Nilishangazwa sana na jinsi mapolisi walivyomchukua kijana wa watu aliyetaka kuwasilisha yanayomsibu na mwenge, alichukuliwa na kuaanza kupigwa mbele ya Rais na halaiki nyingine nikajiuliza hivi kwa nini polisi wamefundishwa kupiga tuuuu hata kama suala lenyewe sio la kupiga. Watanzania wengi kwa kweli wanahoji huo mwenge unafaida gani kwa jamii badala yake tunapata majibu mepesi sana kutoka kwa watu wenye kukoumbatia huo mwengi bila justification yenye mishiko, hivi kweli mwenge unaunganisha watanzania?, unalete amani?. Kufungua gesti house za watu binafsi ni maendeleo ya mwenge? mimi pengine ni mbumbumbu wa maendeleo lakini kwa uelewa wangu mwenge ulitakiwa uwekwe makumbusho angalau watu wanaweza kutembelea na kulipia pesa ambayo itasaidia kwenye uchumi.
Hivi mlishawahi kuwasikiliza wakimbiza mwenge walivyo wanasiasa wanapoongea na wananchi