Kiinua mgongo nssf, ikoje hii?

kisute

Member
Oct 6, 2010
54
3
Wana janvi, naomba msaada wenu hapa. Malipo yatolewayo na NSSF kama kiinua mgongo baada ya kutimiza miaka 15 na zaidi ya uanachama hutolewaje? Je, Mwanachama huchukua malimbikizo yake yote kwa pamoja? Mfano; nimechangia Tshs 40,000,000 hadi sasa ndani ya miaka 16. Nimeacha kazi au kuachishwa nitalipwaje?
Nitalipwa fedha hiyo taslim then kiinua mgongo au inakuwaje? Msaada tafadhali kwa waelewa. Nawakilisha.
 
Unatakiwa uwe umechangia kwa miaka 15, then uwe umetimiza umri wa kustaafu (yaani miaka 55 kwa hiari na miaka 60 kwa lazima)! Hata hivyo endapo umeanza kazi kabla ya Julai 1998 michango ilikuwa haihesabiki kama credit moja ya uchangiaji kama ilivyokuja kuhesabika baada ya hapo (kuna fomula ya kufanya convertion-wasiliana na NSSF kwa hili)! Pia kama umeacha kazi kazi kabla ya umri wa kustaafu na umechangia michango kwa miaka 15 au azidi utalipwa Special lump sum ambayo inakokotolewa kwa kuangalia mchango wa mwisho ukizidishwa na idadi ya michango. Ushauri wangu ni kwamba kama umebakisha muda mfupi kufikisha miaka 55 tafuta pa kujishikiza ili uendelee kuchangia ili mwisho wa siku uwe pensionable! Wishing you all the best!
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako.
Je ikiwa bado hujafikisha miaka hamsini inakuwaje?
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako.
Je ikiwa bado hujafikisha miaka hamsini inakuwaje?[/QUO

ili upate sifa ya kulipwa pensheni lazima uchangie kwa miaka 15 na ufikie umri wa kustaafu 55-60.kama hujafika umri wa kustaafu utalipwa withdrawal benefit.ambapo utapewa contributions zako zote let say 40 m kama ulivyospecify hapoo juu pamoja na interest.ukifikisha umri wa kustaaafu ila muda wa kuchangia haujafika miaka 15 au zaidi basi utalipwa specila lump sum formuler yake ni total no of credits(miezi uliyochangia)X mchango wa mwisho.
 
Je interest hiyo ni % ngapi? Let's assume umechangia kwa miaka 10 kamilifu..
 
Back
Top Bottom