nashukuru mzima
JF-Expert Member
- Jul 11, 2017
- 1,014
- 1,896
Habari,
Kujitolea katika Serikalini au kwenye private kwa sasa imekuwa ni ugonjwa mkubwa sana nchini.
Baada ya Uhaba mkubwa wa ajira nchini, kumekuwa na wimbi la Hali ya mashirika,taasisi za umma na binafsi kuhitaji watu wa kujitolea kwenye sehemu za kazi.
Kiuhalisia kujitolea sio jambo baya kwa sababu ni jambo ambalo linaleta uzoefu mkubwa hasa kwa Fresh graduate na uzoefu kama ilivyokuwa ikifanyika miaka ya awali.
Ila kwa sasa suala la kujitolea limefanywa kama ni aina fulani ya ajira rasmi yenye lengo la kuwanyonya wanaojitolea.
Kwanza kabisa nafasi za kujitolea kwa sasa zinafuata utaratibu wote wa ajira kuanzia kutangaza, kuita watu kwa usaili, kupata watu katika nafasi zinazotakiwa na kuwaingiza kazini.
Ila Watu wengi wanaojitolea pindi wanapoingia makazini wanakutana na mambo kadhaa.
Kwanza Posho/Mshahara mdogo usiokuwa na hadhi hata kidogo ya thamani ya Elimu, yake ukubwa wa majukumu na muda anaotumia kazini unakuta mtu amesoma Account ilibidi alipwe million 1.2 labda ila kwenye kujitolea atalipwa laki 2 na hela inakuja kwa kuchelewa.
Pili Unyanyasaji mkubwa sana katika maeneo ya kazi baina ya wafanyakazi waliojiriwa tayari na wakuu wa Sehemu hizo za kazi wanawanyanyasa sana Wanaojitolea na kuwaona hawana thamani yoyote uonesha kwa vitendo na kwa kusema kabisa.
Tatu Wanaojitolea hawapewi Mikataba yenye kuonesha hali ya matibabu itakayofanyika pindi watakapoumwa, hela ya kujikimu, overtime, ruhusa wala likizo.
Waajiri wengi wanapowachukua Volunteer huwadanganya kwa kuwaambia mkijitolea kwa muda mrefu mtapata ajira ya kudumu suala ambalo utekelezaji wake mdogo.
Hitimisho: Serikali inatakiwa iweke jicho la Tatu kwenye hili suala