Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,756
- 40,930
Baada ya kufuatilia habari nyingi na majadiliano mengi kuhusu mambo mbalimbali nimegundua kuwa wengi wetu hatuna habari sahihi, na hoja zetu nyingi zinatokana na kushuku na kusikia bila kuwa na habari sahihi za kile kinachozungumzwa. Ni vigumu kupata habari toka serikalini kwani vikwazo ni vingi sana; huwezi kusoma mkataba fulani hadi uwe unahusika katika utekelezaji wa mkataba huo, huwezo kupewa habari kwani "msemaji" hayupo, n.k Ndugu zangu tatizo ni kuwa hatuna sheria inayolazimisha vyombo vya serikali (wizara, idara, mawakala nk) watoe habari kwa raia.
Ni kwa sababu hiyo basi inakuwa vigumu sana kupata habari sahihi na zisizofichwa fichwa. Leo hii ukitaka kuona mikataba ya madini, nishati n.k huwezi kupewa kwani ni ya siri! Kinachoudhi zaidi ni kuwa wabunge wa Upinzani ndio wanaonekana wakisema mambo ya maana bungeni na kuhoji mambo ya msingi!! Hivi wabunge wa CCM wanakilisha watu gani? Hivi haiwaumi wao malalamiko ya wananchi!! Hivi wote ni waoga hakuna wale waenda peke (mavericks)?
Ninachosema ni kuwa wakati umefika Bunge badala ya kuomba taarifa toka serikalini, au kwa viongozi wa serikali litunge na hatimaye sheria ipitishwe yenye kulazimisha vyombo vya serikali kutoa habari kwa uhuru kwa wananchi bila kuficha vingevyo chombo hicho kinatozwa shilingi milioni 10 kwa kila siku inapochelewa kutoa taarifa hiyo, na viongozi wake wanatozwa laki moja kwa kila siku wanachelewa kutoa habari hizo! Sheria hii ijulikane kama "Sheria ya Uhuru wa Habari". Hii italazimisha mikataba kujulikana na kuwekwa wazi, itatufanya tujue nani amefanya nini na wapi, itatusaidia kutambua ni wapi kwenye udhaifu! Ama sivyo tutaendelea kuota, na kuombea watuonee huruma na kutupa habari!!!!