Ewe mwanaume tambua kuna mke na mwanamke

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Tambua kuna mke na mwanamke ,makosa wafanyayo wanawake na kujikuta wameupoteza mwezi kwa ujinga wa kuhesabu nyota .


Kuwa makini ndugu yangu, maisha yasije yakakuchanganya ukachanganyikiwa na ukapotea ,maana kuna watu wanadata na kuvurugika akili kwa sababu ya maisha na tambua maisha ni changamoto kwa kila mmoja wetu ,Duniani hakuna kupumzika utapumzika ukifa ,JE UMEOA MKE AU MWANAMKE.?JE UMEPATA MME AU MWANAUME ,unaweza ukahisi umepata mke kumbee hapana umepata mwanamke ,makosa hufanya binadamu na siyo malaika ,kama ndoa yako imevunjika basi tambua uliyenaye hakuwa MKE bali ni MWANAMKE ,kama huna amani katika ndoa yako basi Tambua kwamba uliyenaye siyo mme bali ni mwanaume ,unaweza ukahisi umepata mme kumbee uliye Naye ni mwanaume na siyo mme ,acha kuishi kizembe angalia uliye Naye ni mke kweli ..!,jichunguze sawasawa je uliye naye ni Mme au mwanaume

Mke anaposhindwa kumtii mme wake anapoteza sifa ya kuwa mke anabaki kuwa mwanamke ,mke anapokuwa mbogo na mkorofi hata kama alikuwa mzuri na ameumbika VIP umbo lake linakuwa sawa na uchafu machoni kwa mwanaume na dunia kwa ujumla ,mke mwema siku zote ni mwenye hofu na mcha Mungu ,mke huwa hajibizani na Mme wake Bali anatakiwa awe na lugha mubashara na bashasha kwa mumewe hata kama Mme wake amepanda kiasi gani ,mke hatakiwi kuwa mbabe na mkali kupitiliza mke ameumbwa kuwa mpole na mnyenyekevu siku zote ,mke yoyote ambaye humdharau mme wake na kumsema vibaya au kwa kumvujishia siri Huyo siyo mke Bali ni mwanamke ,mke mzuri ni yule mwenye kifua cha kutunza siri ya ndoa yake pasipo kutoa nje ya ndoa yao , SIYO WANAWAKE WOTE WALIUMBWA KUWA WAKE HAPANA WENGINE WATABAKI KUWA WANAWAKE SIKU ZOTE .

Mwanamke mbishi na mbabe hawezi kuishi na kudumu katika ndoa ,mwanamke ambayee hambiliki wala hasikilizi ni ngumu kudumu katika ndoa yake ,mwanamke anaposhindwa kumuheshimu mumewe anapoteza utamu na ladha yake ya asili ,mwanamke mjuaji mbishi na mtata anapoteza sifa na anavaa sura ya kigaidi na kinyama machoni kwa mumewe na dunia kwa ujumla ,mwanamke hata awe mzuri vipi anapokosa heshima na utulivu anakuwa kama bango lilillobandikwa barabarani na kupigwa na jua ,mwanamke ambaye judge ni yeye ,mhukumu yaye ,mtuhumiwa ni yeye kila kitu anajua yeye , mwanamke wa namna hiyoo hata awe mzuri kama Cleopatra au Rita Ora au pengine kama Marie Antoinette anakuwa hana maana yoyote machoni kwa jamii anakuwa kama mchoro wa kuku aliyetolewa manyoya ,mwanamke anapaswa kuwa na adabu iliyotukuka ,mkimya mtaratibu mstahimilivu ,mvumilivu na mwenye kuheshimu watu wote wanamzunguka na siyo mvujisha siri za ndani ,siyo mpenda vita visasi na ugomvi ,siyo mruka njia anayeongozwa kwa tamaa Bali mtiifu na mwenye hofu ya Mungu ndani yake .

mke ameumbwa na kuagizwa utiifu na heshima kwa mwanaume na siyo vinginevyo ,tangu kuumbwa hii duniaa vitabu vitakatifu Quaran na Bilblia imewaagiza wanawake kuwa watiifu na wanyenyekevu pamoja na kuheshimu waume zao ,hii imeandikwa katika vitabu vyote na watumishi wa Mungu pamoja na mashekh misikitini na viongozi wengine wengi kutoka tamaduni mbalimbali duniani kote wamekuwa wakihubiri hivo sasa mwanamke unapoyapuuza hayo na kufuata usasa na kujifanya simba mla nyasi unakuwa umekwenda nje na kinyume na matakwa ya vitabu vitakatifu na unapoteza automatically utamu na uzuri wako na kubaki kama mchoro au picha ambayo imebandikwa ukutani isiyokuwa na maana yoyote ile .

Makosa yanayofanywa na wanawake na kujikuta wamechezea shilling chooni ,Kuna kundi kubwa mtaani la kina dada na wakina mama wenye umri wa miaka 28-35 na kuendelea ambao wengine wameachwa na mabwana zao , wengine wamekimbia shida , wengine wamedanganywa , wengine hawajaolewa kwa sababu bado hawajapata wanaume ,wengine wameamua kuwaacha waume zao na kwenda kuishi maisha yao ,wengine hawajawapata wanaowataka , wengine hawapati mabwana kwa sababu wanaishi maisha feki ambayo siyo yao , ni vyema pia maana wengine baada ya kugundua umri umeenda wanaamua kujikita kwenye biashara na kujijenga kiuchumi kitu ambacho ni kizuri na ukienda katika majiji makubwa kama Dar-es-Salaam ,Mwanza ,Arusha ,Mbeya na maeneo mengine kuzunguka nchi utakutana na wakina Mama wazito wanafanya biashara zao ,wana majumba na Mali za kutosha ni baada ya kuona ndoa kwao ni kikwazo hivyo wanaamua kujikita katika biashara na ni baada ya kugundua mwanaume hawezi kutoa kila kitu hivyo wanaamua kupambana kujitafutia kipato .

mwanaume anakuletea ndizi roast na mihogo ya kuchoma unamwambia nani amekwambia mimi nakulaga mihogo vyakula vya kuku,unaniletea mihogo kwani Mimi ngo'mbe kwanza unanionaje sipo kwa ajili ya kuteseka kama umeshindwa kunihudumia sema , mimi nakulaga bhaga na pizza nyama choma au chips kuku ,tayari hapo unaishi maisha ambayo siyo yako , mwanaume anakwambia agiza chakula wewe unaaigiza chakula kama vile mko vitani ,unaagiza chakula cha 30000 au 25000 na vinywaji inakuja kama 30000 hapo ni wewe mwenyewe tu bado mwanaume hajaagiza na hapo hujaolewa bado ni wapenzi ukiendelea na tabia hiyo hutaolewa utajikuta unafikisha miaka 28-35 bado unadanga na kuendelea kutumika maana hakuna kijana mwenye miaka 28-35 mwenye umri kama wako atakaye kuoa wewe maana kimsingi unakuwa umepoteza sifa na mvuto wa asili .

Hakika umri mzuri wa mwanamke kuolewa ni miaka 18-24 kwa kijijini na kwa wale ambao hawajaenda shule , mjini pia ni miaka 24-26 maana katika miaka hiyo unakuwa katika ubora wako , pia mwanamke mwenye miaka 27-35 tayari amekanyaga msitari mwekundu na ule mvuto wake unakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa na kuolewa kwako inakuwa ni ngumu sana na kupata tu mwanaume wa kumhudumia bado inakuwa ni kikwazo kwake na kwa lugha nyepesi binadamu uwezi wake wa kuzalisha unapungua kadri umri unavyozidi kwenda na ndiyo maana ni vyema ukafanya vitu kama kijana maana kadri miaka inavyokukimbia ndivyo uwezo wako na ufanisi katika ufanyaji kazi wako unapungua .

Unataka kuolewa na mwanaume mwenye pesa na majumba mbona mpaka leo hujampata ..?cha msingi tambua mwanaume wa kweli hutengenezwa na mwenye jukumu LA kumtengeneza ni wewe mwanamke ,ukishindwa ukatoa boko lazima mwanaume wako atakuwa boko, Unaposema unataka mwanaume mwenye mali zake embu kwanza hao wanaume wenye pesa mtaani kwenu wako wangap ..? Wanaume wenye pesa unao wataka wewe wengi wana miaka 50 na kuendelea na wewe una miaka 25-30 , ok inawezekana hujanielewa vizuri ikoo hivi dada zangu hakuna kijana kuanzia miaka 25-35 mwenye majumba na pesa maana pesa kama wapo basi za wazazi wao na kama wapo ambao wana majumba na magari ya kifahari basi ni wachache mno mtaani na kama ukabahatika kuwaona basi tayari walishaoa wako na familia zao .

Tatizo kubwa la kina dada na baadhi ya kina mama wanaishi maisha ambayo siyo yao , maisha maisha ya kuigiza afu unataka mwanaume wa kweli ,wanawake wengi wa kizazi hiki wanapenda kuishi maisha ya watu wengine na hii ni hatari kwao maana wanajikuta wanachelewa kuolewa na wengine kuachika na ndoa zao kufunjika vunjika , wanawake wenye umri wa miaka 20-30 , wengi wanafata mkumbo , wengi wanashindwa kuishi maisha yao maana wanaishi maisha ya watu wengine , mtu kaolewa kaona mambo hayaendi anaamua kuachana na mme wake kisa kaona mbona fulani kaachana na bwana wake kwani mimi nikiachana na bwana wangu kuna shida gani ..?? Anasahau kwamba mda umekwenda , anasahau kwamba umri unasonga na kumpata mwanaume anayeeleweka siku hizi ni ngumu mno maana kulingana na ugumu wa maisha wanaume wengi wamebaki na mikonyonyo yao kwenye suruali zao lakini kimaisha hamna kitu yaani hawana wa kujimudu wenyewe , wanamalengo lakini imeshindikana ivyo wamebaki kubeti , na ukiwapata wenye pesa atakutumiaa kama mbwa koko , sikipingi wala sikutishi ila hapa namaanisha kama mwanamke kuelekea mafanikio yako lazima uwe makini na mwanaume wa kweli mjini kwako wewe mwanamke ni kazi yako .

Ulisema unataka mwanaume atakaye kujali na kukuheshimu mpaka leo ujampata tuu , ulisema unataka mwanaume kibopaa mwenye nyumba na kazi zake vp mbona wapo wengi lakini mpaka sasa hujaolewa ..?ni kwa sababu ya wewe mwenyewe hueleweki ,mwanamke unajitutumua na kujishauwa utafikiri uko peke yako katika hii dunua ,ngebe zako ,uchangu wako ,mashauzi yako ,kudanga kwako ,upuuzi umekujaa kichwani afu unataka kuolewa na atakuoa MTU mwenyewe uko bize kama YouTube na unachokifanya haikionekani kabisa , kamaa vijana tunakumbushana nakupa sumu itayokusaidia kumua nyoka mwenye sumu , uwe mdada au kaka tambua hakuna atakayekuja kukutengenezea maisha , hakuna atakaye fanya kazi ya kukuhudumia maisha yako yote , hakuna mtu wa na namna hiyo hivyo basi maisha yao utayatengeneza mwenyewe , maisha ni zawadi tumepewa ukiharibu sawa ukiitunza itapendeza zaidi.

Ukitaka watu wakupe kila kitu kubali kuwa mtumwa wao , ukitaka mwanaume mwenye pesa hutampata na ukimpata mwisho wako utakuwa ni chumbani na getini , ukipenda kula vya watu hovyo na wewe kubali kuliwa vile vile , ukiona una miaka 28-35 na bado hujaolewa na hujapata mwanaume unayemtaka basi jiangalie vizuri na ujitathimini wapi unakosea wapi unapungukiwa na ukiona hivyo una miaka 30 na hujaolewa usitegemee utampata yule unayemtaka wewe na usitegeme utampata kijana mwenzako kama wewe hapana lazima utaolewa na mwanaume mwenye umri kuanzia miaka 38 mpaka 40 ambaye na yeye ni yule ambaye alioa akaachika na tofauti na hapo labda wewe ndo umuoe mwanaume kwa mwanamke umri ukisogea sana inakuwa ngumu kumpata mwanaume anaye mtaka.

Wanawake wanakua haraka na kupevuka haraka sana lakini piaa wanachoka na kuzeeka haraka hivyo hivyo, ujumbe wangu kwenu dada zangu kuanzia miaka 28-35 ambao bado kuolewa kwenu ni kitendawili , ukiona umekosa mwanaume mwenye pesa basi tafuta za kwako , ukiona umemkosa mwanaume mwenye majumba basi tafuta kujenga nyumba yako , ukiona umekosa mwanaume mwenye elimu basi soma wewe , kumbuka nazungumziaa juu ya maisha ni umri na hakuna mchawi wa maisha yako ila mchawi ni wewe mwenyewe usipende kuchagua chagua sana maana mchagua nazi upata koroma , kutamani vitu ambavyo hujavitolea jasho ni kosa kubwa sana yaani ni sawa na kuchomeka simu chaji wakati umeme umekatika , unatumiaje umri wako kwa maisha ya baadae , haijalishi wewe ni wa kiume au wa kike ni mazingira gani unandaa kwa ajili ya kesho yako .

Kuna namna nyingi sana ya kushiriki katika chakula cha jioni au cha mchana , unaweza ukashiriki kama muhudumu au unaweza ukashiriki kama chakula kinachotakiwa kuliwa ama unaweza ukashiriki kama mlaji wa chakula hicho , chagua moja unataka kuwa nani katika maisha yako , unataka kuwa msimamizi wa chakula kinacholiwa...? Au unataka kuwa chakula kinacholiwa , au unataka kuwa muhudumu wa chakula chagua unataka kuwa upande gani ...? Katika haya maisha ya ujana kuna ambao wanakuwa wasindikizaji na hawa mara nyingi hutumika na watu fulani ili kuyafikia malengo yao , kuna watu wapo kwa ajili ya kutumika tu na hawalitambui hilo kwamba wanatumika ,kuna watu piaa wapo kwa ajili ya kuwatumia wenzao ili wafikie malengo yao chukua hatua na ujitathimini uko upande gani..??

kuna wengine wapo tu na wamekubali kutumiwa na watu wengine maana wagumu ndiyo wanaodumu, chagua upo wapi ..?? Chagua unataka kuwa nani ..? Jitafakari vyema juu ya malengo yako rafiki yangu james mtafungwa ananiambia haya maisha ni marahisi mno yani ni kama vile unateremka kwenye mpera au mpapai yaani ni suala LA kugusa hapa na kuacha kule, "only the strong will survive the weak will never survive " Darwinism theory , katika maisha kuna kupanga na kuchagua , katika maisha wenye nguvu tu ndiyo watakao kuwa salama , watu wenye kupanga na kusimamia mipango ipasavyo hao ndiyo watakao toboa kimaisha , watakao pambana mpaka mwisho bila kuchoka ata tamaa hao ndiyo watakaofikia malengo yao lakini wavivu , tayari u wasiojua kucheza na refa naotumia mda wao mwingi kulala na kujipwaale ambao wanawekeza kwenye sura na kwenye makalio, wale ambao wamewekeza kwenye happbirthday nanguo , wale mnaowekeza kwenye mapenzi na majungu na uchawi , wale wanaowekeza kwenye mawigi waliowekeza kwenda club,wale wanaowekeza kwenye kudanga kutoboa kwao kiuchumi ni ngumu labda watoboe mabox na makopo lakini siyo kimaisha isipokuwa .
 
Du, hadithi ndefu namna hiyo, nimefanikiwa kuisoma aya moja tu ya kwanza. Umesema “Duniani hakuna kupumzika utapumzika ukifa, hiyo itategemea ulijiandaa vipi ulipokuwa Duniani. “Je, umeoa mke au mwanamke”, huoi mke bali unaoa mwanamke ambaye baada ya hapo anakuwa mke!!
 
Mkuu somo zuri ila ungeweka wasichana hapo badala ya wanawake maana wanawake in my opinion ni better level/top choice/ top experience na wasichana ndo hawa wasiojitambua yan bado akili zimelala aka mapopoma
 
Kama huwezi kupanga na kusimamia mipango kisawasawa huji kutoboa kamwe ndo nilichosoma
 
As if mke ni mwanaume, na mwanamke hawezi kuwa mke...


Mkuu, majority tuna stress, habari ndefu ni kupewa maji ilhali huna kiu
 
Sijawahi kukutana na maelezo marefu kama haya JF, hata ukiamua kututolea mtihani tutafeli.

Kibaya zaidi hujatupia hata picha moja ya kutushawishi kusoma. Bora ungeandika kitabu mkuu, ukauza nakala, badala ya kuandika uzi.
 
Punguza mkuu
FB_IMG_1536380013803.jpg
 
Mkuu umenena vyema kabsaaa somo zuri kwetu wanawake....nimependa pale pakuwa upande gani wa chakula ,mhudumu or kuwa chakula au kuwa mlaji .....
 
wengi watasoma huu uzi kama hadithi.....but hili ni somo zuri sana kwetu sote...na sisi wazazi tunawaandaaje watoto wetu? asante mleta uzi......wataelewa tuu.....
 
Back
Top Bottom