra" chatoka!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,395
39,531
Tafadhali jipatie nakala yako ya bure ya kijarida chetu hiki ambacho kinaanza kukoleza moto wa mabadiliko. Tunawashukuru wasambazaji waliojitokeza kuanzia Dar penyewe, Kagera, Mara, Mwanza na Mbeya. Tunasubiri maeneo mengine watakaotaka kujitolea kusambaza (watapata nakala mapema Jumatatu) ili waweze kuchapa na kugawa nakala za kijarida hicho bure.

KUbwa ni kuwa ukimaliza kukisoma usibakie nacho mkononi, mpatie mtu mwingine!!!

Ingia kwenye "Current News"

kijaridachacheche.jpg
 
Last edited by a moderator:
Tafadhali jipatie nakala yako ya bure ya kijarida chetu hiki ambacho kinaanza kukoleza moto wa mabadiliko. Tunawashukuru wasambazaji waliojitokeza kuanzia Dar penyewe, Kagera, Mara, Mwanza na Mbeya. Tunasubiri maeneo mengine watakaotaka kujitolea kusambaza (watapata nakala mapema Jumatatu) ili waweze kuchapa na kugawa nakala za kijarida hicho bure.

KUbwa ni kuwa ukimaliza kukisoma usibakie nacho mkononi, mpatie mtu mwingine!!!

Ingia kwenye "Current News"

Ningependa kujipatia kamoja tuu!Nothern Zone hujapata msambazaji?
 
Mkuu,
Mbona hauko wazi ni wapi haswa tutakipata hicho kijarida? Je wanapouza magazeti mengine au wapi, sema baba.
 
Heshima Mbele Mkuu wangu! Kazi nzuri na mwanzo mzuri sana nkuu wangu keep it up for betterment of Tanzania and its people.
 
Mkuu hongera sana nimeona mambo yako kwenye kijarida.Actually I managed to print a few copies nikawagia wafanyakazi wenzangu hapa ofisini na hata kutumia some of my friends as an attachment nao wa[ate kuyaona mambo ya JF.
Am impressed with your good work.
 
Poa sana naiprint sa hivi naenda kusambaza nyumbani na mtaani, btw huyo mhariri kwenye picha ndo mwanakijiji?
 
Hicho kijarida mbona kinakuja na pop-ups za kumwaga tu? Au ni mimi na tarakilishi changu tu?
 
Mzee Mwanakijiji,

Hongera kwa juhudi kubwa. Ila naona kuna pop-ups kibao kwenye website yako kuanzia wiki hii. Angalia na rekebisha vinginevyo watu wengine wanaweza kuogopa na kukimbia
wakidhani wanashambuliwa.
 
Mwanakijiji,

Mpangilio Mzuri,ila layout ya makala haijaka vizuri..weka mpandilio mzuri ambao ina mtiririko.

Naweza kuandika Makala katika kijarida hicho??nitaaandika Bure tu
 
Mzee Mwanakijiji et al

Hongera sana...this is walk the talk...well done.

Maoni: Ningekuomba kiwe kinatumwa pia kwenye e-mail kama newsletter badala ya attachment.

Binafsi natengeneza mailing list kwenye e-mail address yangu special kwa ajili ya kutuma kijarida hiki kila wiki kinapotoka.

Kazi nzuri indeed.
 
wazee hata mimi nimenotice tangu jana napata pop ups za ajabu; tutaliangalia sijui nini...
 
Kijarida.........kwa nini ki-Jarida....mbona mnashusha chat yake....went through it with some dudes here.........job well done MKJJ.
 
Mzee Mwanakijiji,

Kwanza napenda nikupe hongera kwa kuja na wazo kama hili. Sikuzote nimekuwa nikisema inatupasa tuangalia ni namna gani ya kuwafikia watu wengine ambao wako nje ya Mtandao wa JF na hata wale ambao hawana access ya internet. Kwa Tanzania ni wengi sana. Njia za kuwafikia Watanzania hawa ni pamoja na:
 • Mtandao
 • Magazeti na Vijarida
 • Radio
 • TV
 • Networking

Tumekuwa very effective so far katika Mtandao, lakini sasa umeonyesha njia kwa kuja na Kijarida cha "CHECHE ZA FIKRA". Safari na iendelee.

Jina la Kijarida ni zuri sana na hata mwonekano na mpangilio wa Kijarida ni mzuri. Images ziko so clear na maandishi yanasomeka bila taabu. Zaidi ya yote nimeona hoja nyingi ni hoja nzito sana.

Nina maoni machache ya kuboresha:

 • Wakati wa Ku-Insert images ni vema ziwekwe vizuri. Katika baadhi ya sehemu flow ya maandishi si nzuri sana. km page ya mbele sehemu nyingine maandishi yanakatikia pabaya na mtu asipokuwa makini anapoteza flow.
 • Pia nashauri kuwe na habari mbalimbali nyingine mbali na za kisiasa ambazo ndiyo zimesheheni, km habari za uwezeshaji kwa ujumla (unajua Watanzania wengi ni Masikini), habari za akina mama n.k.
 • Katika kipindi kama hiki cha bunge, unaweza ukatuletea hoja ambazo ni nzito na zilizogusa wengi toka bungeni.
 • La mwisho, kwa kuwa kiko katika PDF format, unaweza pia ukaki-upload hapa JF. Ni kweli mara kadhaa hata mimi nilishindwa kuki-download kwa ajili ya Pop-ups kama Mzalendo Mtanzania alivyosema.

Nakutakia kila la heri. I hope Cheche za Fikra zitasaidia kuchochea mabadiliko katika Jamii.
 
Sanctus.. kitu ambacho nataka kiwe tofauti kabisa na natumaini tutaweza ni kuwa:

Kijarida nataka kiweze kuwa localized. Tukipata habari za kazi au matukio muhimu ya eneo la Morogoroo kwa mfano au Kanda ya Ziwa n.k. basi pamoja na habari muhimu na makala kulingana habari za mahali zinaendena na wapi watu wanasoma kijarida hicho.

Hivyo kama hilo unalolisema la mambo ya uwezeshaji au nafasi za kazi n.k au matangazo fulani specific kwa watu wa Dar, basi toleo la Dar litakuwa na habari za Dar zaidi na watu wa mwanza wataweza kujua matukio ya maeneo yao.

Na zaidi ya yote nataka tuweze kufikia mahali kuwa kama mtu anasambaza kijarida hiki bure Kipunguni au Magomeni, basi habari za mambo ya maeneo hayo zinaweza kuingizwa na hivyo kinakuwa pia ni community newsletter. Magazeti makubwa hayawezi kufanya hivyo.

Ushauri wako huo mwingine tumeupokea vizuri na tutajitahidi kufanyia kazi na tunakaribisha makala hoja, mawazo au maoni kuhusu jambo lolote la kijamii kutoka kwako binafsi au kama kiongozi wa TPN...

shukrani za dhati.
 
Mwanakijiji,

Mpangilio Mzuri,ila layout ya makala haijaka vizuri..weka mpandilio mzuri ambao ina mtiririko.

Naweza kuandika Makala katika kijarida hicho??nitaaandika Bure tu

hahahah mzee hata kama ungetaka malipo sina ingebidi uandike bure tu. Yes nakaribsha makala fupi fupi na tunaandika kwa majina yetu aidha yote kamili au hata la kwanza tu. Makala yoyote itufikie kabla ya mwisho wa Ijumaa.

Asante kwa ushauri.
 
Hongera mkuu nimeona mambo yako.Cosider tu maneno ya wadau ili kukiboresha.cc wengine tutakuwa tuasambaza kupitia mail list zetu.Binafsi nina mail list kama ya watu 160 hivi hivyo ukinifowadia basi be sure 160 people will read it.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom