Waziri Ngeleja amvutia kasi Makamba
Send to a friend Wednesday, 09 February 2011 21:31 0diggsdigg
Ramadhan Semtawa
SIKU moja baada ya kuvuja waraka mzito wa Mbunge wa Bumbuli January Makamba kutaka ufafanuzi wa hali ya umeme, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema tayari ameusoma, lakini serikali haijatoa majibu Bungeni na kwamba atamjibu mwenyewe.
Msimamo wa serikali, unazidi kuua mipango mikakati ya kuirejesha bungeni hoja ya Dowans na Richmond kwa mlango wa nyuma, baada ya ofisi ya Bunge kukataa hoja ya Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, kuhusu hali ya umeme na hukumu ya ICC.
Waraka wa Makamba pamoja na mambo mengine, umeibua jambo zito kwa kumwanika mwanasheria mmoja wa Tanesco aliyesimamia kesi ya Dowans, ambaye alishauri mkataba dhidi ya kampuni hiyo, uvunjwe na upande mwingine akiisifia na kuiombea mkopo wa Sh 20 bilioni kutoka Benki ya Stanbic.
Akizungumzia waraka huo, jana kwa njia ya simu kutokea Dodoma Ngeleja alisema hajausoma waraka huo.
"Jana (juzi) sikuwa nimeisoma hiyo, barua, lakini sasa hivi nimeisoma, Ninachoweza kusema ni kwamba tutamjibu yeye mwenyewe," Alisema Ngeleja.
Waraka huo, ulosomeka hivi ‘Yah: Taarifa ya Serikali Bungeni kuhusu Umeme Nchini,' Mbunge Makamba ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM, anataja mambo mawili makuu ya msingi, ambayo ni kesi mbili za IPTL zilizopo Hong Kong dhidi ya serikali na mgongano wa mawaziri kuhusu Dowans, ambapo alimtaka waziri afafanulie umma kupitia bunge.
"Kesi hizo ni ICSID No ARB/10/20, dhidi ya Tanesco iliyofunguliwa Oktoba mosi, 2010 na ICSID No ARB/10/12 dhidi ya Jamhuri ya Muungano, iliyofunguliwa Juni 11, 2010, zinaweza kuwa na madhara makubwa kwa umma na zinaweza kuigharimu serikali fedha nyingi kuliko zinazodaiwa katika kesi ya Dowans," alifafanua Makamba.
Lakini, Ngeleja akifafanua zaidi, alisema mbunge huyo ameomba taarifa kwa waziri kwa mujibu wa barua yake, hivyo kitakachofanyika ni kuandaa majibu na kumpatia mwenyewe.
"Tunaandaa majibu na tutampatia mwenyewe, aliomba majibu kwangu nikiwa ni waziri na pia kutoa ushauri, hivyo utaratibu wa kiserikali ni kumjibu yeye mwenyewe na wala si kuzungumza na vyombo vya habari," alisisitiza Ngeleja.
Kwa mujibu wa Waziri Ngeleja, amekuwa akipokea ushauri kutoka kwa wabunge wengine ambao wanataka ufafanuzi wa mambo ambayo, amekuwa akiwajibu katika utaratibu wa mawasiliano.
Ngeleja akizungumzia tuhuma za mwanasheria huyo, aliyecheza karata pande mbili za Tanesco, Ngeleja alisema;"Hilo liko nje ya uwezo wangu. Waulizeni Tanesco waseme wenyewe, kwasababu siwezi kuwasemea. Hilo liko nje ya uwezo wangu," alisema Ngeleja.
Meneja Uhusiano wa Tanesco Badra Masoud alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo, hakuweza kupatikana na simu zake za viganjani hazikuwa hewani.
My Take:
Wanamuachia JM options mbili tu... both not very appealing..