Kijana wa kisasa anatakiwa kuwa na vitu gani hasa!?

Kijana wa kisasa anatakiwa awe na yafuatayo.

1 Timotheo 4:12
"Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi."

Hapa (1Tim4:12) Mt.Paulo anatufundisha vijana Tuwe KIELELEZO katika USEMI (Kijana unapaswa kuwa na kauli njema, yenye kuvutia na Kumpendeza Mungu.. sio mijitusi, mala kuwa na kauli za kishetani, sio kusema Uongo, mara kauli za kuusifia uzinzi na ulevi hapana, Kauli yako kijana iwe Safi kwa Lugha ya staha), Lakini pia Kijana anatakiwa awe KIELELEZO katika MWENENDO (Mtindo wa maisha ya kijana kwanza Uwe wenye Kumpendeza Mungu, na kisha umvutie mwanadamu, uwe Mwema, Mpole, Mwenye Kiasi, Mpenda Haki n.k sio Mzinzi, Mlevi, Mchawi, Mgomvi, n.k), Lakini pia awe mwenye UPENDO (kwa watu wote), IMANI (Mungu pekee ndiye chanzo cha uhai na mafanikio ya haki, Mtafute Sana Mungu na Uyashike Maagizo yake), Mwisho kijana awe na USAFI (Kijana lazima awe safi Rohoni, Mwilini na Kwenye Fikra zake - Pureness)

Mengine yote ni ubatili.
Nimekuelewa Sana
 
(1)Awe na mfumo mzuri wa mawasiliano,simu nzuri ya smart phone yenye uwezo mkubwa.ikiwezekana na laptop awe nayo.
(2) Awe na chanzo cha fedha,iwe ajira au biashara.
(3) Awe na ari ya kufanya kazi kwa kijituma huku akijali mda na kuheshimu mambo aliyoyaorodhesha kwenye diary yake.
(3)Awe na uhusiano mzuri na wazazi wake.
 
Back
Top Bottom