Kijana wa miaka 18 ajinyonga baada ya kuugua Ukimwi

Kijana wa miaka 18 ajinyonga baada ya kuugua Ukimwi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Kijana aliyetambulika kwa jina la Abdallah Salumu wa miaka 18, mkazi wa Charambe Mianzini, Wilaya ya Temeke alikutwa akining'inia chumbani kwake, akiwa amejifunga kamba aina ya katani aliyoitundika kwenye kenchi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke Engbert Kondo, alisemsa kijana Abdallah Salumu alikutwa amekufa juzi kwa kujinyonga, huku akiacha ujumbe kuwa "UGONJWA HUU WA UKIMWI UMENISUMBUA SANA".
Source By Mwananchi.
 
Hivi latest ARV zina msaadia mwenye vvu kudunda mpaka miaka mingapi?
 
Hivi latest ARV zina msaadia mwenye vvu kudunda mpaka miaka mingapi?

Madabida na ccm wameshazichakachua, tunalishwa vidonge vilivyotengenezwa na unga wa sembe, kwa hiyo hizo dawa hazisaidii tena...
 
Amejinyanyapaa maskini. Hawa ndo wale wenye tabia ya kucheka wenye ukimwi, ukimpata anaona kiama kimemfika. Miaka 18 ya umri mbona angedunda sana kwa kujitunza? Angeoa na kupata watoto kabisa!
Pole kwa wazazi na wafiwa wote na kigelofrendi.
 
Madabida na ccm wameshazichakachua, tunalishwa vidonge vilivyotengenezwa na unga wa sembe, kwa hiyo hizo dawa hazisaidii tena...
Achilia mbali hizi na nyinyiem, nipe taarifa ya zile genuine aka original.
 
Achilia mbali hizi na nyinyiem, nipe taarifa ya zile genuine aka original.

Arv zikitumika na kufuata masharti yote kama kutokunywa pombe, kula vizuri balanced diet, kuepuka ngono zembe na kupumzika vya kutosha, zinaweza kuvuta hadi miaka 30 bila matatizo. Na kuangalia afya mara kwa mara ili kutibu magonjwa nyemelezi. Actually hiv haina ubaya kama ule wa hypertension (tunaitaga bp), manake haikuui ghafla. Hata kisukari ni hatari zaidi kuliko hiv, kujinyanyapaa tu ndo issue.
 
Amejinyanyapaa maskini. Hawa ndo wale wenye tabia ya kucheka wenye ukimwi, ukimpata anaona kiama kimemfika.

Umejuaje kuwa amejinyanyapaa na hajanyanyapaliwa?

Umejuaje kuwa alikuwa na kawaida ya kucheka wenye UKIMWI?

Wewe ndo unamnyanyapaa marehemu
 
Umejuaje kuwa amejinyanyapaa na hajanyanyapaliwa?

Umejuaje kuwa alikuwa na kawaida ya kucheka wenye UKIMWI?

Wewe ndo unamnyanyapaa marehemu

Hahaha, typical you. Ni mambo mangapi wewe umenyanyapaliwa na haujajiua? Angeuwawa hapo kweli, lakini kajiua mwenyewe. Well, uzuri hata ukimnyanyapaa marehemu haoni wala hana feelings, ama unaonaje mwalimu? Angalia usianze kuninyanyapaa.

But on a serious note, mara nyingi tuna hulka ya kujinyanyapaa kabla hatujanyanyapaliwa. Hata kugoma kupima hiv ni dalili ya kujinyanyapaa. Cousin wangu anaishi na hiv for kama 15 years nnazozijua mie. Aliushinda unyanyapaa kwa kuongelea waziwazi kabisa. Na hata kwenye ubaguzi wa msosi she would explain kwa nini diet yake ni tofauti na kuelezea umuhimu wa kupima. Hata wanyanyapaa hawakuwa na nafasi manake kabla hujamhudumia incase anaumwa anakuambia vaa gloves mdogo wangu. Hapo utamnyanyapaaje sasa?
 
Arv zikitumika na kufuata masharti yote kama kutokunywa pombe, kula vizuri balanced diet, kuepuka ngono zembe na kupumzika vya kutosha, zinaweza kuvuta hadi miaka 30 bila matatizo. Na kuangalia afya mara kwa mara ili kutibu magonjwa nyemelezi. Actually hiv haina ubaya kama ule wa hypertension (tunaitaga bp), manake haikuui ghafla. Hata kisukari ni hatari zaidi kuliko hiv, kujinyanyapaa tu ndo issue.
Hapo kwenye blue ndo mpango mzima, kuacha kukata kiu ya hiyo kitu si mchezo. Huyu dogo angetulia na miaka yake 18 + 30 ya arv angefikisha 48 ambapo si haba. Huyu atakuwa alikuwa anaumwa hofu ambao ni zaidi ya hiv yenyewe..!
 
Hahaha, typical you. Ni mambo mangapi wewe umenyanyapaliwa na haujajiua? Angeuwawa hapo kweli, lakini kajiua mwenyewe. Well, uzuri hata ukimnyanyapaa marehemu haoni wala hana feelings, ama unaonaje mwalimu? Angalia usianze kuninyanyapaa.

But on a serious note, mara nyingi tuna hulka ya kujinyanyapaa kabla hatujanyanyapaliwa. Hata kugoma kupima hiv ni dalili ya kujinyanyapaa. Cousin wangu anaishi na hiv for kama 15 years nnazozijua mie. Aliushinda unyanyapaa kwa kuongelea waziwazi kabisa. Na hata kwenye ubaguzi wa msosi she would explain kwa nini diet yake ni tofauti na kuelezea umuhimu wa kupima. Hata wanyanyapaa hawakuwa na nafasi manake kabla hujamhudumia incase anaumwa anakuambia vaa gloves mdogo wangu. Hapo utamnyanyapaaje sasa?

Hadi muda huu Mimi sijawahi kunyanyapaliwa kwa jambo hata moja achilia "mangapi". Hilo moja.

Pili, Waswahili wanamsemo wao "mzigo wa mwenzio kanda la usufi". Kwa vile wewe hupo katika position yake ni rahisi sana kusema "ahhhh kanyanyapaliwa kidogo tu ndo ajiue" wakati hujui ana matatizo gani ya kisaikolojia na mengineyo

Tatu, nilichozungumza Mimi ni wewe ku-jump kwenye hitimisho wakati hujui chochote. Hujui kama hajanyanyapaliwa kwa hiyo hukuwa na haki ya kusema kuwa hajanyanyapaliwa au usemavyo sasa kuwa hata kama kanyanyapaliwa ni kidogo. Hujui
 
RIP
lakini kwa wale potential suicidials ...., kujiua sometimes ni kuwa selfish kwa kuwaachia majonzi wanaokupenda na kuwapa shida na matatizo ya kukugharamikia, unless hakuna anayekumiss na hapo basi angalau kwenye barua yako ya kujiua acha na pesa za gharama ya mazishi yako na usumbufu sio kuwaachia mzigo wengine (sooo inconsiderate)
 
Back
Top Bottom