Kijana wa kisasa anatakiwa kuwa na vitu gani hasa!?

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
800
1,050
Ni kipi ambacho Kama kijana wa Sasa hutakiwi kuwa haunacho!?

Ni vitu gani ambavyo vinafanya uonekane au usionekane kuwa kijana wa kisasa!?

Na Ipi ni misingi ya kua kijana wa kisasa!?

Nilishawahi kusikia "Kijana wa kisasa hutakiwi kukosa suti kali ambayo utaitumia sana kuingia katika maeneo rasmi/ -a kiofisi"

"Kijana kutokosa vitu Kama vision,biashara au elimu"

Binafsi naona vijana wengi wanatumia (Marijuana) au Vilevi na wale wasiotumia ndo huonekana wa kizamani,pia wengi kumiliki simu janja bila kutazama uhitaji na hali zao kiuchumi....Masuala ya dhambi za fashion n.k

Najua tunatofautiana sana kimawazo....ndiyo maana nikaamuua kuuleta huku huu mjadala ili vijana tukae katika mstari mnyoofu kama vijana wa kizazi cha kileo...

JE KIJANA ILI UWE WA KISASA UNATAKIWA UWE NA KITU GANI HASA?
 
1.I phone
2. Biashara nzuri. Udalali wa magari au duka la nguo au simu.
3. Nyumba nzuri yakupanga
4. Ka gari kazuri. (Inategemea)
5. Pesa mkononi na kwenye mtandao wa simu. Mpesa, Tigo pesa nk. Bank hakuna ulazima sana
6. Hakosi vi hela vya bia za promosheni.
7. Pisi kali.
 
1.I phone
2. Biashara nzuri. Udalali wa magari au duka la nguo au simu.
3. Nyumba nzuri yakupanga
4. Ka gari kazuri. (Inategemea)
5. Pesa mkononi na kwenye mtandao wa simu. Mpesa, Tigo pesa nk. Bank hakuna ulazima sana
6. Hakosi vi hela vya bia za promosheni.
7. Pisi kali.
Kwanini Nyumba ya kupanga?
 
Back
Top Bottom