Kijana, Kulelewa na mwanamke uwe mvumilivu

connections

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
2,177
3,005
Vijana wa mujini, wenyewe wanaita msingi kiuno, yaani unapata mwanamke mtu mzima kakuzimikia anaamua kukuchukua mkaishi wote kwake huku anagharamia bill zote ikiwemo kodi, umeme, maji, gharama za simu,nauli/mafuta & service ya gari n.k.

Lakini kwa namna wake zetu (nimeoa) walivyo na maneno ewe kijana nakushauri kama una roho nyepesi bora utafute pesa yako mwenyewe ili mtu asiwe anakusimanga (Kikinuka). Maana siku mmetibuana Bi. Mkubwa atatema "cheche" utukaniwe mpaka bibi yako (marehemu) aliyekufa kabla ya wewe kuzaliwa.

Yote haya ni ndani ya sekunde 60 tu. vijana tufanye kazi, tutafute vya kwetu.
UPDATE:
Hapo Zamani mambo haya hayakuwepo

cc. W-Si-Biii
 

Attachments

  • vijana.png
    vijana.png
    752.2 KB · Views: 377
Vijana wa mujini, wenyewe wanaita msingi kiuno, yaani unapata mwanamke mtu mzima kazimikia 6 packs zako anaamua kukuchukua mkaishi wote huku anagharamia bill zote ikiwemo kodi, umeme, maji, gharama za simu,nauli/mafuta & service ya gari n.k. Lakini kwa namna wake zetu (nimeoa) walivyo na maneno ewe kijana nakushauri kama una roho nyepesi bora utafute pesa yako mwenyewe ili mtu asiwe anakusimanga (Kikinuka). Maana siku mmetibuana Bi. Mkubwa atatema "cheche" utukaniwe mpaka bibi yake aliyekufa kabla ya wewe kuzaliwa. yote haya ni ndani ya sekunde 60 tu. vijana tufanye kazi, tutafute vya kwetu.
Pole kaka kwa yaliyokupata....natumain akina mjini msingi kiuno watajifunza hapa!
 
Ndugu yamekukumba yepi mpaka unatoa anagalizo hili? anyway, hata vitabu vitakatifu vinaagiza kuishi na mke kwa akili. So, yabidi kuwa na busara ya hali ya juu kabla ya kuchukua uamuzi wa kuishi na mke/chepuko/Gmama.
 
nilishawahi kutukanwa na mchuchu baada ya kuomba tutoke, twende club nikamuambia sina hela! daah aliporomosha matusi akaanza kumsifia ex-BF kuwa bora yeye alikuwa anamuhonga, daah! nilipata HASIRA+AIBU kwa pamoja. hawa vicheche wa kukutana nao mlimani city si wa kuwaamini kabisa.
 
Mpaka unafikia hatua ya kuishi na mwenza, kama mke na mume kunataka akili kupevuka na uwe (mwanaume) na chanzo cha pesa cha uhakika sustainable. Kutegemea pesa ya mwanamke ni kutafuta maneno (matusi) wakati wa mgogoro.
NB: Kinamama, mtusetiri pale tunapokuwa tumefulia badala ya kutuaibisha mbele ya umati.
 
There is always a price to pay for everything. Tatizo watu hasa vijana wanataka shortcuts tu. Hawataki kujibidiisha na kuumiza bongo zao ili kujikwamua kimaisha wenyewe.

Kwakuwa shortcuts mostly tend to be wrong cuts, basi ngoja waionje joto ya jiwe.

Otherwise, pole kwa yaliyokupata mkuu and I hope walengwa wamekusikia. Pia usisite kutumegea japo kidogo yale yaliyokusibu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom